TANZIA Mfanyabiashara Emilian Woiso afariki dunia

Acheni utoto...unawajua hawa!
1.Marehemu dena hamsi?
2.yoyo?
3.fidel
4.game theory?
5.field marshal Es (maremu wm)
6.Mike Mushi (owner wa JF...co founder)
7.Nyani Ngabu
8.pakajimmy
9.lara na madame b
10........acheni Utoto!
Wako hapi hao wote uliowataja?
 
Mkuu kuna wakati nakula konyagi yangu nawaangalia watoto wangu naishia kucheka tu...nawaambia nyie mnapata hela kirahisi sana sa hv...ila kuna vitu ukihadithiwa utaona either uwongo au movie..kuna wakati inabidi uchukue hela za watu kinamna vyovyote tu hamna jinsi!

Mzee alikua ni master kabisa...walienda walioenda na hakucheka na mtu! Ila mwishoni aliokoka kweli na trakea ikawa kanisa badala ya baa...woiso wa Wop ni kijana mdogo sana...sidhani hata kama 44 anafika...ila kwa umri wa woiso kulikua hamna namna ya namna ya kutafuta hela kipindi chao...hela ilikua haipatikani instagram ilibidi uichukue kwa watu!
Kweli kabisa siku hizi hela ipo Instagram, ndio maana tunawaona machawa kama akina Mwijaku,Doto Magari ,Haji Domo, Konde na wajinga wajinga wengi wakiwa mamilionea kwa kuwa wajinga na wengine kwa kuonyesha misambwanda huko Instagram.
 
Duh hatari sana 80s kweusi serikali ilikuwa hamna nini bado akaendelea kuwepo mtaani
Huyu aliwahi kumwambia rafiki yangu mlokole mjanja ambaye ana nyumba za kupangisha 15 maeneo mbalimbali ya jiji ya Dar Es Salaam, kuwa ha yaani nyumba 15 nawe unasema una nyumba hapa jijini, yaani unatakiwa angalau una nyumba kuanzia 30 na kuendelea bwashee, maneno hayo anamwambia hapo kanisani kwao!
 
Jf ni balaa watu wanaubuyu balaa yani mzee marehemu amedadavuliwa kama wachambuzi wa soka wanavyo lichambua soka.
Kiufupi ukisoma komenti karibia zote zinaonesha marehemu alikuwa mtu hatari.
Kinachonifurahisha ni kwamba humu kuna memba amesoma na kila marehemu. Yani koment rip classmate hatakama marehemu alikuwa na miezi miwili utaikuta.
Kaanzia kwa Captain, hata mimi nimemshtukia!
 
Mnakosea sana. Hamjui biblia. Nenda kasome baada ya daudi kushika madaraka nchi ikawa bado haibarikiwi na David alipouliza alijibiwa nini na nabii? Waliambiwa utawala uliopita wa sauli uliua wana wa Gibeon so waende wakawaulize hao wana wa Gibeon kifanyike nini ili wasamehe na nchi itakasike? Wakawaambia wawaonyeshe mabaki ya jamaa ya sauli wawaue ili kulipiza kisasi na walipofanya hivyo nchi ilitakaswa. Mfano mwingine Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunz wake patana na mshitaki wako kwanza kabla hamjafika kwa hakimu na akasema hautatoka humo kamwe mpaka ulipe senti ya mwisho. Mfano mwingine wa zakayo alipompokea Yesu tu alikumbuka dhambi zake na akasema atawarejeshea mara kumi aliowadhulumu. Ni hiv, Mungu sio dhalimu wewe unaweza kukuta umenidhulumu halafu unaenda kuokoka lakin unasahau mimi kila asubuh naamka namkumbusha Mungu asisahau uovu ulionifanyia umenidhulumu. Na kuhakikishia Mungu ni wa haki hata sikia sala yako ya kuokoka bali atamsikiliza aliyekosewa. Ndio maana Yesu alikuja kwakuwa sheria ya roho ni lazima haki yote itimizwe Mzee so kama umeiba umedhulumu nenda watafute uliowatendea uwarudishie vyao ndio uje madhabahuni kuokoka. Mungu ni haki na kweli.
Duuh
 
Mzee Emil Lesheya Woiso amefariki leo asubuhi. Msiba upo nyumbani kwake Tegeta karibu na IPTL.

Alikuwa mmiliki wa Tarakea Restaurant pale Mwenge na Cornelius Girls Secondary School pale Tegeta Skanska

natoa faraja kwa wafiwa. kifo kinauma, ukifiwa moyo unaumia, wanahitaji wafarijiwe. hata Yesu alilia pamoja na waliolia.

ila nyote mnaosoma hapa, jiandaeni kwa kifo kwa kumpa Yesu Maisha yenu ili kama mkifa mfe katika Bwana na mkiishi muishi katika Bwana. msidanganywe na mapadre na wachungaji wanaowadanganya kwamba mkifa wataombea maiti zenu au makaburi yenu na huko mliko mtasamehewa. baada ya kifo ni hukumu. hivi ndio vifungo vimewafanya wakatoliki na watu wa dini zingine waogope hata kuondoka,ndio mnyororo na pingu za kuwashikilia kwenye madhehebuhayo yasiyo na Mungu, watu wanaogopa wakiondoka watazikwa na nani? nani atawaombea wakiwa maiti? as if wakiombewa watasamehewa. Kama ingekuwa mtu akifa anaombewa na kusamehewa Mungu asingeelekeza tuache dhambi, si ndugu zangu wangeniombea? unafanya zako dhambi, unakufa, wanakuombea ndugu zako, unaenda mbinguni. ingewezekana kweli?

BIBLIA INASEMA KATIKA UFUNUO 14:13; Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

MANAKE, ukifa matendo yako yatafuatana nawe, yaani yatakufuata ukahukumiwe nayo, pale tu unapokufa, jua ndio itakuwa deadline ya wewe kutengeneza na Mungu kwa kutubia dhambi zako, hatutubu tukiwa tumekufa, opportunity hiyo ni ukiwa hai. na hii mkifunguka itawasaidia kuyakimbia makanisa yasiyohubiri wokovu, hayo yanayohubiri kuomba kwa maria na wafu badala ya Jina la Yesu, hayo yanayohubiri kuombea watu as if wao ndio wenye ticket ya kukufanya uende mbinguni au motoni, wao wenyewe hawana Mungu. kimbieni huko, kimbieniiii.
 
Mkuu wewe very soon unajinyonga .....hebu tafuta mshauri mkuuu kam una HIV sio mwisho wa maisha ....ila kunywa dawa vizuri maana ikifika AIDS hata nguvu ya kujinyonga utakuwa huna ...

Kama una kansa tumia morphine hadi mauti yatakapo kuja

Kama ni depression kaa na ndugu zako vizuri watakushauri namna bora kuepuka depression pia kukupa upendo epuka kukaaa pekee yako kuanzia sasa

Maana nimesoma uzi wako juzi na hiii reply yako naona una roho ya kujiua imeingia na kutoka huwa ni ngumu hadi ujiue usipopata ushauri
Huyuuu ashaenda mkuu ashauriki labdaa ushauri wanguu aandike wosia asitutesee msiban upended wa mirathi
 
Back
Top Bottom