Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

Mawazo yako ni kama ya Msigwa. Haya ni mawazo ya ki-BAVICHA BAVICHA. Tunaposema OFFICIAL CHANNEL ina maana yake. Hili neno hatujaliweka hapa kimakosa au kutokujua.

Barua imetoa siku 21, kwa hiyo kwa mawazo yako haya unadhani barua ni pambo la ofisi kwenye mafaili.

Kweli BAVICHA ni janga la Taifa.

Kamuulize nkangaa na kesi ya Lema arusha, naye alifuata proper official chanel, tunaangali authetisity of the object related to subject,
kinana ataaibika soon, likewise ccm.
 
Mawazo yako ni kama ya Msigwa. Haya ni mawazo ya ki-BAVICHA BAVICHA. Tunaposema OFFICIAL CHANNEL ina maana yake. Hili neno hatujaliweka hapa kimakosa au kutokujua.

Barua imetoa siku 21, kwa hiyo kwa mawazo yako haya unadhani barua ni pambo la ofisi kwenye mafaili.

Kweli BAVICHA ni janga la Taifa.

mkuu hawa watu watakupa shida uelewa wao tatizo.
 
mkuu tumwamini nani wewe, msigwa ama mwandishi? kwenye thread imeandikwa na inamnukuu mch.Msigwa

"Msigwa amesema hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa"

hapa inaonekana kabisa kuwa Mch.Msigwa bado hajapata wito/taarifa isipokuwa Kinana amekimbilia kwenye vyombo vya habari...nani mkweli? wewe, msigwa au source?

Kinana hajawasiliana na Msigwa. Aliyewasiliana na Msigwa ni mwanasheria wa Kinana.

Msigwa ni mgeni kwenye game, anadhani kila kitu ni siasa.

Vuteni subira muone kitakachotokea...
 

MCHUNGAJI MSIGWA (MB) AMTAKA MHE. KINANA AWAHI KORTINI

685036564.JPG
Mch. Msigwa (picha: Francis Godwin/MATUKIO DAIMA)​
Na Francis Godwin, via blog, Iringa--

Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amememtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw Abdulrahman Kinana kutokusubiri muda wa siku 21 alizozitoa Wakili wake kumfikisha mahakamani.

Mch. Msigwa amesema kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kamwe hata kuwa tayari kumwogopa mtu na siku zote atasimama katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.

Msigwa amesema hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa.

Akasema suala la Kinana kwenda Mahakamani ni sawa na kumtishia nyau mtu mzima.

Msigwa ameseme CHADEMA ina mawakili waliojitosheleza na hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho.

Msigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) mjini Iringa katika stendi ya mabasi ya Mikoani, akiwataka wafanya biashara hao kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine Tatu bila kufanya vurugu zozote. Amesema suala lao la kunyanyasika ameshaanza kulipigania bungeni kwa Waziri mwenye dhamana, hivyo machinga wa Iringa wasikubali kamwe, kunyanyasika.



this man is a great mind...for great people the tanzanians, na sio hao majangili hawa wanajipa majina --eti ni mwasiasa mweledi-- kumbe ni katibu wa genge la waovu wakuu wanaoogopa hata wakisikia ngedere analia porini wanaweweseka wanatamani kukimbia, wa wakisikia rasilimali za umma wanameza mate ya tamaa ya kuiba hadi mali ya ambao bado hawajazaliwa. ---- Je, sasa Kinana si ametoa tamko? na tishio kali, na kusema kama Msigwa ni jasiri amwombe msamaha la sivyo atampeleka mahakamani na huko atadaiwa mabilioni ya fidia kwa kumharibia? (hapo yeye kinana alishajihakikishia ushindi!), na ole wake sasa asipoenda mahakamani, tunawaomba wanasheria wa CHADEMA wapokee kijiti kama marathoni wawahishe kesi mahakamani ili huyu jangili afumuliwe na genge lote linaloangamiza taifa kwa kuuza rasili mali zetu hadi wanya hai, litatambulika rasmi kwa kupitia kesi hii...! wakati ndio sasa, Mungu atupe nini tena cha kutufunulia?
Mh Msigwa, aluta conti nua na Muumba yuu mbele yako na mbele ya umma wake...pambana baba, thawabu yako kikombee kitajaa pomoni, usiogope!
 
mkuu taratibu za kesi unazifaham mpaka uulize hilo swali.

KWANI HIZO TARATIBU ZA KESI NI SIRI KAMA MIKATABA YA GESI NA MADINI MPAKA NISIZIJUE!!!!
hizo siku 21 ni kutoa nafasi ya utekelezaji wa matakwa ya hiyo barua, mlalamikiwa hana cha kufanya na hizo siku 21, upande wa pili uhitaji tukutane kwa kort haraka zaidi ili kuokoa muda na fedha ikiwezekana
 
Mawazo yako ni kama ya Msigwa. Haya ni mawazo ya ki-BAVICHA BAVICHA. Tunaposema OFFICIAL CHANNEL ina maana yake. Hili neno hatujaliweka hapa kimakosa au kutokujua.

Barua imetoa siku 21, kwa hiyo kwa mawazo yako haya unadhani barua ni pambo la ofisi kwenye mafaili.

Kweli BAVICHA ni janga la Taifa.

Je mlikua na haja gani ya kuita waandishi wa habari na kuwaeleza juu ya hilo swala.Hawezi kuwajibu kwa maandishi kwani hata hizo tuhuma hakuzitoa kwa maandishi. Alizitoa mbele ya jamii kwa hyo hakuna siri hapo.AU kosa alilofanya ni kujibu akiwa Iringa? Au mlitaka aende mwanza pale mbugani aweze kumjibu? Acheni porojo hapa tunataka muwahi mahakaman.
 
mbona msigwa hajapelekewa barua officially, ameisikia sikia juu juu kama ulivyo isoma wewe kwenye gazeti, amesema pale kwenye mkutano leo.
 
Hakuna Chama kilichokuwa na mawakili wakali kama NCCR MAGEUZI,
Lamwai,
Sengodo Mvungi
Mabere Marando, na wengineo wengi lakini kiko wapi sasa.

Chadema hakiwezi kuja kuongoza taifa hili kamwe kwa sababu imejaa makanjanja wengi sana walioko pale kupiga deals tu.

Wangekuwa wengi ungefikisha orodha ya angalau 5, jitofautishe na mtumwa aliyeshibishwa.
 

nifulsa yako sasa kumtazama kamanda msigwa akichangia jana kuhusu machinga
 
Last edited by a moderator:
Wamachinga wa iringa ndo
tumempa msigwa kura sio wewe........ Anawajibika kwetu sisi sio
wewe..... Anatakiwa atujibu sisi na sio wewe.....hata hivo
hongera.....unajitahidi kushiriki thread nyingi...

Mkuu,hao akili zao zipo unyayoni,we m2 ushaambiwa kupitia utafiti wa kisayansi kuwa miaka 10 ijayo hali ikiendelea hv hakutakuwa na tembo halaf jitu kwa maslahi yke binafsi linatetea huku halifikiri kuwa tembo ni among ze big5 watalii hupendelea kuwaona,afanye ecomical impact assesment juu ya janga hlo,hatabisha
 
zemarcopolo hata kama ni ubunge huwezi kuupata kupitia jf,jaribu kuwa kama mwalimu usipotoshe kwa makusudi najua hizo zote ni kelele kusudi nape akuwekee kifua kwa ajili ya ubunge.
 
Wewe na nape akili zenu sawa badala ya kueneza sera za chama mnahangaika na chadema,vipi muulize nape makundi mane ya uraisi yamekwisha?Toezi kwanza BORITI ndani ya ccm muweze kuona KIBANZI.
 
Wamachinga wa iringa ndo tumempa msigwa kura sio wewe........ Anawajibika kwetu sisi sio wewe..... Anatakiwa atujibu sisi na sio wewe.....hata hivo hongera.....unajitahidi kushiriki thread nyingi...

Ili aingize buku saba
 
Mkuu hiyo sentensi yako ya mwisho sasa sijui ulitakaje? Maana nafikiri wewe pia hufanya hivyo kila uvaapo kiatu!

atakuwa anasikiaga huwa wanavaa soksi labda masikini hana miguu ndiyo maana hajui wanaanzia kuvaa soksi ndo kiatu kinafuata,pole yake!
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Mheshimiwa sana, mbona unajiharibia?? sasa kutakua na tofauti gani kati ya wewe na msigwa wakati na wewe umekwenda JF kujibu ndio una tofauti na mtu aliyejibu gulioni??

VIjana mna kujumu la kusimama kwenye hoja na haki na kuacha ushabiki, hasa mkiwa wasomi mliosomeshwa na pesa kiduchu za wadhamini
 
Hii nimeipenda kuita KINANA Lager haaa haaa haaaa
 
Je mlikua na haja gani ya kuita waandishi wa habari na kuwaeleza juu ya hilo swala.Hawezi kuwajibu kwa maandishi kwani hata hizo tuhuma hakuzitoa kwa maandishi. Alizitoa mbele ya jamii kwa hyo hakuna siri hapo.AU kosa alilofanya ni kujibu akiwa Iringa? Au mlitaka aende mwanza pale mbugani aweze kumjibu? Acheni porojo hapa tunataka muwahi mahakaman.
Communication through OFFICIAL CHANNEL siyo lazima mawasiliano yawe niya SIRI. HAwezi kwenda mahakamani mpaka siku alizompa kuwa EXPIRED. Siyo kila jambo linafanyika ki-BAVICHA BAVICHA. Kuna misingi ya mawasiliano inayotambulika kiutaratibu na kisheria.
 
"Mkuu ina maana msigwa anafanya vurugu akitegemea cover ya bure, sasa kama Lisu akisepa inakuwaje hapa?
Tatizo msigwa anadandia gari kwa mbele na hii ni hatarai sana kwa huyu Mchungaji" (Chilisosi, Chris Lukosi )
 
DENTIST - Kinana alikuwa ana beep, cha kushangaza Kamanda Msigwa amempigia anaogopa kupokea.

DENTIST aende mahakamani kwa jeuri ipi aliyo nayo ? Labda mahakama za Somalia land.
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

Kutoa majibu hakuangalii unamhutubia nani...
Kwa hiyo unataka kusema hata Rais hana akili timamu kuzungumzia mgomo wa wafanyakazi kwa wazee wa dar?
 
Back
Top Bottom