Serikali inachukua hatua stahiki kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula

AFRIKAMOJA

Member
Aug 11, 2022
30
37
NI KUWEKEZA KWENYE UZALISHAJI PEKEE NDIO KUTATUTOA HAPA NA SERIKALI IMEJUA NA IMESHACHUKUA HATUA.

Hali ya bei za vyakula kwenye masoko mbalimbali nchini bei inaonekana kuongezeka mara mbili mpaka tatu ya bei zilizozoeleka. Hali inayoibua manung'uniko kila kona ya Nchi yetu kuanzia wenye kipato kidogo mpaka kikubwa. Wanasiasa wa upinzani nao wameibeba kama agenda na turufu ya kupata ushawishi wa kuungwa mkono na wananchi.

Hata hivyo ni jambo la kushukuru Mungu kwamba pamoja na bei hizi kupanda bado chakula kinapatikana kwa wingi katika maduka, magenge na masoko yetu hivyo wananchi tunachagua kipi cha kununua kulingana na pesa tuliyonayo maana havifanani bei.

Ukweli ni kwamba zipo sababu nyingi za kutufikisha hapo:-

1. Kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa sababu mbalimbali kama vile wakulima kupunguza ukubwa wa ardhi/mashamba waliyokuwa wakilima kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya pembejeo ikiwemo mbegu na mbolea.

2. Tatizo la mabadiliko ya tabia Nchi lililopelekea ukame/upungufu wa mvua na kufanya mazao kukauka hivyo wakulima kukosa mavuno mazuri.

3. Athari za vita ya Ukraine na Urusi pamoja na maradhi ya Uviko-19 vimeathiri uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za pembejeo toka viwandani kuwafikia wakulima. Gharama za meli na bima zake zimepaa hivyo usafirishaji wa meli bei nazo zikapaa.

4. Ongezeko kubwa la Idadi ya watu, idadi ya watu imekua kwa kasi hali iliyosababisha mahitaji ya chakula kuzidi kiwango cha uzalishaji hali iliyoleta upungufu.

5. Mazao ya chakula leo yanashindanishwa sokoni kama bidhaa zingine katika ile dhana ya kilimo biashara hivyo wafanyabishara wanaotaka kupata faida kubwa wanatumia fursa hii hivyo hakuna namna bei zitakuwa juu tu.

6. Bei nzuri sokoni huwatamanisha wakulima kuuza chakula chote bila kubakiza akiba kwaajili ya matumizi yao.

Hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kukabiliana na hali hii kwa sasa na baadae:-

I. Kutoa ruzuku ya mbolea ili wakulima walime zaidi kuliko msimu uliopita na hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula. Kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya uzalishaji mbolea ni mpango wa kupata majawabu ya kudumu kwenye suala la mbolea ambapo tayari kiwanda kipya cha Intracom kimeshakamilika Nala mkoani Dodoma kimeanza uzalishaji wa tani laki mbili kikiwa kimeajiri 972.

II. Kuongeza nguvu na kasi ya ujenzi wa vihenge vya kisasa vya kuhifadhi mazao ya nafaka ili kuongeza uwezo wa nchi kuhifadhi mazao hayo kwa lengo la kukidhi mahitaji wakati wa changamoto au majanga.

III. Kuingiza sokoni mazao ya chakula kwa bei ya chini ili kusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei uliopo

IV. Kuwekeza kwa nguvu katika kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga miundombinu ya skimu za umwagiliaji takribani shilingi bilioni 400 zimewekwa huku pamoja na ununuzi wa mitambo ya uchimbaji mabwawa ambayo tayari imeshagawanywa ili kuondokana na utegemezi wa mvua katika kilimo hivyo kupunguza athari za mabadiliko ya tabia Nchi.

V. Kuendelea kutoa elimu juu ya namna bora ya kuhifadhi chakula baada ya mavuno pamoja na utunzaji wa chakula katika ngazi ya kaya.

VI. Kuendelea kuhamasisha utii wa sheria, utunzaji wa amani, usalama na utulivu wa nchi ili kujenga mazingira mazuri kwa uzalishaji na shughuli zingine za maendeleo.

VII. Kuwaelimisha wakulima kuhusu kilimo cha kisasa ili kulima kwa tija na kuepuka uharibifu wa mazingira pamoja na kuwawezesha maafisa ugani katika ngazi ya vijiji pikipiki ili kurahisisha kuwafikia wakulima katika ngazi ya kaya pamoja na vifaa maalum vya kupima afya ya udongo

VIII. Kwenye eneo la mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo nk) serikali imeendelea kupima na kutenga maeneo kwa ajili ya malisho, inajenga majosho, inahamasisha upandaji wa nyasi lishe kwa ajili ya malisho kwa lengo la kuepusha mifugo kusafiri umbali mrefu au kuhamahama wakati wa ukame kutafuta malisho pamoja na utaratibu wa uchimbaji mabwawa kama nilivyoeleza hapo juu.

Tushirikiane kutumia mazingira haya kuzalisha kwa tija ili kuweza kunufaika na upungufu au ukosefu wa chakula utakaozikumba nchi nyingi duniani kwa kuuza mazao yetu pamoja na kujihakikishia upatikanaji wa chakula kwa bei rafiki kwani uzalishaji ndio utaamua bei ya soko sio vinginevyo.

#SerikaliMakini #RaisMakini #SSHKaziIendeleeView attachment 2496237
IMG_20230126_100000_742.jpg
View attachment 2496238View attachment 2496239View attachment 2496240
 
... baada ya Lissu kuanza nalo ndio wanaongea ujinga? Walikuwa wapi siku zote including hao wabunge wanaotakiwa kuwa wasemaji wa wananchi? Hawa watu sijui wakoje!
 
4. Ongezeko kubwa la Idadi ya watu, idadi ya watu imekua kwa kasi hali iliyosababisha mahitaji ya chakula kuzidi kiwango cha uzalishaji hali iliyoleta upungufu.
... si tulihimizwa tufyatue? Leo tumegeukwa?
 
Back
Top Bottom