Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 969
- 1,939
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, amewashutumu vikali viongozi wa vyama vya upinzani kwa kuendesha siasa za vurugu na kutumiwa na mataifa ya nje kuharibu amani ya nchi.
Akizungumza, Mei 18, 2026, kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Ismani, Emmanuela Mtatifikolo, huko Migoli mkoani Iringa, Chatanda amesema upinzani unachezea wema na upole wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Chatanda amerejea matukio yaliyojiri katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akieleza kuwa maeneo yaliyokumbwa na ghasia "hayana hamu" kutokana na mipango ya watu wachache waliotaka kuiharibu Tanzania.