Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,175
- 143,968
Hivi watu walioenda JKT huwa wanaweka hiyo kwenye resume zao?
Halafu kwa nini hii administration ya Kikwete ina watu ambao academic qualifications zao ziko questionable? Sikuwahi hata siku moja kusikia watu waki question qualifications za Dr. Pius Ng'wandu au Prof. Kigoma Malima na wengine ktk administration zilizopita. Why this one?
Mtanzania said:JokaKuu,
Hapo juu hauko sahihi. Fuatilia data za watu ambao walikuwa wanajisomesha au wanasomeshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, nao ilikuwa lazima waonyeshe vyeti vya JKT.
Kuna watu walisoma international schools toka utoto wao na bado walienda JKT.
Mtanzania,
..requirement ilikuwa ni kwa udhamini wa serikali kwa ajili ya higher learning. hiyo ilikuwa inahesabiwa kuanzia high school.
..ukimaliza form 4 halafu uka-attend high school ya serikali basi ulipaswa kujiunga na JKT. pia kama huku-attend high school ya serikali lakini unahitaji udhamini wa serikali chuo kikuu basi ulilazimika kutumikia JKT.
..huo ndiyo uelewa wangu wa sheria ile. vinginevyo mwenye copy ya sheria ya kuanzishwa kwa JKT ailete hapa na kama nimekosea nitaomba radhi.
Mwafrika wa Kike,
..kuna wahindi walikuwa wamesoma kivyao-vyao na wanajidhamini UDSM hawakudaiwa vyeti vya JKT.
..kwa uelewa wangu JKT ilikuwa ni kwa wale waliosomeshwa na serikali baada ya form 4, au waliotaka udhamini wa serikali chuo kikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu.
Ushirombo said:You have missed a lot mkuu, uelewa wako kwenye JKT ni vizuri ungeliacha kuachangia, Kwa kifupi ilikuwa ni lazima kupitia JKT kabla ya kuingia chuo kikuu. Hakuna Justification ya Masha kutoenda huko kwa mujibu wa sheria. Kuna wahindi walikuwa na michongo ya kusoma nje, lakini still walipitia JKT ingawa walikuwa maselule ile mbaya, tulikuwa nao JKT Ruvu, ama unataka kusema Masha alipitia JKT ya voda fasta? Mfumo wetu mbovu kama aliweza penya UD bila gamba la JKT, nakumbuka kwenye form za university kulikwa na kipengere kuonyesha umetumikia JKT
Ushi wa Ushi wa Rombo
Ushirombo,
..huu mtizamo kuhusu sheria ya JKT siyo wangu peke yangu. kuna jamaa nimemuuliza na amenihakikishia kwamba ni suala la UDHAMINI wa serikali.
..hao Wahindi uliokutana nao Ruvu JKT ni kwasababu walikuwa na intentions za kutumia udhamini wa serikali chuo kikuu.
..nadhani ni bora tuletewe sheria hapa ukumbini. kama sheria ikiletwa na ikathibitika nimekosea basi nitaomba radhi.
NB:
..sijasema popote kwamba Masha alipitia JKT. nilichosema ni kwamba kama Masha alikuwa privately sponsored sheria ilikuwa haimbani kutumikia JKT.
BabaDesi said:Mkuu hapo juu, kwa mujibu wa sheria za nchi wakati ule ilikuwa ni lazima kijana yoyote akimaliza kidato cha sita ama chuo apite kwanza JKT kwa mwaka mmoja kabla hajaingia UD ama kuajiriwa. Ilikuwa haina mjadala.
Ushirombo said:JK
Nimepitia JKT na kusoma chuo kikuu nalijua hili bila ubishi. Pia Mkuu tuangalie sheria ya kuanzishwa kwa JKT...Kuna wenzetu kwa bahati mbaya walijikuta wamepata zero kidato cha sita maana hapo walipoteza sifa za kuingia Uni, lakini JKT hawakuacha mkuu...JKT na udhamini wa serikali hakuna uhusiano mkuu, na waliosoma na Masha hakuwa private sponsored....ni mfumo wetu mbovu kwisha si kosa la Masha mkuu wangu....
Ushi
BabaDesi,
..sasa Laurian Masha hakumaliza kidato cha sita, au chuo, kama ulivyoelezea hapo juu. amesoma majuu tangu utoto wake mpaka alipojiunga UDSM.
..kulikuwa hakuna mjadala wa wale waliotumia UDHAMINI wa serikali. tena kuna wengine walikuwa wanafuatiliwa mpaka makazini.
Mimi nadhani kuna haja ya (kama ni lazima) kujua kulikuwa na exceptions gani ambazo ziliwa ruhusu wengine kuingia UD bila ya kwenda JKT. Nasema hivi kwa sababu nina mfano halisi wa mtu ambaye aliingia UD miaka ya 70 akiwa ni raia mtakatifu wa Jamhuri ya Muungano na JKT hakuiona.
Mwawado said:Ukweli wa mambo Kisura ni kwamba huyo jamaa yako alipinda utaratibu..Katika miaka hiyo unayoitaja haikuwa rahisi sana kuingia UDSM bila kupitia JKT,Mimi nina mfano wa jamaa zangu watatu ambao Baba zao walikuwa watumishi serikalini kwenye Embassies,lakini vijana wao walipitia JKT walipotaka kujiunga UD..Katika miaka hiyo unayoitaja kwa kweli ilikuwa ni lazima na hakukuwa na ujanja kama wa miaka hii ya 80/90 ambapo watoto wengi wa Vigogo walikuwa wanakwepa Jeshi na mnakutana nao kwenye Makorido ya UD.
Kwa kifupi Tu,Jeshi lilikuwa lazima kabla ya kuingia kwenye Chuo cha Elimu ya Juu Chochote au kupata Ajira serikalini...Hii situation ya Masha kutokwenda jeshini ina walakini.
Ukweli wa mambo Kisura ni kwamba huyo jamaa yako alipinda utaratibu..Katika miaka hiyo unayoitaja haikuwa rahisi sana kuingia UDSM bila kupitia JKT,Mimi nina mfano wa jamaa zangu watatu ambao Baba zao walikuwa watumishi serikalini kwenye Embassies,lakini vijana wao walipitia JKT walipotaka kujiunga UD..Katika miaka hiyo unayoitaja kwa kweli ilikuwa ni lazima na hakukuwa na ujanja kama wa miaka hii ya 80/90 ambapo watoto wengi wa Vigogo walikuwa wanakwepa Jeshi na mnakutana nao kwenye Makorido ya UD.
Kwa kifupi Tu,Jeshi lilikuwa lazima kabla ya kuingia kwenye Chuo cha Elimu ya Juu Chochote au kupata Ajira serikalini...Hii situation ya Masha kutokwenda jeshini ina walakini.
umbea, majungu, unafiki, uzandiki, ufukunyuku, ukosefu wa mambo ya maana ya kuzungumza na uchimvi ulokithiri kama kawaida ya wabongo!!! Zero kabisa....
His academic qualifications are not questionable... inamaana georgetown wamempendelea lol.. au UDSM.. kama alipendelewa admission,
Ushirombo,
..huu mtizamo kuhusu sheria ya JKT siyo wangu peke yangu. kuna jamaa nimemuuliza na amenihakikishia kwamba ni suala la UDHAMINI wa serikali.
..hao Wahindi uliokutana nao Ruvu JKT ni kwasababu walikuwa na intentions za kutumia udhamini wa serikali chuo kikuu.
..nadhani ni bora tuletewe sheria hapa ukumbini. kama sheria ikiletwa na ikathibitika nimekosea basi nitaomba radhi.
NB:
..sijasema popote kwamba Masha alipitia JKT. nilichosema ni kwamba kama Masha alikuwa privately sponsored sheria ilikuwa haimbani kutumikia JKT.
. FMES na Viongozi;
Inaelekea uko karibu na Mh. Masha kiasi cha kumpeleka katika Mtihani na Kuchukua Majibu. Napenda utusaidie kupata facts zifuatazo ambazo ziliulizwa hapa ikiwezekana tunaomba utuulizie:
Je, Masha alipitia JKT?
Je Masha alibadili uraia na kupata wa Marekani au ni Raia wa Tanzania? Nimesoma mahali kwamba alisoma shule huko Marekani ambazo raia wa kule ndo wanayo nafasi ya kulipiwa. Kuhani, nisaidie hapa juu ya Education System V/s Uraia.
Inawezekana Masha alipata mafanikio ya kibiashara mapema katika Law Firm yake na partners. Unavyomfahamu wewe, je ni Mzalendo? Ana uChungu na Nchi yake? Ni mkereketwa wa Maendeleo?
Mwisho napenda kujua kabla ya kuwa Mwanasiasa kama ana record yoyote ya kusaidia vyama vya kijamii au hata wenye shida.
Majibu ya maswali haya yatatusaidia kutoa mwelekeo pia ni viongozi wa namna gani wanafaa kuwa mawaziri badala ya kuchaguliwa tu na rais bila vigezo maalumu.