Meseji niliyoikuta kwenye simu ya mke wangu

hakya mungu kaka pole.

mna mda gani ndani ya ndoa?
mna watoto? wangapi
siku ya kwanza kukutana na mkeo ilikuwa baa, stand,barabarani, kanisan,sokoni, kwao?

kwa kukwa adhabu unaijua wewe basi ila kama ni ushauri basi piga chini maana halua haina kipolo!!

haijalishi wamekutana wapi kinachomata ni uaminifu katika mahusiana
 
Kaka umesema hutaki ushauri ila mi ntakupa ushauri, juu yako kuuchukua au la.

UCHUNGUZI: Hapa ushaharibu kwa kuweka hii mada hapa, ingawa lengo lilikuwa kuondoa hasira, manake uwezekano ni mkubwa habari zitawafikia watuhumiwa,unless ulikuwa smart enough kwa kuandika jina la uongo,yani coleman liwe jina umelitunga wewe na kubadili mazingira kdogo ya tukio

SULUHISHO : Ukijiridhisha kwa njia unazojua mwenyewe kuwa ni kweli mkeo amefanya hicho kitu MUACHE MKEO mara moja, utaishi kwa amani zaidi na furaha.usijidanganye na hayo mawazo eti forgive and forget, kuna mambo wanaume tunaweza kuforgive na kuforget, lakini sio hilo. That's the most practical solution
 
Coleman naamini nimshikaji wangu nilisoma nae Minaki Boys, maana anafanya kazi mitaa ya Samora . kama ni huyo anamke mzuri sana, peleleza uthibitishe kama ni yeye, kisha nakushauri mmegee mkewe kwa kiwango kilekile ulichotendewa , kisha akikutumia msg yakukushukuru mahaba yako nawe jidai umesahau simu sebuleni ili mkeo aisome, akikomplain unamwambia huyo ni mke wa Coleman. ananishukuru kwa starehe nimpayo , tafadhali akikisha unaitunza hiyo msg vizuri ili akizidi kelele unamsomea huo ujumbe....otherwise pole, usimuache mkeo ila sera yako iwe jino kwa jino, sikio kwa sikio.
 
Ukifuata umbea utavunja unyumba wako.
sms kwenye simu ya mkeo achana nayo.Yaweza kuandikwa na wabaya wenu.
 
kaka hapo hiyo ndoa haina uwaminifu tena cha msingi ni kuita wakubwa na kumwambia aachane na hiyo tabia na aende katika vyombo vya dini akaape.
 
Ahhhhh Bujibuji pole kiongozi wangu...mi yamenikuta kama hayo jamaa linamwambia wife ur so sweet i will never leave you alone....mi nilitaka nipigane...nikamtaiti wife akasema kweli jamaa kagonga ngozi kama mara 3 hivi...nikamwambia aache mungu hapendi.
 
Mchana huu wa leo mama watoto alinipitia na tukaenda kwenye kiji mgahawa kimoja hapo jirani na jengo la ppf tower.
Pale tukakutana na wafanyakazi wenzangu na hivyo basi mama watoto akawa akibadilishana nao mawazo.
Wakiwa wanaendelea na mazoezi nikawa nimeishika simu ya mama watoto ili nichue namba ya shangazi yangu aliyeko shamba.
Baada ya kuichukua ile namba nikaingia kwenye meseji.
Sina utamaduni wa kukagua simu ya mama watoto, hata yeye analijua hilo lakini leo sijui ni kitu gani kimetuma kufanya hivyo.
Hii ndiyo sms niliyoikuta kwenye simu yake "mi sina la kusema, coz najua hou u make me crazy on bed, roll it babe!"

basi nikajiforwadia kwenye simu yangu, na nikaichukua namba ya huyo mtumaji ambaye anaitwa coleman.
Mpaka naachana na wife sikusema chochote na nikajaribu kuficha machungu yangu ili kati yetu asiwepo wa kujua na kuniuliza ni nini kimetokea.
Sitaki mnielekeze kuwa nimsamehe au nimuadhibu..
Nimeongea hapa ili kutoa donge la hasira na uchungu vilivyonijaa moyoni.

omba kibali cha kingia mambo ya kikubwa
haya matatizo yasingekuokea ;kuna mada za wanaume kushika simu za wake zao;wanawake kushika simu za waume zao na madhara yake;nafikiri moja ya madhara yalikuwa yakiandikwa hili lako ni oja wapo labda kabla ya kuendelea tueleze ulipofikia umefanya lolote;ama kijiua;kumpeleka polisi;kuondoka nyumbani;ama kunywa valou kila siku na kushindwa kwenda kazini lipi linaaloendela
pole sana usikate tamaa huyo ni wako wa maisha
no money no hny
 
Duh haya ndio maisha kaka.....sio kula peremende tu bali na machungu pia. Kuna mambo mengi binafsi naweza kushauri.

Mtazamo wa suala lenyewe

1. Ni vizuri ukatumia muda na busara zako kujiridhisha juu ya uhalisia wa hiyo message i.e. je imekosewa mlengwa au ilikuwa intended kwa mkeo. Kama ni suala la kukosea namba hicho ni kitu cha kawaida.....mengi yametokea mfano kutuma muda wa maongezi kusikohusika n.k.

2. Kama ilikuwa intended kwa mkeo, ni vizuri kujiridhisha kuwa ilitumwa kwa makusudi ya kukugonganisha au ni mawasiliano ya kawaida baina ya wapenzi. Kupata namba ya mtu sio kitu kigumu sana, watu wengi wametumia fursa hiyo kutuma ma-ujumbe ya ajabu-ajabu ili kuleta mtafaruku kwenye nyumba za watu (usisahau mkuu ndio maana pamoja na mambo mengine hawa jamaa wanataka kusajili namba za simu zetu kutokana na kero kama hizo).

3. Kama ilitumwa kwa minajili ya kubadilishana salamu za kimapenzi baina ya wapenzi, hapo ndipo kwenye tatizo na fursa. Tatizo ni kuwa mkeo ameteleza...na fursa ni kuwa umefahamu hilo na uko katika nafasi ya kulirekebisha. Ni mapenzi ya Mungu umejua hilo sasa na ni wajibu wako kurekebisha kasoro hiyo.

Ushauri wangu

1. Ikiwa na kukosewa namba au sms ya kukugombanisha....just ignore it! Binafsi nikupe kisa live. Siku tulikesha kikazi somewhere...ilipotimu saa tisa alfajiri mfanyakazi mwenzetu mmoja akapokea forwarded sms toka kwa mkewe ikielezea kuwa jamaa amelala kwenye nyumba ndogo. Alichokifanya yule bwana ni kumpigia mkewe simu instantly na kutupatia tuongee nae, shemeji yetu aliridhika na alituomba radhi kwa kutokuwa mstahimilivu

2. Ikiwa mkeo ameteleza....ni vizuri ukae nae chini umtake ajirekebishe. Hataweza kukubali kuwa anafanya mchezo huo....lakini muombe atunze heshima yako na umwambie mjitahidi kurekebisha tatizo hilo mapema. Usiwe na maswali ya kipolisi, ujikakamue uweke msimamo wako imara. Kuoa au kuolewa sio mwisho wa kupenda....hivyo huwezi kuzuia kupenda kwa mabavu bali kwa hekima na werevu. Inauma sana lakini ndio maisha....sisi sote binadamu tuna udhaifu na mapungufu....ni budi kutumia busara zetu kurekebisha mapungufu pale yanapotokea. Endelea kumpenda mkeo kwa heshima kubwa uliyonayo kwa watoto wako
 
Ahhhhh Bujibuji pole kiongozi wangu...mi yamenikuta kama hayo jamaa linamwambia wife ur so sweet i will never leave you alone....mi nilitaka nipigane...nikamtaiti wife akasema kweli jamaa kagonga ngozi kama mara 3 hivi...nikamwambia aache mungu hapendi.

duh...!?
 
huyo mtu atakuwa ana mke sasa wewe na wewe anza kumtumia msg za mapenzi kila usiku wa manane mpaka yamkute yaliokukuta
pole kamanda wangu;wengine yalitukuta tukafungua njia mapema wengine wapite
 
Kaka umesema hutaki ushauri ila mi ntakupa ushauri, juu yako kuuchukua au la.

UCHUNGUZI: Hapa ushaharibu kwa kuweka hii mada hapa, ingawa lengo lilikuwa kuondoa hasira, manake uwezekano ni mkubwa habari zitawafikia watuhumiwa,unless ulikuwa smart enough kwa kuandika jina la uongo,yani coleman liwe jina umelitunga wewe na kubadili mazingira kdogo ya tukio

SULUHISHO : Ukijiridhisha kwa njia unazojua mwenyewe kuwa ni kweli mkeo amefanya hicho kitu MUACHE MKEO mara moja, utaishi kwa amani zaidi na furaha.usijidanganye na hayo mawazo eti forgive and forget, kuna mambo wanaume tunaweza kuforgive na kuforget, lakini sio hilo. That's the most practical solution

Mkeo akikukamata naye akuache??? mara ngapi mmetoka nje ya ndoa zenu?? give him a break to think wisely.
 
...kama mtu aweza piga wrong number, hata msg yaweza potea njia. Kwani vipi, humuamini au?
 
Mnapenda sana drama!wake zenu wako smart sana oooh ukiikuta ujue ck hy Mungu amekuonyesha tu kazi kwako kuna mengi makubwa zaidi hata ukute ni utani wa kazini....angalia asub wakifika makazin wake zenu wanapokelewa kwa kiss na shangwe zote utasikia mume wangu wa kazini nimeku miss sana tangu friday!!hata smsm wala call??
 
Ahhhhh Bujibuji pole kiongozi wangu...mi yamenikuta kama hayo jamaa linamwambia wife ur so sweet i will never leave you alone....mi nilitaka nipigane...nikamtaiti wife akasema kweli jamaa kagonga ngozi kama mara 3 hivi...nikamwambia aache mungu hapendi.

You are so lovely..., keep it up
 
jina la mtumaji ni coleman na liko saved kwenye phonebook ya amama watoto

Pole sana mkuu,inawezekana huyo Coleman anafahamiana na wife wako,na hiyo sms alikuwa anamtext girlfriend wake akakosea akaisend kwa mkeo kimakosa,fanya uchunguzi wa kina kabla ya kumhukumu mkeo!!!
 
Pole sana mkuu,inawezekana huyo Coleman anafahamiana na wife wako,na hiyo sms alikuwa anamtext girlfriend wake akakosea akaisend kwa mkeo kimakosa,fanya uchunguzi wa kina kabla ya kumhukumu mkeo!!!

Haya ndiyo majibu yao ili kukupoza baada ya hapo unarembuliwa macho na kuambiwa kwa sauti ya upole "I Love you honey, don't you trust me babe?" ukimpa kisogo tu anakung'ong'a na kujisemea kimoyomoyo kwisha habari yako zezeta mkubwa huyu kwenye simu yangu alikuwa anafuata nini haswa?. LOL!
 
Ahhhhh Bujibuji pole kiongozi wangu...mi yamenikuta kama hayo jamaa linamwambia wife ur so sweet i will never leave you alone....mi nilitaka nipigane...nikamtaiti wife akasema kweli jamaa kagonga ngozi kama mara 3 hivi...nikamwambia aache mungu hapendi.

teh teh mkuu we kweli kiboko,yaani mamaa kakiri kweli tena kagonga mara tatu!du aisee ukamwambia mungu hapendi,yaani mbavu zinauma kwa kucheka heri yangu mimi nilighairi kuoa katikati ya safari,na sasa ndio kabsaa ntakaa hivihivi lol.
 
Back
Top Bottom