Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Mimi nadhani hii ni sinema tu...
Huyo Masha na Mengi kwa muda mrefu wamekuwa nje ya media hivyo wanafanya kutukumbusha kuwa bado wapo mtaani kama Diva - Madonna!
 
Sijaelewa kitu kimoja. Sijaona Masha kutajwa kwenye taarifa ya Mengi. Au Mengi alimtaja sehemu nyingine?
 
Serikali yachunguza vitisho dhidi ya Mengi

2008-12-06 11:39:17
Na Joseph Mwendapole


Serikali imesema inafanyia uchunguzi madai ya kutishiwa kuuawa yaliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, na itachukua hatua kali endapo itabaini kuna ukweli.

Akizungumza jana katika kipindi cha Jambo Afrika cha TBC, Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, alisema serikali inachunguza waliohusishwa na tuhuma hizo na wakibainika watachukuliwa hatua.

Masha alisema kwa kuwa Mengi alisema ana ushahidi wa tuhuma alizotoa, serikali haitapata shida ya kuhangaika na ushahidi na imemtaka apeleke ushahidi huo.

Alisema tayari ameshaagiza maofisa wa wizara yake walifanyie uchunguzi wa kina suala hilo na kisha wampe taarifa.

Waziri Masha alisema ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa raia na mali zao hivyo hawezi kuacha kufanyia kazi suala zito kama hilo.
``Mengi alisema ana ushahidi wa kutosha hivyo tumempa siku saba atuletee huo ushahidi ili tuufanyie kazi na ikibainika kuna ukweli hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika,`` alisema Waziri Masha.

Kwa mujibu wa Masha, endapo Mengi hataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma alizotoa serikali itaangalia hatua za kuchukua.

Kwa upande wake, Mengi alisema jana kuwa siku saba alizopewa na Masha ni nyingi sana na kuongeza kuwa angempa muda kidogo ili auwasilishe ushahidi huo kwa kuwa yu tayari hata leo hii (jana).

Alisema amemshangaa waziri huyo kama alizungumza kama msemaji wa wizara hiyo ama msemaji wa mawaziri vijana kwa kuwa yeye (Mengi), alichozungumzia ni serikali nzima kwa kuwa wizara nyingi zina mawaziri vijana.

``Wizara ya Masha inatoa hoja nyingi. Kuna wengine wanasema nimeripoti taarifa za vitisho polisi na wengine wanasema sikuripoti,`` alisema Mengi na kuongeza kuwa, kama itabainika amedanganya, atakuwa tayari kufungwa na kama ni kweli Masha awe tayari kujiuzulu
.
Katikati ya wiki hii, Reginald Mengi alimtuhumu Waziri mmoja kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kutokana na vyombo vyake vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele ufisadi.

Mengi alisema waziri huyo ameahidi kumnyamazisha kabisa kutokana na kupigia kelele vitendo vya ufisadi.

Mengi alisema waziri huyo amekuwa akijigamba kuwa atamnyamazisha kwa kuhakikisha anafilisiwa kama alivyofilisiwa tajiri mmoja nchini Urusi.

Mengi alisema kuwa waziri huyo anadai kuwa vyombo vyake vya habari vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri na linawanyanyasa baadhi ya watu.

``Nilitarajia waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanyakazi...anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na si mmiliki,``alisema.

Alisema ingawa tayari amemsamehe waziri huyo, lakini anapaswa kujua kuwa asiyekemea maovu katika jamii anakuwa sehemu ya maovu hayo.

Mengi alisema waziri huyo na wale ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa vitisho lazima wakumbuke kuwa hata wakifanikiwa kumnyamazisha yeye (Mengi), moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za Watanzania hauwezi kuzimika kamwe.

Alisema lazima ieleweke kuwa sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi na vyombo vya habari ndivyo vimechukua jukumu la kusaidia kupaza sauti zao.

Mengi alisema ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo wa kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

``Nampongeza sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na serikali yake dhidi ya ufisadi....sisi sote lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribu makubwa,`` alisema Mengi.

Alisema ufisadi wote ambao Rais Kikwete amekuwa akipambana nao ulifanyika wakati wa serikali ya awamu ya tatu.

Alisema Kikwete amekuwa jasiri na shupavu katika kupambana na maovu ambayo alikuta tayari yamefanyika wakati anaingia madarakani.

Mengi aliwashauri waandishi wa habari kuandika pia mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya nne, badala ya kuelemea zaidi katika ufisadi.

``Tuendelee kuandika habari za ufisadi lakini mazuri yanayofanywa na Rais Kikwete nayo yapate nafasi ili isije ikaonekana kama hajafanya kitu wakati yapo mengi sana amefanya kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani,`` alisema.

Vile vile, Mengi alisema kuna watu wameanza kutoa vitisho dhidi ya watu wanaopinga vitendo vya ufisadi.

Alisema watu hao wamebuni mbinu mbalimbali za kukwamisha wale ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo hivyo.

``Wakati kuna kundi la watu limeamua kwa dhati kabisa kupambana na ufisadi, kundi lingine limeamua kupingana nao lakini nawapa moyo kuwa wasitishike na wasikate tamaa, wazidi kupambana na waamini kuwa ushindi ni wao,`` alisema.

Baadhi ya ujumbe wa vitisho aliotumiwa kwenye simu yake kutoka kwenye simu namba 0768 373967 ulisomeka hivi: ``Ni afadhali kunyofoa roho yako ipotee kuliko uendelee kuchafua amani na utulivu wa nchi kwa tamaa zako za kuutaka urais...ugomvi wako na Manji hauwezi kutufanya watu wote tuingie katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, uliyofanya yanatosha enough is enough kaa tayari.``

Ujumbe wa pili aliotumiwa Mengi ulisomeka hivi : ``Unachafua sana amani ya nchi kwa uchochezi wako unapenyeza sumu ya uzandiki watu waichukie serikali. Hivi ikitokea vita wewe utasalimika? Wewe ni mnafiki mkubwa unajifanya uko karibu na serikali kumbe ni mnafiki wa kutisha jihadhari lazima tutakumaliza.``

Wakati huo huo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema kuwa mikakati inayodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa serikali kuwakwamisha wamiliki wa vyombo vya habari vinavyofichua ufisadi ni aina nyingine ya ufisadi ambao unapaswa kulaaniwa na watu wanaoitakia mema Tanzania.

Akihutubia mkutano wa hadhara jana jioni katika uwanja wa Sahara mjini Mwanza, Zitto alisema amesikia kuna kikao kilichofanyika kwa ajili ya kumhujumu Mengi kwa kuwa vyombo vyake vya habari vimekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi.

Alisema ni aibu kwa viongozi waandamizi wa serikali kukaa na kupanga kuwahujumu watu ambao wanataka kusaidia taifa badala ya kujadili mambo muhimu yanayolikabili taifa.

Alisema kutokana na mpango huo kuwahusisha vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuna haja ya wazee wa chama hicho kuwaita vijana wao na kuwafundisha nini maana ya kuwa viongozi, kuzingatia maadili ya uongozi na kuepukana na kauli ambazo zinaweza kulisababishia taifa matatizo.
 
Mengi angekuwa muungwana naye si angetaja jina la huyo waziri mambo ya kutufumbia mafumbo tena ya nini?

Mhemshimiwa Mengi was right since the message was anonymous na alimjua pengine kwa utafiti wake binafsi na timu ya usalama wake. Kusema vile pia nayer alibidi ku-react anonymously ili naye ajue anonymously amejulikana na kwamba ngoma yake ni kitoto. Unajua mtu ukipata madaraka ghafla na kuisau shida ghafla utendaji huwa kama watu wote no ngombe na hawana intelijensia. Waache hizo!!!! Era hii ni mbaya sana ambayo hata watoto wadogo wana maswali yasiojibika kwa viongozi wetu sembuse MENGI!!! They must be running mad shortly. Mengi utashinda kwani unacheza na timu ya cha ndimu; beckham hachezi cha ndimu, itamwumiza akili. Umecheza mechi nyingi cha ndimu kuanzia kwenye michakato ya ubinafsishaji etc. Kodi walipe au wathibitishe wao kwa mabilion walonayo kwenye account waonyeshe walilipa wapi na kiasi gani ku-amount kwa mabilioni hayo. Wizi mtupu wala walikutishie. Nini?
 
It is once again very interesting and funny too! Hili swala lina manufaa gani kwa jamii kwa sasa. Hat Mengi aliona halina maana sana na ndo sababu akaliweka ki-anonymous, ila wao sasa wanataka liwe public ili wacheze-delay tactics zao kwenye mambo yenye manufaa kwa umma. Why walisitumie strategies hizi hizi kufuatilia mambo yenye msingi kwa taifa? Hapa kuna tatizo la kuhoji kuhusu akili zao!! Really funny!
 
I'm not a lawyer but here is my 2 cents:::

1.Mengi made allegations against people who he did not name as a citizen.
2. Mengi said he has forgiven those people.
3. Let for the sake of discussion say Mengi had no point whatsover, what is he liable for???? As a citizen let us say he had no basis for what he said but rather he is just paranoid, is that illegal???

Masha as a minister has given Mengi 7 days, what if Mengi does nothing within those 7 days?? what will Masha do??? Has it become a crime for citizens to make allegations nowadays?? If the allegations are false, si we just ignore au??????

Masha U are doing things personally while using Govt weight which is a disaster waiting to happen. We know why U are mad son, but U have lost this battle because U are fighting the battle against a citizen who can not lose by merely making allegations no matter how far fetched the allegations are.
 
wud differ here: Mengi ni mtu mtu tajiri na prominent business man hapa kwetu (a successful businessman); Masha ni successful young man to be at his post at that age; they shud have taken a wise decision; and we expect wisdom from the two. For sure hii ndiyo ina prove how hapa kwetu watu wenye vyeo na wenye pesa hawana discipline! These people had time to contact each other even before going to media stalls. They shud be very busy working as they hav more important priorities than what they are doing now! Hapa ni ubabe tu, huyu anajua ana cheo na huyu anajua anayo-pesa; cowards!

approach was to seek elders or even the president and talk it friendly!

IO,
I think you are forgetting "mafahali wawili hawakai zizi moja". I agree with you that both men are successful in their own right. They just need to learn to play fair and get along!
 
hebu msome kwa kutulizana, ama sivyo nyie ndio mnakuwa (as you like to put it) "wakurupukaji"

mleta habari hapo juu amesema, "nimesikia tbc leo asubuhi kwamba mh. Masha kama waziri wa mambo ya ndani amempa siku saba mr mengi athibitishe kauli alizo toa . Kazi imeanza."

keyword, kama waziri wa mambo ya ndani....hivyo, kutokana na habari hapo juu, masha hajasema kuwa mengi athibitishe maneno yale yametoka kwake.

Ama la, labda habari haijakuwa quoted kama ilivyokuwa reported. Slow your roles!

tanzania oyee siasa ya ujamaa na kujitegemea oyeee gurudumu la maendeleo oyee
 
Indeed, you are very right moelex23. That's what I said in my previous post that Masha has misfigured the image of the government in this issue. His political weight was wrongly used, in the name of the state, to try to defend the indefendable (at least in the way he presented it). Consequently, the government suffers from logical public criticism of having incapable ministers in sensitive ministries. It doesn't enter into the mind of an analyst that a mere citizen is given 7 days by the minister to produce evidences of his allegations against an individual. This is merely a minor allegation in the hands of the police force without any necessity of the minister's interventions unless the minister is the one alleged against. If he is the one, then, here is another crystal clear example of the abuse of power. I advise Mr. Mengi not to produce the evidence to the ministry, but, if he wills, to open a file in the court of law against the alleged individual straight away. Evidences for the allegations will be produced there.
 
Masha yani miaka miwili yatari kashainga in the system deep?? dah..nyota yake itazima sasa.................nishai kweli...

Masha ni master kwenye ufisadi pia na yumo kwenye kale ka list ketu ka mafisadi. Ni mtuhumiwa wa Deep Green Finance.
 
Channel Ten inaripoti habari kwa uwazi zaidi kuliko hata ITV. Mmiliki wake sijamsikia popote akilalamika kama alivyo Mzee wetu huyu MZAWA. Mengi na vyombo vyake hivi ana agenda nyingine iliyojificha?

Umewahi kusoma gazeti la This Day au Kulikoni la bwana Mengi?kama hujawahi tembelea maktaba ya taifa omba nakala za zamani spend some days na uzipitie kisha ufananishe na Channel ten.Kumbuka ITV kuna kitu kinaitwa kipima joto ule pia ni msumari tosha kwa Serikali maana vitu vingi vinavyotolewa maoni vinaihusu Serikali moja kwa moja na mara nyingi watu wamekuwa wakipigia kura ya kutoridhiswa na baadhi ya matendo na mabo ya Serikali. Japo yapo mengine ya jamii kwa ujumla lakini kwa wingi ni ya Serikali.

Tafakari
Chukua Hatua!!!
 
Serikali ya kishikaji kamwe haiwezi kuongoza nchi: Raia watagoma, watazomea, watapiga mawe misafara, ...... hatimaye kuondoa utawala husika madarakani. It is a shame for Masha - the minister mshikaji!
 
Umewahi kusoma gazeti la This Day au Kulikoni la bwana Mengi?kama hujawahi tembelea maktaba ya taifa omba nakala za zamani spend some days na uzipitie kisha ufananishe na Channel ten.Kumbuka ITV kuna kitu kinaitwa kipima joto ule pia ni msumari tosha kwa Serikali maana vitu vingi vinavyotolewa maoni vinaihusu Serikali moja kwa moja na mara nyingi watu wamekuwa wakipigia kura ya kutoridhiswa na baadhi ya matendo na mabo ya Serikali. Japo yapo mengine ya jamii kwa ujumla lakini kwa wingi ni ya Serikali.

Tafakari
Chukua Hatua!!!

Tangu lini kuikosoa serikali imekuwa kosa namna hiyo?
 
- Hoja hujibiwa kwa hoja, sio lazima wote tuwe upande mmoja ili kutowaboa wengine, anyways nimekusikia sasa ngoja niwaachie wote wa upande mmoja mjadiliane ili msiboane, maana tusipokubali kuwa upepo wa bendera basi tunaboa, you got it!

- Hayo magazeti ya Mengi si ndiyo yaliyokuwa yakiwasifia Mtandao, hawa kina Masha kwenye kampeni za urais au sio yenyewe? Na huyu si ndiye yule yule Mewngi aliyekwua rafiki wa karibu sana wa Mkapa, au? Anyways nisije nikawaboa zaidi kwa hiyo I am out!
Thanxs and out!

Mkuu FMES, heshima yangu ni kubwa sana kwako na hii inatokana na unavyojua kujibu hoja na kutuletea news zenye uhakika hapa JF, Lakini kwa hili hapa kwa kweli linalonijia hara haraka kichani mwangu ni kufikiri kuwa inawezekana unamgongano wa kimasilahi na hii kampuni ya Mengi maana sikutarajia mtu kama wewe kuanza kumshabikia Masha while amechemka, kama umemsoma mengi alichoeleza nafikiri huna sababu ya kumtetea huyu Masha, jamaa amechemka na asipo anagalia ataaibika maana always Mengi husema kitu ambacho anauhakika na ushahidi hawezi kukurupuka kwa kutoa tuhuma kama hizo, anyway ngoja tuone siku saba si nyingi ingawa Menfi amesema hizo siku saba ni nyingi sana kwake na kama vipi huyo waziri aende mahamani anytime
 
JokaKuu,

Inaelekea huijui hiyo iliyokuwa sheria ya JKT. Masha kama Mtanzania alitakiwa kupitia JKT kabla ya kuingia mlimani.

Kama angesoma huko nje muda wote mpaka university na kisha kuamua kurudi TZ kufanya kazi, bado angetakiwa kwenda JKT kwanza.

Mtanzania inaelekea wewe ndo umechanganya mambo. Ulilazimika kupitia JKT kama
a) ulisoma sekondari A level ya serikali
b) ulitaka kusoma UDSM chini ya udhamini wa serikali
c) ulitaka kufanya kazi serikalini

Sasa zamani ilikuwa no way kwa sababu ajira zote zilitoka serikalini lakini miaka ile ya Masha masharti yalibadilika na wengi waliamua kutokwenda jeshini kama walijua wanapata private sponsorship au kusoma nje na walikuwa hawana mpango wa kuajiriwa serikalini.
Mtu aliyemaliza Form 4 kwa mfano alikuwa pia haendi jeshini.
 
- Hoja hujibiwa kwa hoja, sio lazima wote tuwe upande mmoja ili kutowaboa wengine, anyways nimekusikia sasa ngoja niwaachie wote wa upande mmoja mjadiliane ili msiboane, maana tusipokubali kuwa upepo wa bendera basi tunaboa, you got it!

- Hayo magazeti ya Mengi si ndiyo yaliyokuwa yakiwasifia Mtandao, hawa kina Masha kwenye kampeni za urais au sio yenyewe? Na huyu si ndiye yule yule Mewngi aliyekwua rafiki wa karibu sana wa Mkapa, au? Anyways nisije nikawaboa zaidi kwa hiyo I am out!

Thanxs and out!

FMES mkuu, heshima mbele, naomba nikusahihishe kidogo Mengi na Mkapa ni paka na panya. Mengi hafanyi siri ya kuwa Mkapa alimwekea vikwazo katika mipango yake mingi sana ya biashara lakini kilichobaki kama doa na kufanya Mengi aweke kinyongo kwa Mkapa ni Kilimanjaro hotel alafu Kiwira. Nadhani wewe mkuu unaweza kupata taarifa zote kuhusu ishu hii bila mimi kuweka zaidi hapa. Asante
 
1.
Mkuu FMES, heshima yangu ni kubwa sana kwako na hii inatokana na unavyojua kujibu hoja na kutuletea news zenye uhakika hapa JF,

- Ahsante mkuu na heshima ikurudie pia, ingawa nilishamua kutoka hii mada lakini sina taizo kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu wa kuelewa.

2.
Lakini kwa hili hapa kwa kweli linalonijia hara haraka kichani mwangu ni kufikiri kuwa inawezekana unamgongano wa kimasilahi na hii kampuni ya Mengi

- Ina maana msimamo wako huu ni kwa sababu una mgongano wa kimasilahi na waziri wa ndani, au?

3.
maana sikutarajia mtu kama wewe kuanza kumshabikia Masha while amechemka, kama umemsoma mengi alichoeleza nafikiri huna sababu ya kumtetea huyu Masha, jamaa amechemka na asipo anagalia ataaibika

- Kutofautiana kwetu mawazo haina maana ya ushabiki wa anything, ila ni ku-practice demokrasia to the fullest, mtizamo wako ni kwamba hapa kuna kushabikia mtu, mtizamo wangu ni kwamba hapa kuna utata wa kisheria unahitaji kutatuliwa na pande zote mbili zipewe haki kisheria na ni lazima hii ishu iende kwenye sheria, kusiwe na anything less ili kupata ukweli wa kina na kwa faida ya wananchi in the future.

- Eti waziri wa jamhuri anachemka kwa kusimamia sheria za jamhuri ya kuwalinda wananchi wake ndani ya taifa?


4.
maana always Mengi husema kitu ambacho anauhakika na ushahidi hawezi kukurupuka kwa kutoa tuhuma kama hizo, anyway ngoja tuone siku saba si nyingi ingawa Menfi amesema hizo siku saba ni nyingi sana kwake na kama vipi huyo waziri aende mahamani anytime

- Mkuu taifa limedumaa kwa sababu ya kutotii sheria, hakuna anayemkatalia Mengi kuwa ana uhakika na anachokisema, lakini ninasema hivi lazima kuwa na utaratibu kisheria, Mengi ana uhakika basi aupeleke kwenye sheria ili kama ni waziri mwenye makosa aabike not only kisheria bali hapa sasa hoja ya kumtaka ajiuzulu inakua na nguvu akifikia mahali akiabika kisheria,

- Sina tatizo na Mengi as individual anajua hilo, lakini nina tatizo kubwa na the way alivyoi-handle hii ishu, in fact toka ile ishu ya mashehe nilishaanza kua na wasi wasi naye na agenda zake, mkuu hili litakua ni taifa la namna gani ambalo wananchi watakurupuka tu na kuwarekodi wengine kwenye video na tapes, halafu kwenda kwenye media na kuwatishia nazo, wewe huoni kuwa huo ni u-Banana Republic? Sheria iko wapi?

- Sasa mwananchi anadai kuna waziri anamhujumu, kudai wkangu sheria itumike kuamua ukweli wa hii tuhuma kunanifanya niwe na beef na kampuni za Mengi? Hujanitendea haki hapo mkuu!
 
NN, issue ya Mengi na CTN ilikuwa ni kuhusu nani ana rights za kuonyesha World Cup 94, mwishoni Mengi alilalamika sana akaishia kuweka giant screen Mnazi Mmoja gardens na akapewa ulinzi na serikali. Lakini hakuthibitisha hayo madai.

Mkapa alihakikisha Mengi hapati ile treatment aliyokuwa anaipata wakati wa Mwinyi alimfungia milango yote ya kuingia Ikulu anapojisikia ndio maana leo sishangai kuona magazeti yake yako kooni kwa Mkapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom