Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

Wewe na Msigwa akili zenu hazina tofauti!

Unaandikiwa barua na mwanasheria, unawajibu wamachinga!!!
ndio akili za ovyo,upewe barua na mwingine,umjibu mwingine kwa maneno,inabidi watu kama hawa warudi shule wakasome upya
 
Hii kesi itawapa umaarufu zaidi cdm kwakuwa ushaidi tunao tutawapa cdm,

tunakerwa na vitendo hivi vya ujangili, vinavyofanywa na makada wa ccm wkishirikiana na kinana,

na amini usiamini hii kesi akipewa "tundu" utakuwa mtihani wake wa mwisho, tunafikiria kumpa uwaziri wa sheria, state attoney au ujaji mkuu katika serikali ijayo
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Nenda mahakamani hima
 
Alichofanya msigwa ni sawa kabisa, kwani mwanasiasa anaongea na wapiga kura wake mambo yanayomhusu kama mwanasiasa, mbona rais anahutubia taifa mara kibao kwa kuongea na wazee wa Dar es Salaam? Hapa wakili wa kinana akafungue kesi mahakamu kuu ngoma ianze. Manake CHADEMA wanajua wanachosema na wanasema wakimaanisha. Tunasubiri kuambiwa kesi namba ngapi ya mwaka 2013, May.
 
Hizi ni akili ya level ya bavicha na Msigwa.

Mnashindwa kuelewa kuwa swala sio kuwadharau wamachinga, ila huwezi kuandikiwa barua na mwanasheria halafu unaenda kuwajibu wamachinga au unaandikiwa barua na wamachinga halafu unaenda kumjibu mwanasheria.

Hizi ni cheap politics. Msigwa anatafuta sympathy.

Wamachinga hao wanahusika nini na UDAKU aliouzusha? Wamachinga wana kero zao, hizo ndio wanataka kusikia zikijadiliwa.

Kesi binafsi ya Msigwa haina uhusiano na biashara za wanachinga.

Ndio maana ya uwakilishi, wakili wa Kinana anapomwandikia mwakilishi wa Tanzania wote (except wewe na Maccm) ni sawa na kutaka kupambana na watanzania maana wale tembo ni inheritance ya watanzania na wanaoumia kwa wizi unaofanyika ni watanzania.

Sasa si watanzania wote ambao tutaongea tukilalamika kuhusu wizi anaoufanya mwenzetu, tunae muwakilishi wetu mchungaji Msigwa ambaye kila step ya jambo hili anapaswa kuja kutupa updates.

Kwa kuongea na wamachinga wa Iringa ujumbe umefika kwa watanzania wote wanaoipenda nchi yao, again, except wewe na maccm menzako.
 
Siku zote fisadi hujaribu kujisafisha kupitia mahakama na kwa kuwa ana tembodollar anadhani anaweza nunua hata haki.bravo Msigwa ile ndiyo sehemu sahihi na ya mkato kwa majibu ya Kinana.:nod:
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Unataka kutuambia hao Kinana aliowapa Tenda ya Kutoa Taarifa Ndo Walimpa Ukatibu Mkuu wa CCM ama ndo wamempa Kibali cha Kuua Tembo wetu????
 
Kinana hajawasiliana na Msigwa. Aliyewasiliana na Msigwa ni mwanasheria wa Kinana.

Msigwa ni mgeni kwenye game, anadhani kila kitu ni siasa.

Vuteni subira muone kitakachotokea...

Naona unaongea kama PASCO kwenye ile Bonafide Genuine.
 
Wewe na Msigwa akili zenu hazina tofauti!

Unaandikiwa barua na mwanasheria, unawajibu wamachinga!!!

Sasa unashangaa nini? Rais Jakaya Kikwete aliongea na wazee wa Dar es Salaam na kuwajibu wafanyakazi waliotaka kugoma na kumshambulia sana Bwn. Mgaya. Afadhali ya Mhe. Msigwa aliyasema hayo akiongea na wapiga kura wake. Hata hivyo unajitahidi sana kuchangia ukiponda kila kitu cha upande wa upinzani.
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

We ndio mpuuzi kweli huyo kinana alitakiwa amuandikie MSIGWA hiyo barua shuruti ampatie kutoa kwenye gazeti ni alternative means iwapo MSIGWA angekuwa hapatikana na sababu MSIGWA hana mpango wa kufanya hayo ambayo KINANA amemtaka ayafanye hukuwa na haja ya kujibu barua hiyo formal kama unavyosema kwanza kaisoma kwenye vyombo vya habari......Hivi NAPE anapokuwa anawa recruit uwa mnafanyiwa INTERVIEW KWELI sasa mbona uelewa wenu mdogo sana any way ata BOSS wenu ni ZERO kabisa nimewasamehe.
 
kinana hana jipya yeye kama anaona msingwa ni muongo aende mahakamani ili aone madudu yake yatakavyo anikwa
 
Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Atakuwa nazo ila ni kidogo ndio maana anaweza kuanzisha mjadala na wafanya biashara wakubwa.
Ishu ya kutoa Tamko kwa viongozi wetu huwa haijalishi, Nishaona na kusikia mara kadhaa viongozi wetu wanakuja katika misiba halafu wanatoa maagizo ya kiserikali na yanachukuliwa na watendaji.
 
Eee, uelewa wako ni questionable, pale ilipofikia lazima kila mhusika afuate formality Kinana kupitia kwa mwanasheria ametoa demand notice, wewe unasema

Nakuuliza, magazeti ni public au sio public? Eric Ng'maryo, Mwanasheria wa Kinana, aliitisha press conference kisha "matangazo" ya kuombwa radhi yakatolewa magazetini (whole page). Mimi na wewe nani uelewa wake ni questinable?
 
Wewe na Msigwa akili zenu hazina tofauti!

Unaandikiwa barua na mwanasheria, unawajibu wamachinga!!!

Nafikiri ndugu yangu ZeMarcopolo unakosea sana. Kama barua imeandikwa na mwanasheria wa Kinana na addressee ni Pastor Hon. Msigwa then kwa nini iende kuchapishwa magezitini kooooooote kama kweli iliandikwa in a very polite and communicative manner kama unavyoonesha hapa.

Ndugu yangu km hujadhamiria kupotosha basi ni bora uone kuwa Kinana alikuwa na lengo la kujisafisha kwanza and then amtake Hon Pastor amsafishe mara ya pili ili "atakate" kabisa.

Hakuna objectivity kwenye barua ya Kinana. Otherwise, ingeandikwa na kupelekwa Bungeni Dodoma kwa Mchungaji aipate ili ajue kusudio lake. Sasa kuchapisha magazetini tena kwa kulipia page nzima (kumbuka ni pesa nyingi) inalenga nini?

Fikiri tena, fikiri saaaana!!!
 
Iringa. Siku mbili baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kumtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kufuta kashfa dhidi yake, mbunge huyo ameibuka na kusema kamwe hatafuta kauli hiyo aliwahi kuitoa bungeni na katika mikutano ya hadhara.

Alisema ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma dhidi ya mtendaji huyo mkuu wa CCM.

Mchungaji Msigwa aliwahakikishia wapigakura wake kuwa hana hofu juu ya msimamo huo na kwamba yuko makini kwa kila anachokifanya.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mashine tatu katika Manispaa ya Iringa juzi, mbunge huyo alisisitiza kuwa tuhuma hizo ni za kweli.

Alisema tuhuma hizo alikuwa amezitoa bungeni lakini pia katika mikutano mbalimbali ya hadhara na kwamba ana ushahidi nao.

Alisema siku 21 zilizotolewa na Kinana kupitia kwa wakili wake Erick Ng’maryo kumtaka afute kauli hizo, ni chache na kwamba yeye yupo tayari kwenda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

“Nilipotoa hotuba yangu bungeni nilimtuhumu Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa anahusika na matukio ya ujangili ya uwindaji wa wanyamapori wakiwemo tembo hapa nchini. Sasa katibu huyo amenipa siku 21 nifute kauli yangu na nimwombe radhi, mimi ninasema siombi radhi nasubiri wito kwa kwenda mahakamani,”alisema Msigwa.

“Kinachonisikitisha zaidi wametoa taarifa hiyo kama maelezo makubwa ya kujisafisha kwenye gazeti huku mimi wala ofisi yangu ikiwa haijapatiwa barua yoyote,”alisema.Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajapata barua rasmi kutoka kwa wakili wa Kinana kumtaka aufite tuhuma hizo.

Source: Gazeti la Mwananchi
 

MCHUNGAJI MSIGWA (MB) AMTAKA MHE. KINANA AWAHI KORTINI

685036564.JPG
Mch. Msigwa (picha: Francis Godwin/MATUKIO DAIMA)​
Na Francis Godwin, via blog, Iringa--

Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amememtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw Abdulrahman Kinana kutokusubiri muda wa siku 21 alizozitoa Wakili wake kumfikisha mahakamani.

Mch. Msigwa amesema kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kamwe hata kuwa tayari kumwogopa mtu na siku zote atasimama katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.

Msigwa amesema hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa.


Akasema suala la Kinana kwenda Mahakamani ni sawa na kumtishia nyau mtu mzima.

Msigwa ameseme CHADEMA ina mawakili waliojitosheleza na hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho.

Msigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) mjini Iringa katika stendi ya mabasi ya Mikoani, akiwataka wafanya biashara hao kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine Tatu bila kufanya vurugu zozote. Amesema suala lao la kunyanyasika ameshaanza kulipigania bungeni kwa Waziri mwenye dhamana, hivyo machinga wa Iringa wasikubali kamwe, kunyanyas.



Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Samahani Mkuu, hapo nilpokoleza wekundu ulikuwa umepasoma au haraka ya kujibu imekufanya usipaone ?
 
kinana hana jpya sio saizi ya Msigwa bora angekaa kimya. fisadi
 
Back
Top Bottom