Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
You know,

Unabonda, unabonda, halafu unarudia kile kile ulichobonda!Unapoteza moral authority yote uliyojenga katika kubonda. Zaidi ya hapo, ili kumuonyesha mtu aliyefanya "name calling" kuwa ni mtu frivolous, dispute name calling kwa kuonyesha ilipo wrong. Unasema mimi ni Press Secy wa Masha siyo, ona hapa nilimsema hivi, hapa nilimhold responsible hivi, hivyo siwezi kulinganishwa na Press Secy. Otherwise kukuita Press Secy kunaweza kuwa a bit below the belt, but will actually encompass a shorthand and concise reflection of what a politically correct description could take a whole paragraph or two.

- Name calling ina maana moja tu nayo ni kutokuwa na hoja.
 
Mengi jino kwa jino na Masha

Habari Zinazoshabihiana
• Polisi avunjwa jino kwa chupa ya bia 03.08.2007 [Soma]
• Shekhe jino kwa jino na Mchungaji kuhusu Dito 22.03.2007 [Soma]
• Kupanda kwa bei za mafuta:Masha asema Serikali inafanyia kazi mapendekezo 27.05.2006 [Soma]

*Serikali yampa siku saba ajieleze kuhusu kutishwa
*Yeye asema nyingi, amtaka Waziri ampeleke kortini

Na Waandishi Wetu

SERIKALI imempa siku saba Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi, kuthibitisha madai yake kwamba kuna waziri kijana katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete amemtishia na kwamba kuna mikakati ya kufilisi biashara zake.

Akizungumza na Kituo cha Televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) na kurushwa jana asubuhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha, alisema madai yaliyotolewa na Bw. Mengi yanaonesha kwamba Serikali haiwalindi vyema raia wake.

Waziri Masha alisema Mwenyekiti huyo anapaswa katika muda huo awe amethibitisha madai hayo, ili Serikali iweze kuangalia taratibu za kuyashughulikia.

Alisema jana angemwandikia rasmi barua ya kumtaka kuthibitisha madai yake ambayo aliyatoa juzi mbele ya vyombo vya habari, Dar es Salaam.

Kabla ya kutolewa agizo hilo jana, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilisema lilikuwa halijapokea taarifa yoyote kutoka kwa Bw. Mengi kuhusu kutishiwa na Waziri na hivyo lisingeweza kuliingilia suala hilo.

Akizungumza na Majira, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Evarist Mangala, alisema hadi juzi Desemba 3 hawakuwa na taarifa yoyote ambayo iliripotiwa kuhusu kutishiwa maisha kwa Bw. Mengi na badala yake walizisoma taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Kuhusu siku saba alizopewa na Bw. Masha kuwasilisha ushahidi wake, Bw. Mengi alisema siku hizo ni nyingi na kumtaka Waziri kumpeleka Mahakamani haraka iwezekanavyo.

"Vitisho ni vingi sana, lakini si kila kitu ninaweza kupeleka taarifa Polisi, hivyo ninaangalia kikubwa ni kipi kinachotisha zaidi ndipo ninatoa taarifa Polisi, lakini iwapo itagundulika kuwa niliudanganya umma kuwa nilitoa taarifa katika kituo cha Polisi wakati sijatoa, niko tayari kwenda jela,

"Lakini pia iwapo itagundulika kuwa Waziri pia ameudanganya umma kuwa sikutoa taarifa Polisi wakati nilitoa, je yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake?" alihoji Bw. Mengi.

Kuhusu suala la kumtaja Waziri kijana na msomi aliye katika Wizara nyeti, Bw. Mengi alisema kwa kawaida Mwenyezi Mungu ana nguvu kubwa na za kipekee, hivyo zinaweza kumfanya mtu huyo kujitaja mwenyewe.

"Kwa kawaida Mungu ana nguvu kubwa na za pekee sana, hivyo katika mazingira ya sasa, nguvu hizo zinaweza kumfanya mhusika kujitaja mwenyewe," alisema.

Bw. Mengi alisema ameshindwa kuelewa majukumu ya Waziri Masha katika jambo hili alilosema kupitia TBC1, kwani hajawahi kusikia kama yeye ni Msemaji Mkuu wa Serikali au wa Wizara.

"Kitu nisichokielewa ni majukumu ya Waziri Masha katika suala hili, alikuwa akitoa tamko hilo kama Msemaji Mkuu wa Wizara au Serikali, alikuwa akizungumza kama nani, nauliza hivyo kwani sijui taratibu za Serikali kama yeye ni msemaji wa sehemu hizo.

"Nilizungumzia Waziri kijana wa wizara nyeti, mawaziri vijana wako wengi, yuko Ngeleja (William, 41), Kamala (Deodorus, 40) na yeye Masha (38) hivyo umri wao unashabihiana, sijui atakuwa amezungumza kwa niaba ya vijana wengine ama vipi?," alisisitiza Bw. Mengi.

Bw. Mengi alihoji kuwa iwapo suala la kuripoti Polisi linalomhusu yeye katika Wizara yake ameshindwa kukubaliana nalo, je kuwapo kwa suala la kumfilisi ambalo haliko katika wizara yake, atakuwa tayari kulikubali?

Waziri Masha alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la kumpeleka Bw. Mengi mahakamani haraka iwezekanavyo na kumpelekea barua ikimtaka kutoa ushahidi ndani ya siku saba, alisema suala la kumpa siku saba Bw. Mengi si sababu, hivyo angeweza kupeleka ushahidi huo hata jana.

Bw. Masha alisema alishindwa kupeleka barua hiyo jana asubuhi, kutokana na kuwa mkutanoni, hivyo aliahidi mara baada ya kutoka mkutanoni angeipeleka barua hiyo mara moja.

Hata hivyo, hakuweza kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, kutokana na kuwa mkutanoni na Waziri mwenzake wa Burundi.

Awali vyombo vya habari viliripoti kuwa Bw. Mengi anadai kutishiwa kifo na mtu aliyemtaja kuwa ni Waziri kijana katika Serikali ya Rais Kikwete akihusisha vitisho hivyo na msimamo wake wa kukemea ufisadi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao ulifanyika juzi, Mengi alidai kuwa amekuwa akitumiwa ujumbe ambao unavituhumu vyombo vyake vya habari kuwa vimekuwa mstari wa mbele katika kukemea ufisadi jambo ambalo 'waziri kijana' kuwa si jambo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

huenda suala hili litasaidia wananchi kujua sheria zinasemaje kuhusu mwanachi
kulalamika hadharani (kutumia vyombo vya habari) kuhusu usalama wao.

huenda na mwakilishi wa maalbino akatakiwa athibitishe kauli yake iliyounganishwa na madai ya kumtaka waziri ajiuzuru kwani waziri amekanusha
na kudai hakusema hivyo. labda na yeye ataandikiwa barua na asipotoa ushahidi atapelekwa kwa pilato.

kama hiyo barua haitakuwa tayari leo jioni ni vyema waziri akumbuke kuiacha hiyo barua tayari kabla hajasafiri kikazi (nje ya nchi) wiki ijayo. itakuwa vizuri wananchi tukijulishwa kufikishwa kwa barua hiyo kwani naamini wapo wengi tu wanaofuatilia kuona mengi kama mengi atawasilisha ushahidi au atabana tu.

sasa najua naweza ambiwa haya mambo ya barua ni masuala ya kiserikali
lakini si ndo tushaonjeshwa "trailer" kwanini mtu asidai kuona "full movie"?

oops! sasa hizo siku saba zitaanza kuhesabika kuanzia lini?
 
1.
Binafsi natatizwa mno na kauli ya Masha. Napata picha kuwa hakuwa makini na alikurupuka. Pengine dhamira inamsuta kuwa ndiye aliyepeleka vitisho hivyo na sasa anajihami kutumia madaraka yake au ni ulevi wa madaraka unaopumbuza uwezo wa kufikiri.

- Waziri wa ndani ni wajibu wake kusimamia taifa na hasa usalama wa raia Mengi akiwemo pia, waziri amewakilisha msimamo wa serikali kuhusu madai ya Mengi ambayo yana tatizo kwa taifa, kama sheria iko kwa Mengi basi itaonekana kwenye sheria, lakini hakuna aliyekurupuka ni sheria ndio itaamua nani aliyekurupuka, sasa hivi ni mapema mno kusema what is what!

2.
Natatizwa na kauli yake kwasababu:
(1) Amekurupuka kutangaza hadharani kabla hajampelekea mhusika barua, na hata hiyo barua ilikuwa haijaandikwa wakati anatangaza. Je kulikuwa na haraka gani? Tangazo lenyewe litadumu kwa siku 7!
(2). Akipata hivyo vielelezo na kama vinamuhusu yeye binafsi kama Masha, atafanya nini? Maana naye yumo katika hiyo probability (1/3).
(3). Ni kwanini adai vielelezo vipelekwe wizarani wakati utaratibu wa kawaida unafahamika kuwa hayo ni masuala ya polisi na mahakama? Yeye kama waziri, si ingetosha kumshauri Bwana Mengi, tena si lazima kupitia TBC, kufungua kesi ya kutishiwa kuuawa na kupeleka vielelezo vyake mahakamani ili mhusika wa vitisho awajibishwe kwa mujibu wa sheria.
(4). Kama anafikiri maelezo ya Bwana Mengi yameiumbua serikali, basi serikali haiwezi kuwa hakimu wa kesi yake mwenyewe kwa kudai vielelezo kutoka kwa mtuhumiwa wake - Bwana Mengi. Serikali ilipaswa kufungua kesi dhidi ya Mengi ili Mengi alioshe jina la serikali mahakamani.

Napata wasiwasi kuwa kwa mtindo wa kufikiri wa Masha, serikali haina kiongozi katika wizara hii. Namshauri kwa dhati kabisa Bwana Mengi asipeleke vielelezo vyake wizarani. HAKUNA MANTIKI yeyote ya kufanya hivyo. Hata akiletewa barua (kichekesho: barua inafuata tangazo!!!!), aijibu barua hiyo kwa kumwambia waziri apeleke suala hili mahakamani na yeye (Mengi) atoe vielelezo vyake mahakamani kama mshtakiwa.

- Serikali imetatizwa na kilio cha mwananchi wake yaani Mengi, na imemtuma waziri wake kuhakikisha haki inatendeka kisheria, kama waziri ambaye ni serikali yuko wrong basi sheria itasema kama vile Mkapa alipofukuza kazi wakuu flani BOT sheria ikamkuta kua alikuwa wrong ingawa alikuwa rais, serikali ikaamuriwa iwalipe fidia wale maofisa wa BOT, na this one too sheria ifuate mkondo wake mwenye makosa atabainika na kupewa ukweli wake kisheria kama ni waziri na serrikali yake, au Mengi ndio maana ya utawala wa sheria, maana hapa it not abpout Mengi, it si about sheria na taifa letu.

3
. Binafsi, nalichukulia tangazo la Masha kama la kitoto. Halipaswi kutolewa na waziri kwa namna alivyoitoa. Masha anaiaibisha serikali, wizara na taaluma yake ya sheria.

- Nafikiri mwananchi yoyote mwenye akili timamu ataamua mwenyewe kwamba ni lipi hapa ni tangazo la kitoto, kati ya lile la Mengi la kudai kuna "waziri flani kijana ananifuata fuata" na tamko la serikali la kumtaka Mengi awakilishe madai katika misingi ya kisheria, ili serikali iweze kumsaidia.

- But unazo some strong points, lakini sio jinsi the ishu ilivyokaaa umewahi kabla ya wakati mkuu.

Heshima mbele!
 
1. Ni huyu Masha aliyehusika kwa namna moja ama nyingine katika usajili wa kampuni ya Deep Green akiwa mkurugenzi wa IMMA.
2. Ni huyu Masha ambaye kama Waziri mdogo wa Nishati na Madini alibana kimya wakati wa Richmonduli akidai hahusiki.
3. Ni huyu Masha akiwa Waziri wa mambo ya nndani aliyekimbilia kumtetea Ridhwani kwa misingi isiyoeleweka.
4. Ni huyu Masha alizomewa kwenye jimbo lake akijaribu kutetea mikataba mibovu ya madini.
5. Ni huyu Masha waziri wa mambo ya ndani aliyewatembelea kwa siri MAFISADI walioswekwa lupango, Keko.
6. Ni huyu Masha, Waziri katika serikali ya JK, anayetoa siku saba kwa mzalendo anayehofia usalama wake !!!!
7. Ni huyu Masha n.k Grrrrrrrr!! Grrrrrrr!! Grrrrr!!

Na si peke yake, serikali nzima imejaa watu aina ya Masha. Nikilalamika naambiwa nina chuki binafsi. Katika hali hii wanyonge twende wapi ?
 
Bw. Masha alisema alishindwa kupeleka barua hiyo jana asubuhi, kutokana na kuwa mkutanoni, hivyo aliahidi mara baada ya kutoka mkutanoni angeipeleka barua hiyo mara moja.

- Serikali haina haraka, waziri ndio kwanza amerudi jana usiku kutoka South Africa, kwenye ziara ya kikazi kwa hiyo hili la barua kupelekwa sio tatizo,

tatizo ni kuna tunaotaka kuona haki inatendeka kisheria kwa pande zote mbili, yaani serikali na Mengi, kwa faida ya wananchi at large in the future!
 
You know,

Unabonda, unabonda, halafu unarudia kile kile ulichobonda!

Unapoteza moral authority yote uliyojenga katika kubonda.

Zaidi ya hapo, ili kumuonyesha mtu aliyefanya "name calling" kuwa ni mtu frivolous, dispute name calling kwa kuonyesha ilipo wrong. Unasema mimi ni Press Secy wa Masha siyo, ona hapa nilimsema hivi, hapa nilimhold responsible hivi, hivyo siwezi kulinganishwa na Press Secy.

Otherwise kukuita Press Secy kunaweza kuwa a bit below the belt, but will actually encompass a shorthand and concise reflection of what a politically correct description could take a whole paragraph or two.

Wali aliyehukumiwa kwamba ni press Secy wa Masha sio mimi. Mimi sishabiki watu. Mimi nazungumzi maantiki ya kuweka vipande vya sentesi kwenye argument yako ambavyo havisaidii kujenga rgument yako; vina mdistract tu mtu.

Mara nyingi unaona mtu anaanza kwa "Wewe jamaa mjinga sana, hushirikishagi akili ndo maana demu wako kakuacha ..." halafu ndio anaweka rgument yake sasa kuhus Mengi na Masha. lol

Sawa pengine ningetakiwa kuonyesha kwamba kumfananisha jamaa na press secretary haisaidii argument yake, lakini pengine yeye pia alitakiwa atuonyeshe tu jinsi argument ya mshkaji ilivyo na mkanganyiko, au una wazo tofauti? Kuchomekea press watever ni unnecessary distruction tu, kwa maoni yangu, na saa nyingine inasaidia tu kuonyesha hasira ya mtu na si kuipa argument yake uzito unaostaili.

Heshima mbele.
 
Kuchomekea press watever ni unnecessary distruction tu, kwa maoni yangu, na saa nyingine inasaidia tu kuonyesha hasira ya mtu na si kuipa argument yake uzito unaostaili.

- Finally a clear point, maana mengine sina uhakika na kinachosemwa!
 
- Unajua siku hizi nimegundua kua kuwa mpole na kuwa msikivu kwa maana ya kwako hapa JF ni kufuata bendera ya mtu mmoja humu, I am not ready for that ninakuja hapa kukata ishus sio kujikomba kwa mtu, never!

Labda nimeshindwa kujieleza vizuri. Siwezi kusema kwamba kubali kila wengine wanachosema. La hasha. Kuwa na msimamo wako, na jitahidi kadri unavyoweza kuhakikisha msimamo wako ni sahihi. Mkosoe kwa nguvu yeyote unayedhani msimamo wake au mawazo yake si sahihi kwa kumuonesha kosa liko wapi katika argument yake, na si kumtukana au kumwambia huwa kawaida ana mawazo potofu kwa hiyo na hilo ni potofu.

Lengo likiwa ni kujadiliana na si kulumbana, utaona jinsi mijadala inavyokuwa mitamu.

- Sasa be who you are na mimi niache niendelee kuwa nilivyo lakini tukate ishus za taifa wka kutii sheria za JF, maana mimi I do not care kama wewe ni msikvu au hapana, maana tabia zako it is none of my business!. Halafu please can we talk kuhusu Mengi na Masha kuliko mimi zaidi maana unaweza kufungua thread kuhusu mimi if you want!

Thanxs na nitarudi later!
lol

Amina Baba.

I hope lakini humaanishi kwamba hairuhusiwi kukukosoa ukichemka.
 
- Serikali haina haraka, waziri ndio kwanza amerudi jana usiku kutoka South Africa, kwenye ziara ya kikazi kwa hiyo hili la barua kupelekwa sio tatizo,

tatizo ni kuna tunaotaka kuona haki inatendeka kisheria kwa pande zote mbili, yaani serikali na Mengi, kwa faida ya wananchi at large in the future!

Serikali haina haraka?
Nani aliyetoa siku saba?Sasa hizo siku saba zinatakiwa kimaandishi .
Pia mbona unakuwa unasema unavyosema kuhusu waziri na mambo kama hizi mpaka kupelekea watu kuuliza kuwa wewe ni msemaji wake " press secretary"

Kwa taharifa ya karibuni ni kuwa Mengi kasema hizo siku saba ni nyingi afanye hima apeleke mambo mahakamani .Kwa hiyo hapa watu wenye vitengo vyao ndio wapewe ushahidi .

Hapa ndio mimi nilikuwa nasubiri kitu "mahakamani"
 
Nimesikia TBC leo asubuhi kwamba Mh. Masha kama Waziri wa Mambo ya Ndani amempa siku saba Mr Mengi athibitishe kauli alizo toa . Kazi imeanza.
Mengi jino kwa jino na Masha

Habari Zinazoshabihiana
• Polisi avunjwa jino kwa chupa ya bia 03.08.2007 [Soma]
• Shekhe jino kwa jino na Mchungaji kuhusu Dito 22.03.2007 [Soma]
• Kupanda kwa bei za mafuta:Masha asema Serikali inafanyia kazi mapendekezo 27.05.2006 [Soma]

*Serikali yampa siku saba ajieleze kuhusu kutishwa
*Yeye asema nyingi, amtaka Waziri ampeleke kortini

Na Waandishi Wetu

SERIKALI imempa siku saba Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi, kuthibitisha madai yake kwamba kuna waziri kijana katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete amemtishia na kwamba kuna mikakati ya kufilisi biashara zake.

Akizungumza na Kituo cha Televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) na kurushwa jana asubuhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha, alisema madai yaliyotolewa na Bw. Mengi yanaonesha kwamba Serikali haiwalindi vyema raia wake.

Waziri Masha alisema Mwenyekiti huyo anapaswa katika muda huo awe amethibitisha madai hayo, ili Serikali iweze kuangalia taratibu za kuyashughulikia.

Alisema jana angemwandikia rasmi barua ya kumtaka kuthibitisha madai yake ambayo aliyatoa juzi mbele ya vyombo vya habari, Dar es Salaam.

Kabla ya kutolewa agizo hilo jana, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilisema lilikuwa halijapokea taarifa yoyote kutoka kwa Bw. Mengi kuhusu kutishiwa na Waziri na hivyo lisingeweza kuliingilia suala hilo.

Akizungumza na Majira, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Evarist Mangala, alisema hadi juzi Desemba 3 hawakuwa na taarifa yoyote ambayo iliripotiwa kuhusu kutishiwa maisha kwa Bw. Mengi na badala yake walizisoma taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Kuhusu siku saba alizopewa na Bw. Masha kuwasilisha ushahidi wake, Bw. Mengi alisema siku hizo ni nyingi na kumtaka Waziri kumpeleka Mahakamani haraka iwezekanavyo.

"Vitisho ni vingi sana, lakini si kila kitu ninaweza kupeleka taarifa Polisi, hivyo ninaangalia kikubwa ni kipi kinachotisha zaidi ndipo ninatoa taarifa Polisi, lakini iwapo itagundulika kuwa niliudanganya umma kuwa nilitoa taarifa katika kituo cha Polisi wakati sijatoa, niko tayari kwenda jela,

"Lakini pia iwapo itagundulika kuwa Waziri pia ameudanganya umma kuwa sikutoa taarifa Polisi wakati nilitoa, je yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake?" alihoji Bw. Mengi.

Kuhusu suala la kumtaja Waziri kijana na msomi aliye katika Wizara nyeti, Bw. Mengi alisema kwa kawaida Mwenyezi Mungu ana nguvu kubwa na za kipekee, hivyo zinaweza kumfanya mtu huyo kujitaja mwenyewe.

"Kwa kawaida Mungu ana nguvu kubwa na za pekee sana, hivyo katika mazingira ya sasa, nguvu hizo zinaweza kumfanya mhusika kujitaja mwenyewe," alisema.

Bw. Mengi alisema ameshindwa kuelewa majukumu ya Waziri Masha katika jambo hili alilosema kupitia TBC1, kwani hajawahi kusikia kama yeye ni Msemaji Mkuu wa Serikali au wa Wizara.

"Kitu nisichokielewa ni majukumu ya Waziri Masha katika suala hili, alikuwa akitoa tamko hilo kama Msemaji Mkuu wa Wizara au Serikali, alikuwa akizungumza kama nani, nauliza hivyo kwani sijui taratibu za Serikali kama yeye ni msemaji wa sehemu hizo.

"Nilizungumzia Waziri kijana wa wizara nyeti, mawaziri vijana wako wengi, yuko Ngeleja (William, 41), Kamala (Deodorus, 40) na yeye Masha (38) hivyo umri wao unashabihiana, sijui atakuwa amezungumza kwa niaba ya vijana wengine ama vipi?," alisisitiza Bw. Mengi.

Bw. Mengi alihoji kuwa iwapo suala la kuripoti Polisi linalomhusu yeye katika Wizara yake ameshindwa kukubaliana nalo, je kuwapo kwa suala la kumfilisi ambalo haliko katika wizara yake, atakuwa tayari kulikubali?

Waziri Masha alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la kumpeleka Bw. Mengi mahakamani haraka iwezekanavyo na kumpelekea barua ikimtaka kutoa ushahidi ndani ya siku saba, alisema suala la kumpa siku saba Bw. Mengi si sababu, hivyo angeweza kupeleka ushahidi huo hata jana.

Bw. Masha alisema alishindwa kupeleka barua hiyo jana asubuhi, kutokana na kuwa mkutanoni, hivyo aliahidi mara baada ya kutoka mkutanoni angeipeleka barua hiyo mara moja.

Hata hivyo, hakuweza kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, kutokana na kuwa mkutanoni na Waziri mwenzake wa Burundi.

Awali vyombo vya habari viliripoti kuwa Bw. Mengi anadai kutishiwa kifo na mtu aliyemtaja kuwa ni Waziri kijana katika Serikali ya Rais Kikwete akihusisha vitisho hivyo na msimamo wake wa kukemea ufisadi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao ulifanyika juzi, Mengi alidai kuwa amekuwa akitumiwa ujumbe ambao unavituhumu vyombo vyake vya habari kuwa vimekuwa mstari wa mbele katika kukemea ufisadi jambo ambalo 'waziri kijana' kuwa si jambo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.
 
I hope lakini humaanishi kwamba hairuhusiwi kukukosoa ukichemka.

- Hopefully siku za karibuni kuna mtu hapa JF atatunga wimbo mpya maana huu umeshakua zilipendwa, nikisha tofautiana mawazo na mtu hapa basi lazima huu wimbo upigwe hebu tafuteni mpya wakuu!

By the way Mkuu Manitoba, heshima mbele sana maana it is a long time toka nimewahi kufikira mara mbili kabla ya kuandika, damn it! vigongo vyako ni lazima kufikiria mara mbili kabla ya kujibu, saafi sana na I appreciate your debate's skills,

again respect!
 
1.
Serikali haina haraka? Nani aliyetoa siku saba?Sasa hizo siku saba zinatakiwa kimaandishi .

- Ulishawahi kumsikia baharia mwenzangu kwa jina Memba? Unajua serikali ilimsubiri kwa muda gani? Sasa what is the point siku saba zimeisha?

2.
Pia mbona unakuwa unasema unavyosema kuhusu waziri na mambo kama hizi mpaka kupelekea watu kuuliza kua wewe ni msemaji wake yaani " press secretary" wa waziri?

- Name calling ina maana moja tu kuwa hakuna hoja, by the way jana Shy ndiye aliyekua wa kwanza kusema hili kuwa waziri yuko SA, je "wewe na hao watu" wako hamkuamua kwua na yeye ni press secretary wake waziri?

3.
Kwa taharifa ya karibuni ni kuwa Mengi kasema hizo siku saba ni nyingi afanye hima apeleke mambo mahakamani .Kwa hiyo hapa watu wenye vitengo vyao ndio wapewe ushahidi . Hapa ndio mimi nilikuwa nasubiri kitu "mahakamani"

- Waziri ndiye anayeongoza serikali, Mengi ni mwananchi ni lazima akubali mwongozo wa serikali unaotolewa na waziri kwa niaba yake, amepewa siku saba na serikali imemuahidi kuwa atapewa barua, na mambo yata-move from there not otherwise, maana Mengi haipi amri serikali, hapa tunasubiri haki itendeke kwa Mengi na serikali pia through sheria.

Thanxs! Kesho saaa ya kulala sasa!
 
Mi nadhani, kwa sababu Mengi alimtuhumu waziri (kwa kutaja cheo cha uwaziri wa Serikali ya Tz) basi anakuwa ameituhumu serikali.
Kwa hiyo Masha hapa anafanya kazi ya kuitetea Serikali hata kama aliyetuhumiwa si yeye......japo pia naona kwa upande wa pili aliyepaswa kuliongolea ni hili ni yule waziri aliyesuswa na media.

Kwa nini akurupuke wakati Mengi mwenyewe alishapeleka taarifa Polisi? Kinachotakiwa ni kuwaachia Polisi na vyombo vya usalama vifanye kazi yao. Pamoja na hayo siamini kama hivyo vyombo vitatenda kwa ufanisi na haki kama jamaa alishaanza ku-act kama hivyo. Jina halijatajwa, yeye tayari kisharuka futi 20 na kutoa siku 7. Kazi iko na utamu waja, tega kombe.
 
Now back to the ishu, can we talk the ishu now yaani Mengi Vs Waziri! /QUOTE]

Yes we can. Natumani unaelewa tofauti ya kujua na kuamini lakini. Kuamini si kwenye dini tu, kuchukulia mambo ambayo hayajathibitika kama vile ni ya kweli ni kuamini pia. Na ni ruksa kabisa, ila noma ni pale unapowalazimishia wenzako waichukulie tu imani yako kama ndio kweli bila kukuuliza.

Labda nijaribu kuweka kwa urahisi kidogo.

Hakuna mtu anayejua kwa hakika hapa kama hayo ambayo Mengi ameyasema yalisemwnwa na waziri kijana yamesemwa kweli ama la. Kama wewe unajua tuambie.

Lakini naweza kuamini kuna uwezekano; haitakuwa mara ya kwanza mtanzania kubambikiziwa kodi. Hata waziri mkuu majuzi juzi alikiri hilo kwenye siku ya walipa kodi.

Lakini hata kama yalisemwa, hakuna mtu hapa anajua kama mzee Mengi anao ushahidi ama la. Na kama anaoni ni mzito kiasi gani. Lakini mpaka kuamua kusema aliyosema, naamini kuna uwezekano mkobwa mzee Mengi ana kaushahidi analau kadogo.

Kuhusu kama Masha ndiye aliyesema hayo, sijui. Lakini kwa maelezo yanayotolewa na wataalamu kama wewe humu, na kwa reaction ya Mengi leo, naamini kuna uwezekano mkubwa ni yeye.

Kuhusu kama Masha alifanya sawa kuingia TBC na kufanya aliyoyafanya, sijui, hapo mimi bado nawasikiliza wataalamu wa sheria kama wewe na nnazidi kujifunza mengi. Lakini kumuona waziri kwenye panicy mode namna ile ilinifadhaisha kidogo. Na siamini kwamba "he was just doing is job" kama ulivyosema kwa sababu kuna ishu nyingi tu zenye umuhimu pengine kuliko hata hilo lakini hatujaona akilivalia njuga namna hiyo. Inanifanya niamini kuna motives nyingine. Inawezekana pia kwamba hakuna motive nyingine bali ni hasira tu kama ulizonazo wewe kwamba huyu bwana Mengi sasa "amezidi". 🙂

Hayo ndiyo maoni yangu machanga muheshimiwa sana.
 
1.

- Ulishawahi kumsikia baharia mwenzangu kwa jina Memba? Unajua serikali ilimsubiri kwa muda gani? Sasa what is the point siku saba zimeisha?

Oooh Nimesahau kuwa swali huzaa swali ili kupata jibu ikibidi.Je hapa imebidi?
Ok the thing is I dont know who the heck is Memba,so I dont know if that is a vivid example.
Sio lazima ku respond kwa maswali yote kama huna straight answers.

2.

- Name calling ina maana moja tu kuwa hakuna hoja, by the way jana Shy ndiye aliyekua wa kwanza kusema hili kuwa waziri yuko SA,je "wewe na hao watu" wako hamkuamua kwua na yeye ni press secretary wake waziri?

I rather choose not to answer this,naachia hadhira.
3.

- Waziri ndiye anayeongoza serikali, Mengi ni mwananchi ni lazima akubali mwongozo wa serikali unaotolewa na waziri kwa niaba yake, amepewa siku saba na serikali imemuahidi kuwa atapewa barua, na mambo yata-move from there not otherwise, maana Mengi haipi amri serikali, hapa tunasubiri haki itendeke kwa Mengi na serikali pia through sheria.

Thanxs! Kesho saaa ya kulala sasa!
Mr.Mengi kaipa serikali/waziri amri gani?
Mimi naona ka respond kwa swala la siku saba ! kuwa yeye yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani na hata ikiwa kabla ya siku saba.Is that bothering you?
Mwishoni naona tunaenda sawa haki itendeke kwa Mengi na kwa mtuhumiwa waziri kijana

Ooh goodnight sir!
 
Haya tena sakala la Mengi ndiyo linazidi kupamba moto

Imetolewa mara ya mwisho: 06.12.2008 0010 EAT

• Mengi jino kwa jino na Masha

*Serikali yampa siku saba ajieleze kuhusu kutishwa
*Yeye asema nyingi, amtaka Waziri ampeleke kortini

Na Waandishi Wetu
Majira

SERIKALI imempa siku saba Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi, kuthibitisha madai yake kwamba kuna waziri kijana katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete amemtishia na kwamba kuna mikakati ya kufilisi biashara zake.

Akizungumza na Kituo cha Televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) na kurushwa jana asubuhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Laurence Masha, alisema madai yaliyotolewa na Bw. Mengi yanaonesha kwamba Serikali haiwalindi vyema raia wake.

Waziri Masha alisema Mwenyekiti huyo anapaswa katika muda huo awe amethibitisha madai hayo, ili Serikali iweze kuangalia taratibu za kuyashughulikia.

Alisema jana angemwandikia rasmi barua ya kumtaka kuthibitisha madai yake ambayo aliyatoa juzi mbele ya vyombo vya habari, Dar es Salaam.

Kabla ya kutolewa agizo hilo jana, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilisema lilikuwa halijapokea taarifa yoyote kutoka kwa Bw. Mengi kuhusu kutishiwa na Waziri na hivyo lisingeweza kuliingilia suala hilo.

Akizungumza na Majira, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Evarist Mangala, alisema hadi juzi Desemba 3 hawakuwa na taarifa yoyote ambayo iliripotiwa kuhusu kutishiwa maisha kwa Bw. Mengi na badala yake walizisoma taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Kuhusu siku saba alizopewa na Bw. Masha kuwasilisha ushahidi wake, Bw. Mengi alisema siku hizo ni nyingi na kumtaka Waziri kumpeleka Mahakamani haraka iwezekanavyo.

"Vitisho ni vingi sana, lakini si kila kitu ninaweza kupeleka taarifa Polisi, hivyo ninaangalia kikubwa ni kipi kinachotisha zaidi ndipo ninatoa taarifa Polisi, lakini iwapo itagundulika kuwa niliudanganya umma kuwa nilitoa taarifa katika kituo cha Polisi wakati sijatoa, niko tayari kwenda jela,

"Lakini pia iwapo itagundulika kuwa Waziri pia ameudanganya umma kuwa sikutoa taarifa Polisi wakati nilitoa, je yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake?" alihoji Bw. Mengi.

Kuhusu suala la kumtaja Waziri kijana na msomi aliye katika Wizara nyeti, Bw. Mengi alisema kwa kawaida Mwenyezi Mungu ana nguvu kubwa na za kipekee, hivyo zinaweza kumfanya mtu huyo kujitaja mwenyewe.

"Kwa kawaida Mungu ana nguvu kubwa na za pekee sana, hivyo katika mazingira ya sasa, nguvu hizo zinaweza kumfanya mhusika kujitaja mwenyewe," alisema.

Bw. Mengi alisema ameshindwa kuelewa majukumu ya Waziri Masha katika jambo hili alilosema kupitia TBC1, kwani hajawahi kusikia kama yeye ni Msemaji Mkuu wa Serikali au wa Wizara.

"Kitu nisichokielewa ni majukumu ya Waziri Masha katika suala hili, alikuwa akitoa tamko hilo kama Msemaji Mkuu wa Wizara au Serikali, alikuwa akizungumza kama nani, nauliza hivyo kwani sijui taratibu za Serikali kama yeye ni msemaji wa sehemu hizo.

"Nilizungumzia Waziri kijana wa wizara nyeti, mawaziri vijana wako wengi, yuko Ngeleja (William, 41), Kamala (Deodorus, 40) na yeye Masha (38) hivyo umri wao unashabihiana, sijui atakuwa amezungumza kwa niaba ya vijana wengine ama vipi?," alisisitiza Bw. Mengi.

Bw. Mengi alihoji kuwa iwapo suala la kuripoti Polisi linalomhusu yeye katika Wizara yake ameshindwa kukubaliana nalo, je kuwapo kwa suala la kumfilisi ambalo haliko katika wizara yake, atakuwa tayari kulikubali?

Waziri Masha alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la kumpeleka Bw. Mengi mahakamani haraka iwezekanavyo na kumpelekea barua ikimtaka kutoa ushahidi ndani ya siku saba, alisema suala la kumpa siku saba Bw. Mengi si sababu, hivyo angeweza kupeleka ushahidi huo hata jana.

Bw. Masha alisema alishindwa kupeleka barua hiyo jana asubuhi, kutokana na kuwa mkutanoni, hivyo aliahidi mara baada ya kutoka mkutanoni angeipeleka barua hiyo mara moja.

Hata hivyo, hakuweza kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, kutokana na kuwa mkutanoni na Waziri mwenzake wa Burundi.

Awali vyombo vya habari viliripoti kuwa Bw. Mengi anadai kutishiwa kifo na mtu aliyemtaja kuwa ni Waziri kijana katika Serikali ya Rais Kikwete akihusisha vitisho hivyo na msimamo wake wa kukemea ufisadi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao ulifanyika juzi, Mengi alidai kuwa amekuwa akitumiwa ujumbe ambao unavituhumu vyombo vyake vya habari kuwa vimekuwa mstari wa mbele katika kukemea ufisadi jambo ambalo 'waziri kijana' kuwa si jambo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.
 
Iwapo suala hili litaangaliwa kisiasa: Tanzania Waziri akituhumiwa kutoa vitisho kwa Raia anayetakiwa kumtetea Waziri ni waziri wa Mambo ya Ndani au Bosi wa hao Mawaziri? i.e Waziri Mkuu au Raisi.

Iwapo suala hili litaangaliwa kisheria: Anayetakiwa kutoa tamko la kisheria ni Waziri wa Mambo ya Ndani? au ni Polisi, DPP au AG.

Waziri Masha amekurupuka kama alivyokurupuka kwenda Keko; kwa hili anaiaibisha Serikali nzima.
 
Unless we agree to cut through the BS tutakuwa tunazunguka tu in circles! Sasa Mengi angetakiwa ataje straight anamzungmzia nani kama ana ushahidi na amepeleka malalamiko polisi, au sheria inasema tofauti kuhusu kumtaja mtu aliyekutishia?
Lakini kwa upande mwingine nakubaliana na hoja ya YeboYebo kwamba waziri Masha si msemaji wa serikali na whichever angle we take hakupaswa kuzungumza yeye.
Case shut! Hii siku 7 ni circus tu!
 
"Kwa kawaida Mungu ana nguvu kubwa na za pekee sana, hivyo katika mazingira ya sasa, nguvu hizo zinaweza kumfanya mhusika kujitaja mwenyewe," alisema.

"Kitu nisichokielewa ni majukumu ya Waziri Masha katika suala hili, alikuwa akitoa tamko hilo kama Msemaji Mkuu wa Wizara au Serikali, alikuwa akizungumza kama nani, nauliza hivyo kwani sijui taratibu za Serikali kama yeye ni msemaji wa sehemu hizo.

"Nilizungumzia Waziri kijana wa wizara nyeti, mawaziri vijana wako wengi, yuko Ngeleja (William, 41), Kamala (Deodorus, 40) na yeye Masha (38) hivyo umri wao unashabihiana, sijui atakuwa amezungumza kwa niaba ya vijana wengine ama vipi?," alisisitiza Bw. Mengi.

Kama nilivyosema nina uhakika Mengi hatotaja jina la huyo waziri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom