Exaud Minja
Senior Member
- Mar 13, 2009
- 100
- 13
Mchana huu wa leo mama watoto alinipitia na tukaenda kwenye kiji mgahawa kimoja hapo jirani na jengo la ppf tower.
Pale tukakutana na wafanyakazi wenzangu na hivyo basi mama watoto akawa akibadilishana nao mawazo.
Wakiwa wanaendelea na mazoezi nikawa nimeishika simu ya mama watoto ili nichue namba ya shangazi yangu aliyeko shamba.
Baada ya kuichukua ile namba nikaingia kwenye meseji.
Sina utamaduni wa kukagua simu ya mama watoto, hata yeye analijua hilo lakini leo sijui ni kitu gani kimetuma kufanya hivyo.
Hii ndiyo sms niliyoikuta kwenye simu yake "mi sina la kusema, coz najua hou u make me crazy on bed, roll it babe!"
basi nikajiforwadia kwenye simu yangu, na nikaichukua namba ya huyo mtumaji ambaye anaitwa coleman.
Mpaka naachana na wife sikusema chochote na nikajaribu kuficha machungu yangu ili kati yetu asiwepo wa kujua na kuniuliza ni nini kimetokea.
Sitaki mnielekeze kuwa nimsamehe au nimuadhibu..
Nimeongea hapa ili kutoa donge la hasira na uchungu vilivyonijaa moyoni.
Sikupi pole Mzee kwasababu inawezekana hiyo msg iliingia kwa makosa haikuwa kwa ajili ya Mkeo. Binafsi nilishawahi kutumiwa msg na msichana kwenye simu yangu kwa makosa na ilikuwa ina ujumbe mzito sana kama ingetokea Mke wangu kuiona ingekuwa balaa kenye ndoa yangu mpaka ukoo mzima wangeipata. MSG ilikuwa inasema "JANA UMENIFANYA KOTE HALAFU HELA YENYEWE KUMBE HUNA, USIPONIPA HELA YANGU LEO NAKUJA DAI MBELE YA MKEO".