Meli ya MV Serengeti yazama upande

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,545
7,745
Meli ya MV Serengeti iliyokuwa imefungwa katika gati ya bandari ya Mwanza Kusini imezama upande mmoja wa nyuma majini usiku wa kuamkia leo Desemba 27, 2024.
images (63).jpeg

Taarifa hiyo imetolewa na Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO)na kueleza kuwa MV Serengeti ilisimama kufanya safari zake mwaka 2016 wakati huo ikihudumu kati ya bandari ya Mwanza na Bukoba.
images (62).jpeg

Aidha meli hiyo ni miongoni mwa zile zinazotarajiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa katika kipindi cha mwaka wa fedha ujao.

TASHICO imesema inashirikiana na timu mbalimbali za wataalamu kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wadau wengine katika juhudi za uokoaji.
 
Back
Top Bottom