Meli ya MV Skagit yazama

Meli ya MV Skagit yazama

Jamani chanzo ni nini?

Chazo ni conspiracy theory inayoendelea. Ilipozama MV Spice JWTZ hatukuwaona kushiriki ktk uokozi. Meli ya leo imezama sio chumbe bali ilikuwa karibu zaidi na bara kuliko Zanzibar na meli zote za uokozi zimetokea Zanzibar. Meli zote hizo huanzia safari zake kutoka Dar. Inna lilahi wa inna ilaihi rajuun.
 
Nashindwa ku-connect haya matukio ya kupoteza roho nyingi kwa wakati mmoja katika kipindi fulani. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi tukio la kuzama kwa MV Islanders lilitokea wakati wa heka heka za kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani. Hili la MV SeaGull limetokea wakati wa heka heka za kuanza mfungo wa Ramadhani!

Wakati tukiwapa pole wote waliopoteza ndugu, jamaa, na marafiki katika matukio haya ya "ajabu"; wenye macho ya rohoni kuna kitu cha kujifunza hapa. Huenda adui ameanza kazi zake waziwazi bila kificho sasa - TULIOMBEE TAIFA LETU. Hakika haitatanguka yodi wala nukta moja ya Torati hata yote yatimie. AMEN.
 
inasemekana MV seagul ikitokea Dar kuelekea zanzibar imezama. kila tupato habari tutazidi kuhabarishana

Update:
Ilikua na abiria 200 na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vipo. Meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu mara kadhaa.
View attachment 59156
Ni conspiracy theory inayoendelea. Ilipozama MV Spice JWTZ hawakushiriki ktkt uokozi. Leo meli ilkuwa karibu zaidi na Bara kuliko Zanzibar na hakuna meli hata moja kutoka bara iliyoshiriki uokozi
 
Sasa hapa inabidi tuulizane maana naambiwa pale kivukoni kuna kituo cha kuelekeza meli na hali ya hewa. Je, kituo hiki kilitoa kibali kwa meli hiyo isafiri hata kama hali ya hewa ilikuwa mbaya kiasi hicho?..

MV Kilimanjaro ilipit route hiyo hiyo, na hali ya hewa hiyo hiyo bila shida. Meli yenyewe ni moja kati ya hizi hapa (ambazo kulikua na serious concern over their safety standards): https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/111661-washington-state-sells-2-passenger-ferries-to-tanzania.html



 
Hivi mbona Kenya wana kiherehere na mambo ya Tanzania?

Mkuu hicho sio kiherehere, hili ni janga kwa taifa na ni muhimu taarifa zikarushwa duniani kote ili wenye uwezo wa kuokoa waathirika watoe huo msaada. Huwezi kuficha mkaa wa moto kwenye nguo- lazima tu utaungua.

Fikiria, kama wewe au nduguzo ndo mngekuwa kwenye hili tatizo hupendi lirushwe?? Punguza ubinafsi mkuu, hata kama ni siasa hii ya kwako imezidi.
 
Kuna Ji meli hapa nyang'anyang'anya Linaitwa Capt. Johns limepaki toka 1989 Habourfront wamelifanya Hotel ya Seafood chafuu unaweza kutapika hata kabla kujala chakula. Sasa hivi wameambiwa ifungwe, Meli inauzwa.. pengine niliweke nami ebay naweza pata wateja Tanzania...
 
Back
Top Bottom