Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,876
Ohhh alafu Kloro leo nilikua naangalia DR PHIL kulikua na wadada wawili (watu wazima na watoto kabisa) ila walikua wanamlaumua mama yao kwa yaliyowatokea wakiwa wadogo kwasababu alimpa mwanaume wake kipaumbele badala yao. Huyo mwanaume aliwaMOLEST hao mabinti na walipomwambia mama yao hakujali/hakuwaamini wala hakuhangaika kutafuta ukweli. Mambo mengi tu walikua wanamuuliza iweje ukatuweka sisi watoto wako nyuma na kumjali mwanaume wako bila kujali aliyokua anatufanyia???
Leo hii mama hayupo na mwanaume tena....alibaki analia na kusema sikujua angeweza kufanya hivyo...sikuwahi hata kufikiria.Kabaki na majuto.
Ndo nimekumbuka hii sasa hivi na imenifanya nishawishike zaidi na zaidi zaidi kwamba ni muhimu mzazi akawapa watoto kipaumbele!!!Haijalishi ni baba au mama..
...ubarikiwe sana kwa hili...kwa mie nilojaaliwa kusikia sana vilio vya watu,
nimeshalisikia mara nyingi sana hili, na naijua athari zake kwa huyo mtoto ambaye ndiye
naye anakuwa mzazi wa kesho..-lower self esteem pia inanzia hapa...!-
Well well
Nakiri kwa mara ya kwanza nimelazimika kuukimbia uzi wangu mwenyewe.
Ni ukweli uumao lakini lazima tukubaliane nao. Huu uzi kwa mara ya kwanza ukanipeleka mpaka kwa my dear wife kumuuliza. Nilichojibiwa, khaa!
Sasa nakubaliana na my dear wife, MwanajamiiOne, Lizzy, klorokwini, The Boss,Mbu, MTM, Nyani Ngabu na wengine wote kuwa upendo kwa spouses hauwezi kulinganishwa na upendo kwa watoto. Ni vitu viwili tofauti kabisa
Pia naungana moja kwa moja na Dark City mzee mwenzangu, AshaDii shem langu la ukweli na Nyumba Kubwa kwamba kwa kina mama, akishajifungua basi huwezi toa mapenzi yake kwa kiumbe kilichokaa tumboni mwake kwa miezi takriban tisa. Japo kuna rare cases za kinamama wanaowachukia watoto wao utadhani hawajawazaa wao. Tunayashuhudia mengi.
Nawashukuru wooooooote mliouchangia huu msredi.
Nilichojifunza ni kuwa: Mapenzi ya mama kwa mtoto hayalinganishwi na kitu chochote. Wanaume ili tupendwe zaidi na wake zetu yatupasa kwanza tuwapende watoto wao/wetu.
Kumbe ni rahisi sana kwa wazazi: Pendeni watoto wenu ili mpate sababu ya kuendelea kupendana zaidi na zaidi!!
Baada ya kusema hayo naomba kuwashukuru kwa michango yenu. Nimegradueti!
dahhh, ulikuwa wapi siku zote?
umeamua na kuhitimisha kabisa thread asubuhi asubuhi?
mkuu, ubarikiwe sana kwa topik hii....