usiwaamini hao clouds ...ilipozama ile ya nungwi ile walitoa takwimu za uongo sana
Hamjaiona maiti ya mwigulu mpaka sasa jamani 2nasubiri kwa hamu kuiona
Juzi kuamkia jana kuna meli ilizima Nungwi nafikiria ni hiyo Seagul hii ya leo ni nyingine. Nakumbuka kulikuwa na mpango wa kujenga daraja.
Juzi kuamkia jana kuna meli ilizima Nungwi nafikiria ni hiyo Seagul hii ya leo ni nyingine. Nakumbuka kulikuwa na mpango wa kujenga daraja.
MV Kilimanjaro ilipit route hiyo hiyo, na hali ya hewa hiyo hiyo bila shida. Meli yenyewe ni moja kati ya hizi hapa (ambazo kulikua na serious concern over their safety standards): https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/111661-washington-state-sells-2-passenger-ferries-to-tanzania.html
]Nimeosoma post #1 ya hiyo link[/B] uliyoiweka hakuna sehemu yoyote ililyosema "(ambazo kulikua na serious concern over their safety standards)".
Nilichoona mimi zilisimamishwa kwa kuwa "They had operated between Seattle and Vashon Island until the state got out of the passenger-ferry business in 2009."
La Hawla Wala Quwata Ila Billahi LaAliyu La Adhyim.
Pole kwa wafiwa na watanzania wote kwa ujumla.Picha ninayopata hapa tangu ajali za meli zilizotangulia(km MV Spice Islander) ni kwamba meli zinazo-operate kati ya Bara na Zanzibar, hazifanyiwi ukaguzi wa kutosha na SUMATRA. Na inapotokea ajali ndio SUMATRA hujitokeza na kuwa wakali lakni kiukweli hakuna ukaguzi, na hii inahatarisha maisha ya watanzania wengi tu.
SUMATRA isilaumiwe katika hili. Zanzibar ina mamlaka yao ambayo inahusika na usafiri wa majini na pia usajiri wa meli. Ilifanya hivyo ili kuwa na mamlaka binafsi kwa Zanzibar na kuepuka kuingiliwa katika masuala ambayo wao wanaona si ya Muungano. Kwa nini basi hatari inapojitokeza suala linabadilishwa na kuwa la Muungano? Mchumia janga hula na wa kwao!
inasemekana MV seagul ikitokea Dar kuelekea zanzibar imezama. kila tupato habari tutazidi kuhabarishana
Update:
Ilikua na abiria 200 na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vipo. Meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu mara kadhaa.
View attachment 59156