Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Mgogoro wa Zanzibar watinga Ikulu ya Marekani

Unadhani Marekani wataifanya nini Tanzania kama imeamua kurudia uchaguzi wa Zanziabar? Yaani hujui maana ya nchi huru? Kila siku kulialia kwenye mataifa ya magharibi kwa vijitatizo vidogo vidogo?

Hapa sio kuwa Zanzibar imepinduliwa. Tume yao wenyewe (ZEC) imefuta uchaguzi na kutaka urudiwe. Marekani wanaambiwa hili ili wafanye nini?

Hivi haya mawazo ya kitumwa jamani bado wengine wanayo tu?

Suala LA Zanzibar ni vitatizo vidogo vidogo!
 
Chini ya CCM daima hatuwezi jitawala.Kujitawala kwatakiwa kujiamini na kujiamini kwatakiwa kujitegemea.% kadhaa ya bajeti ya nchi hii yategemea wahisani na wafadhili, huku serikali ya CCM ikiwekeza raslimali zetu kwa masharti nafuu, matokeo yake twabaki kuwaomba haohao misaada. What d'you expect?Ubinafsi umetutawala.Hayo masharti nafuu ya uwekezaji ni kwa ajili ya kupata 10% halafu twalalamika.Kwa ajili hiyo ushindi kwa CCM ni lazima vinginevyo hizo 10% hazitakuwepo.Na maarifa ya kushinda tunayo hata ikibidi kwa goli la mkono,pia hatuwezi kabidhi nchi kwa makaratasi.

Mimi sio mwanachama wa CCM, CUF, CDM, nk. Non-partisan. Mimi naipigia debe Tanzania na maendeleo yake. Haya maendeleo tutayaleta sisi wenyewe. Ukitegemea kulialia Uingereza, Marekani, Ujerumani, hutapata chochote cha maana. Watakutupia pumba (masalia) yao tu wakisha kula na kushiba.

Matatizo ya Tanzania ni jukumu letu wenyewe kuyatatua. Siasa ni siasa. Angali uchaguzi wa mwaka huu. Kama UKAWA wasingefanya ule ubaradhuli wao na kumleta Lowassa, Sumaye, Kingunge ndani ya UKAWA sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine kabisa. Na wala usijaribu kuniambia eti CCM iliiba kura bara.

Kilichopo mbele yetu sasa ni kutatua mgogoro wa Zanzibar. Maalim, Dr. Shein, marais wastaafu wa Zanzibar, pamoja na wasuluhishi wa UN, AU, EU wamejikita kulifanyia kazi hili. Tuwape nafasi wafanye kazi yao. Sisi wengine (au nijisemee mimi) maamuma wa siasa na katiba tungekuwa na subira.
 
Ccm itakapokaa benchi

Nakubaliana na wewe.

Ili siasa ikomae Tanzania ni muhimu CCM ije ipumzishwe kwanza. Bila ya hivyo hivi vyama vingine vitakomaaje?

Lakini kabla upinzani hauja weza kutwaa dola lazima wakue kwanza kisiasa. Haya mambo ya kubadilisha gia angani na kutia oili chafu (Lowassa) kwenye chombo siku zote chombo kitaangamia. Unajua kama UKAWA wasingefanya yale madudu ya kumleta Lowassa leo hii tungekuwa tunazungumzia serikali tofauti sana. Najua UKAWA wanajiaminisha kuwa usemi huu sio sahihi lakini mimi sikubaliani nao.

Kosa lile la UKAWA litaugharimu upinzani kwa muda mrefu sana kwa sababu sidhani kama kuna mtu anaeweza kuigusa CCM tena mpaka 2025.
 
Suala LA Zanzibar ni vitatizo vidogo vidogo!

Ni tatizo dogo tu. Imma Dr. Shein akubali Maalim awe mshindi, au uchaguzi urudiwe.

Sasa hivi wanaendelea (Maalim, Dr. Shein, wasuluhishi wa UN, EU, AU, na marais wastahafu) kufanya majadiliano. Hapa ukubwa wa hili suala uko wapi? Mahasimu wamekaa na wanajadiliana hapo si ndio mwanza wa kupata suluhisho? Hivi hili haliwezekani?

Mbona watu mnataka kukuza mambo madogo ili yawe makubwa? Au lengo lenu ni kuleta machafuko visiwani ili azma zenu nyingine zitimie? Acheni fitna nyie.
 
Mimi sio mwanachama wa CCM, CUF, CDM, nk. Non-partisan. Mimi naipigia debe Tanzania na maendeleo yake. Haya maendeleo tutayaleta sisi wenyewe. Ukitegemea kulialia Uingereza, Marekani, Ujerumani, hutapata chochote cha maana. Watakutupia pumba (masalia) yao tu wakisha kula na kushiba.

Matatizo ya Tanzania ni jukumu letu wenyewe kuyatatua. Siasa ni siasa. Angali uchaguzi wa mwaka huu. Kama UKAWA wasingefanya ule ubaradhuli wao na kumleta Lowassa, Sumaye, Kingunge ndani ya UKAWA sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine kabisa. Na wala usijaribu kuniambia eti CCM iliiba kura bara.

Kilichopo mbele yetu sasa ni kutatua mgogoro wa Zanzibar. Maalim, Dr. Shein, marais wastaafu wa Zanzibar, pamoja na wasuluhishi wa UN, AU, EU wamejikita kulifanyia kazi hili. Tuwape nafasi wafanye kazi yao. Sisi wengine (au nijisemee mimi) maamuma wa siasa na katiba tungekuwa na subira.
 
Attachments

  • 1448444664770.jpg
    1448444664770.jpg
    99 KB · Views: 219
GHIBUU

Haya ndio majadiliano na ushauri mzuri kutoka marafiki zetu na ni muhimu kuuzingatia. Ningependa pia kuona nchi za kiAfrika zikitoa nasaha zao kuhusu huu mgogoro wa Zanzibar.

Kitu kimoja kinabaki palepale. Suluhu ya matatizo yetu tunayo sisi wenyewe (hasa waZanzibari). Sio Uingereza, sio Marekani, Japani, China, Urusi, la! Sisi waMatumbi wenyewe. Acheni kuweka macho na masikio yenu juu juu mkisikiliza mataifa ya magharibi yanasema nini. Tujifunze kutatua masuala yetu sisi wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
U

Tatizo la waafrica tume kufa ki serological, yaani bado tunaongozwa na wazungu, zanzibar na tanganyika bado ni makoloni ya wazungu, ndio maana nchi zote zilizo tawaliwa na queen wa UK zinaitwa common wealth country, sisi watanzania hapa UK tuna right sawa na waengereza wenyewe katika kuchagua viongozi, kwa mara ya kwanza nilipiga kura mara hii, kama mtanzania, nikafuatilia. Zaidi kujua sababu ya kuwa na haki ya kupiga kura ni kwa sababu natoka koloni la mwengereza.

Nimeamini kwamba bado kweli tupo kwenye himaya yake, hawa ndio wenye nguvu, viongozi wetu ni TV tu, remote zipo huku.

Hivyo kuwaomba wao kututatulia matatizo yetu wao ndio wenye power zaidi katika kuwaamrisha viongozi nini wafanye.
http://www.electoralcommission.org....-is-eligible-to-vote-at-a-uk-general-election
 
Last edited by a moderator:
U

Tatizo la waafrica tume kufa ki serological, yaani bado tunaongozwa na wazungu, zanzibar na tanganyika bado ni makoloni ya wazungu, ndio maana nchi zote zilizo tawaliwa na queen wa UK zinaitwa common wealth country, sisi watanzania hapa UK tuna right sawa na waengereza wenyewe katika kuchagua viongozi, kwa mara ya kwanza nilipiga kura mara hii, kama mtanzania, nikafuatilia. Zaidi kujua sababu ya kuwa na haki ya kupiga kura ni kwa sababu natoka koloni la mwengereza.

Nimeamini kwamba bado kweli tupo kwenye himaya yake, hawa ndio wenye nguvu, viongozi wetu ni TV tu, remote zipo huku.

Hivyo kuwaomba wao kututatulia matatizo yetu wao ndio wenye power zaidi katika kuwaamrisha viongozi nini wafanye.
Electoral Commission | Who is eligible to vote at a UK general election?

Nakubaliana na wewe. Pia nimeona urahisi wa kujiandikisha na kupiga kura Uingereza katika hii tovuti uliyoiambatanisha.

Najua waTanzania bado tuna kasumba ya kukimbilia kwa wakoloni wetu watutatulie matatizo yetu. Mimi nitapigana na fikra hizi potovu mpaka pumzi yangu ya mwisho. Lazima tujiamini. Kuna vitu ambavyo vipo katika uwezo wetu kuvitatua. Ndio kukua kwenyewe huko.

Haya, ngoja tuone busara za hawa viongozi wanaojadiliana zitafikia wapi. Hapa ndipo nitakapojua kama tumekomaa kisiasa au hapana.
 
Kifyatu

Unaweza kulinganisha kati ya Marekani na Tanzania? Ni lini USA ilishawahi kuomba misaada Tanzania? Halafu kikwete ameenda USA zaidi ya mara 20, yeye Obama alikuja mara ngapi hapa?
Hauna ajili kabisa. Mali zinazoendwleza marekani zinatoka wapi???? Uchumi unapanda kwao unapandishwq na Mali za wapi? Ni dhahabu zetu za Geita na Alma's na tanzanite. Uwiiiiiiiii soma ustaarabike inauma Sana ukijua
 
CCM wanasema busara zinatumika 'kutatua mgogoro wa Zanzibar'......vichekesho vya mwaka...Kuna busara gani zaidi ya kukubali matokeo kuwa wameshindwa uchaguzi?

Kama kuna mgogoro ni huo uliotengenezwa na CCM baada ya kushindwa uchaguzi Zanzibar.....Rasilimali zinapotea bila sababu za msingi 'kutatua mgogoro' ambao ni UJINGA wa CCM....

Tamko halitoshi bila utekelezaji, Jumuiya ya kimataifa inaombwa ishinikize serikali ya Magufuli 'kutatua mgogoro' wa Zanzibar haraka iwezekanavyo.....Wazanzibari wapate wawakilishi wao na Rais wao mpya (Seif).....

Hahahahah ccm wanajitekenya alafu wanacheka wenyewe,,,,
 
Unadhani Marekani wataifanya nini Tanzania kama imeamua kurudia uchaguzi wa Zanziabar? Yaani hujui maana ya nchi huru? Kila siku kulialia kwenye mataifa ya magharibi kwa vijitatizo vidogo vidogo?

Hapa sio kuwa Zanzibar imepinduliwa. Tume yao wenyewe (ZEC) imefuta uchaguzi na kutaka urudiwe. Marekani wanaambiwa hili ili wafanye nini?

Hivi haya mawazo ya kitumwa jamani bado wengine wanayo tu?

Uhuru gani unaojivunia nao? Uko huru wakati unaenda kuomba hela za millennium kwao
 
Tume imefuta uchaguzi baada ya jeshi la kivamizi la Tanganyika JWTZ kuzingira kituo cha matangazo na kuondoka na mwenyekiti wa tume ambaye record ya video ya kuufuta uchaguzi ilionyeshwa kwenye tv .

Mpaka wakati huu Mwenyekiti wa Tume yuko chini ya ulinzi wa WAVAMIZI kutoka Tanganyika
Sijaona kitufe cha like mkuu, maana kuna watu wanuona ukweli lakini hawataki kuusema, SMZ haina amri juu ya jwtz Bali ni kutoka magogoni Tanganyika,waliweka effort Kubwa kuchakachua humu hadi kuwakamata wale vijana waliokuwa wanajumlisha kura za urais za UKAWA wakasahau Zanzibar kushtuka Maalim keshajumlisha kura zake wakatuma jeshi kwa Jecha, walaaniwe wanaoongoza jeshi la CCM. Si la wananchi kwani linatumiwa dhidi ya wananchi
 
Sioni point ya wao kwenda White House USA.
Marekani washatoa tamko inatosha kabisa, walichokifanya hawa jamaa ni pointless na very stupid.
Inazidi kuonyesha wabongo jinsi gani kichwani hazimo, siamini wamekaa wakakubaliana kabisa ati wakaandamane white house ya US..

It is stupid kwenda white house,and it is very clever for CCM to do what they have done in Zanzibar. Kweli wabongo hazimo ila nyinyi ambao zimo mnakubaliana na mchezo mchafu wa ccm
 
Nani kawashikia waZanzibari mtutu kichwani kuwa uchaguzi ukirudiwa leo wasipige kura walivyofanya awali?

Mimi sijui sheria na KATIBA ya Zanzibar lakini nijuavyo mimi ni kuwa tume ya uchaguzi, ZEC, imesema imeona madudu kwenye uchaguzi uliopita na imetaka uchaguzi urudiwe.

Kwa sasa hivi pande zote zenye malalamiko ziko kwenye majadiliano ya usuluhishi. Hili la kuzungumzia majeshi ya kivamizi ya Tanganyika ni upuuzi mtupu. Yaani waZanzibari mnajisikia mpo karibu zaidi na Oman kuliko Tanganyika? - Eti raia wa Oman walifurahi sana!
  • Leo watu wanakwenda ikulu ya Marekani kuandamana ili Marekani iifanye nini Tanzania?
  • Je, mazungumzo ya usuluhishi yameshindikana kutatua hili tatizo?
  • Marekani ni nani katika muundo na Katiba ya serikali ya Zanzibar?
  • Ni kipi tusichoweza kukizungumza na kuelewana katika lugha yetu ya Kiswahili mpaka tuwaite waMarekani?
  • Kwa nini tusiwaite Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ghana badala ya Marekani na Uingereza?
  • Hiki kiherehere cha kukimbilia nchi za magharibi chanzo chake ni kipi?

Nina maswali mengi najiuliza kwa hili na nakosa majibu. Matatizo tunayo - ndio, lakini hivi hatuwezi kukaa na kupata suluhu sisi wenyewe mpaka tukimbilie kwa "mabwana" zetu huko ulaya? This is pathetic.

Aliyekuwa rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili Mwalimu nyerere kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kufanyika aliasisi pia kudhulumiwa kwa ushindi wa CUF, kwa kwenda kulazimisha atangazwe Salmin Amour. Mwaka 2001 rais Mkapa aliwaua wazanzibari baada ya kuwanyang'anya tena ushindi wa wapinzani, zingatia amiri jeshi ni rais wa serikali ya muungano yuko magogoni, trend ya kuwapora ushindi kila mara inasimamiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa CCM kutoka Tanganyika kwa hiyo kwa nini wajione wako karibu wa watanganyika wanaowaonea hata kuwaua wanapochagua viongozi wanaowapenda.

Mwaka 2010 wakaamua kuunda serikali ya moja wa kitaifa na CUF wakakubali kwa nia nzuri ila inaonekana CCM Hawa kuwa na dhamira nzuri, Leo wameshinda tena wanaporwa ushindi kwa njia ya kihuni na Wewe unayejiona una akili sana, mzalendo sana unaona business as usual waanza tena kukaa vikao miaka mitano hadi uchaguzi mwingine. Punguza chuki za kishetani dhidi ya wazanzibari, wamarekani na wote wapenda amani, kubali kataa ni majeshi kutoka Tanganyika yaliyoenda kuzingira tume ya uchaguzi Zanzibar na kumlazimisha Jecha kuufuta uchaguzi. Weka ukada na ushabiki pembeni tuungane kuukemea udhalimu unaofanywa na Hawa jamaa kutoka Dodoma, wazanzibari wana haki ya kuchagua wanayemtaka Si kuchaguliwa na anayetakiwa na CCM.

Toka mwaka 1995 vinafanyika vikao hakuna suluhisho kwa sababu mshindani(CCM) ndiyo huyo huyo mwamuzi
 
Hauna ajili kabisa. Mali zinazoendwleza marekani zinatoka wapi???? Uchumi unapanda kwao unapandishwq na Mali za wapi? Ni dhahabu zetu za Geita na Alma's na tanzanite. Uwiiiiiiiii soma ustaarabike inauma Sana ukijua
Wewe unafikiri USA ndio hawana mali? kwataarifa yako wana reserve ya mafuta ya kuwatosheleza hata miaka 200 wanakula vya wajinga. halafu wewe mwenye akili mbona unakubali mali kutoka kwetu zikawaendeleze badala ya kukuendeleza wewe unaejiita msomi ? kukariri na kusoma ni vitu viwili tofauti. wewe unasoma vitu vilivyoandikwa na wao bado unajiita ni msomi kuliko wao kweli wewe ni poyoyo
 
Uhuru gani unaojivunia nao? Uko huru wakati unaenda kuomba hela za millennium kwao

Kwa hiyo unadhani waZanzibari sio huru? Nani anawanyima huo uhuru? Au wewe ni ukoo wa yule Sultani aliepinduliwa mwaka 1964? Hebu nifafanulie una maana gani unaposema Zanzibar hakuna uhuru.

Kuomba misaada kutoka mataifa ya magharibi siku zote sio kitu kizuri. Tunakuwa tegemezi kiuchumi. Nchi yetu ni taajiri sana bali kuna watu wenye ubinafsi (CCM, CUF, CDM, n.k., wote wamo) ambao wanachumia matumbo yao tu. Hili tatizo linatatulika na nadhani rais Magufuli atalinyoosha, Inshallah.

Lakini hii tegemezi yetu kiuchumi ndio itufanye tuwe tegemezi kifikra pia? Hapana jamani. Ninakataa utumwa huu wa kifikra. Ni utumwa mbaya sana kuliko utumwa wa kufungwa minyororo ya miguuni na mikononi. Acheni hii kitu.
 
It is stupid kwenda white house,and it is very clever for CCM to do what they have done in Zanzibar. Kweli wabongo hazimo ila nyinyi ambao zimo mnakubaliana na mchezo mchafu wa ccm

What has CCM done to Zanzibar? Please don't use hyperboles you cannot justify.

Ni mchezo gani huu mchafu unaouzungumzia hapa?
- Kurudia uchaguzi ni mchezo mchafu?
- Je, kutangaza matokeo yenye utata ndio mchezo safi?

Grow up!
 
Kwa hiyo unadhani waZanzibari sio huru? Nani anawanyima huo uhuru? Au wewe ni ukoo wa yule Sultani aliepinduliwa mwaka 1964? Hebu nifafanulie una maana gani unaposema Zanzibar hakuna uhuru.

Kuomba misaada kutoka mataifa ya magharibi siku zote sio kitu kizuri. Tunakuwa tegemezi kiuchumi. Nchi yetu ni taajiri sana bali kuna watu wenye ubinafsi (CCM, CUF, CDM, n.k., wote wamo) ambao wanachumia matumbo yao tu. Hili tatizo linatatulika na nadhani rais Magufuli atalinyoosha, Inshallah.

Lakini hii tegemezi yetu kiuchumi ndio itufanye tuwe tegemezi kifikra pia? Hapana jamani. Ninakataa utumwa huu wa kifikra. Ni utumwa mbaya sana kuliko utumwa wa kufungwa minyororo ya miguuni na mikononi. Acheni hii kitu.

Awali ya vyote mkuu kuwa na courage ya kukemea uovu na kuukataa kwa akili yako bila unafiki, mapinduzi ya Zanzibar yamebaki historia kama mapinduzi mengine katika nchi nyingi, kumbuka hii imetumika sana na wahafadhina ndani ya CCM hususan Zanzibar kujimilikisha haki ya kutawala milele.
Fikiria nje ya box, serikali inayochaguliwa kwa kura Leo hii bado inaitwa serikali ya mapinduzi,inaleta maana kwako? Yule mama mjumbe kutoka Zanzibar kwenye bunge maalum la kutunga katiba kutoka Zanzibar alisema na hakuna kiongozi yeyote kutoka CCM na Zanzibar aliyemkanusha kuwa hatutoi serikali kwa vikaratasi.

Askari wa jeshi la wananchi waliovamia tume ya uchaguzi Zanzibar waliamrishwa na nani? Mamlaka hii iko kwa dk Shein?kama Haiko Zanzibar wana Uhuru gani? Achana na hizo dhana za patrionism zinazokupofua macho hata huwezi kuona vitu kwa uhalisia.

Mwisho kuna msemo , kwenye ukandamizaji wowote kama Hau
ko upande wa wanaokandamizwa basi upo upande wa wakandamizaji, na hili Uko wazi kama nyeti za nyani, utawakosoa ukawa mfano kisha la kumuingiza Lowassa lakini utakaa kimya kwa sababu za uozo wa haya vyote, come out waambie CCM wenzako watoe Uhuru wa zanzibar
 
Aliyekuwa rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili Mwalimu nyerere kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kufanyika aliasisi pia kudhulumiwa kwa ushindi wa CUF, kwa kwenda kulazimisha atangazwe Salmin Amour. Mwaka 2001 rais Mkapa aliwaua wazanzibari baada ya kuwanyang'anya tena ushindi wa wapinzani, zingatia amiri jeshi ni rais wa serikali ya muungano yuko magogoni, trend ya kuwapora ushindi kila mara inasimamiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa CCM kutoka Tanganyika kwa hiyo kwa nini wajione wako karibu wa watanganyika wanaowaonea hata kuwaua wanapochagua viongozi wanaowapenda.

Mwaka 2010 wakaamua kuunda serikali ya moja wa kitaifa na CUF wakakubali kwa nia nzuri ila inaonekana CCM Hawa kuwa na dhamira nzuri, Leo wameshinda tena wanaporwa ushindi kwa njia ya kihuni na Wewe unayejiona una akili sana, mzalendo sana unaona business as usual waanza tena kukaa vikao miaka mitano hadi uchaguzi mwingine. Punguza chuki za kishetani dhidi ya wazanzibari, wamarekani na wote wapenda amani, kubali kataa ni majeshi kutoka Tanganyika yaliyoenda kuzingira tume ya uchaguzi Zanzibar na kumlazimisha Jecha kuufuta uchaguzi. Weka ukada na ushabiki pembeni tuungane kuukemea udhalimu unaofanywa na Hawa jamaa kutoka Dodoma, wazanzibari wana haki ya kuchagua wanayemtaka Si kuchaguliwa na anayetakiwa na CCM.

Toka mwaka 1995 vinafanyika vikao hakuna suluhisho kwa sababu mshindani(CCM) ndiyo huyo huyo mwamuzi

Katika aya yako ya kwanza umetuhumu watu kufanya makosa ya jinai (kuua). Kama una ushahidi basi fungua kesi Tanzania au nje ya Tanzania uwashitaki hawa watuhumiwa.

Katika aya yako ya pili, wewe unaona uhuru utapatikana Zanzibar pale tu CUF watakaposhinda. Jua kwamba CCM kwa upande wa Zanzibar ni Afro-Shiraz party. Ni chama halali cha Zanzibar. CCM kwa Zanzibar sio chama cha Tanganyika. TANU haina ngome visiwani.

Mara nyingi watu walikuwa wanasema CUF ni offshoot ya waZanzibari waliokuwa wafuasi wa Sultani aliepinduliwa mwaka 1964. Mimi nilikuwa nawapuuzia lakini sasa ninaanza kupata wasiwasi. Kama uchaguzi siku zote utakuwa batili mpaka Maalim (CUF) ashinde, basi itakuwa shida sana.

Haya madai ya kuwa tokea 1995 Maalim alikuwa anashinda chaguzi bali CCM walikuwa wanapora sasa yanaanza kuchosha akili yangu.

Kwa nini tusirudie uchaguzi, na safari hii usimamiwe na an independent party kama Umoja wa Mataifa, halafu tuone matokeo. Hapa utata uko wapi?
 
Back
Top Bottom