Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

"Nadhani lengo la msigwa halikuwa kujibu mapigo Kwa kinana, hata barua yenyewe haikumtaka kujibu mapigo bali kuomba radhi. Alichofanya ni kuendeleza hoja yake juu ya ujangili wa kinana, pengine ni vigumu kwa Wamachinga wa Iringa kupata taarifa za Bungeni(Tatizo laweza kuwa TBC au Tanesco, Au Umasikini)kwa hiyo baadhi yao hawakuwa wanajua kuwa Kinana Ni JANGILI, na hata wale waliokuwa wakijua walipenda, bila shaka, kusikia zaidi. Pamoja na kuwapa moyo juu ya unyanyasaji wanaofanyiwa na serikali ya CCM. na ujumbe mwingine ni kuwa Hataomba Radhi, kwa hiyo Jangili Kinana awahi Mahakamani Mapema bila kupoteza muda, Watu wa shughuri nyingi za kizalendo M4C ndio kwanzaaa, Kinana aende kortini mapema"
 
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?

What a formal way! Nadhani hujaelewa alichosema Mchungaji, Mwanasheria wa Kinana kasema na waandishi wa habari badala ya kumfikishia yeye taarifa kwanza! So ni sawa yeye kusema kwa wamachinga kabla ya kuwajibu wanasheria wa Kinana! Mesege delivered!

 
Kwanza barua yenyewe imeandikwa kiuogauoga tu. (nafikiri walikuwa wanaandika huku wakimuwaza Tundu Lisu) maelezo mengi ya nini - mtu jasiri huandika brief and to the point. Barua ndeefu na mikwala mingi, halafu unatangaza gazetini badala ya kumpa muhusika.
 
Wamachinga wana kero zao, hizo ndio wanataka kusikia zikijadiliwa.

.

Wamekuwa machinga kwasababu ya ufujaji wa raslimali unaofanywa na wanaotajwa kuhusika na ujangili kwahiyo wamachinga ni wadau wakubwa sana wa hii kesi.
 
Hizi ni akili ya level ya bavicha na Msigwa.

Mnashindwa kuelewa kuwa swala sio kuwadharau wamachinga, ila huwezi kuandikiwa barua na mwanasheria halafu unaenda kuwajibu wamachinga au unaandikiwa barua na wamachinga halafu unaenda kumjibu mwanasheria.

Hizi ni cheap politics. Msigwa anatafuta sympathy.

Wamachinga hao wanahusika nini na UDAKU aliouzusha? Wamachinga wana kero zao, hizo ndio wanataka kusikia zikijadiliwa.

Kesi binafsi ya Msigwa haina uhusiano na biashara za wanachinga.

Unatakiwa kuwa insane ili uwe mtetezi wa magamba
 
Watanzania tumekuwa too emotional katika siasa zetu kiasi kwamba inatu influence katika judgement. When one gets too emotional one ends up making choices/ judgments that are shortlived and in most cases not in the public interest. Ya Msigwa na Kinana tuwaachie wenyewe, sie tuliyebaki let's focus on more important issues e.g gas na mengineo. Kwa mtazamo wangu mashabiki wote wanatoa povu si wa chadema wala wa ccm. Hii kesi sioni sie wengine itatusaidia vp.
 
Watanzania tumekuwa too emotional katika siasa zetu kiasi kwamba inatu influence katika judgement. When one gets too emotional one ends up making choices/ judgments that are shortlived and in most cases not in the public interest. Ya Msigwa na Kinana tuwaachie wenyewe, sie tuliyebaki let's focus on more important issues e.g gas na mengineo. Kwa mtazamo wangu mashabiki wote wanatoa povu si wa chadema wala wa ccm. Hii kesi sioni sie wengine itatusaidia vp.

Unalosema ni kweli lakini kwa sababu Kinana mwenyewe na Msigwa mwenyewe wameliweka public, linatuhusu. Wacha tusemee yoteeee yanayohusu ujangili wa maliasili, madini, gas, uzalishaji umeme na yote yale ya kifisadi.
Hii itatupa mwanga na information zaidi. Vita ya panzi furaha ya kunguru.
 
apo penye red, hivi haka ka utaratibu kwani kapo?

Kwani kameisha lini? Nashangaa tu issue za maana kama za kukemea udini wazee hawa hawaitwi.
Subiri wanainji wawe wanadai jambo la masilahi ya inji yao uone, hao wazee wa magamba wataitwa chap chap as if ndio wawakilishi wa watanzania! Shame to magamba!
 
what a formal way! Nadhani hujaelewa alichosema mchungaji, mwanasheria wa kinana kasema na waandishi wa habari badala ya kumfikishia yeye taarifa kwanza! So ni sawa yeye kusema kwa wamachinga kabla ya kuwajibu wanasheria wa kinana! Mesege delivered!


kaka utapata shida sana kumuelimisha ze macopolo jamaa hiwa haelewi hasa baada ya posho
 
Msigwa ‘amtunishia msuli’ Kanali Kinana


Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa

Na Geofrey Nyang’oro MWANANCHI


Posted Ijumaa,Mei17 2013 saa 20:19 PM

Kwa ufupi

•Mchungaji Msigwa aliwahakikishia wapigakura wake kuwa hana hofu juu ya msimamo huo na kwamba yuko makini kwa kila anachokifanya.


Habari kamili,

Iringa. Siku mbili baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kumtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kufuta kashfa dhidi yake, mbunge huyo ameibuka na kusema kamwe hatafuta kauli hiyo aliwahi kuitoa bungeni na katika mikutano ya hadhara.


Alisema ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma dhidi ya mtendaji huyo mkuu wa CCM.


Mchungaji Msigwa aliwahakikishia wapigakura wake kuwa hana hofu juu ya msimamo huo na kwamba yuko makini kwa kila anachokifanya.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mashine tatu katika Manispaa ya Iringa juzi, mbunge huyo alisisitiza kuwa tuhuma hizo ni za kweli.


Alisema tuhuma hizo alikuwa amezitoa bungeni lakini pia katika mikutano mbalimbali ya hadhara na kwamba ana ushahidi nao.


Alisema siku 21 zilizotolewa na Kinana kupitia kwa wakili wake Erick Ng’maryo kumtaka afute kauli hizo, ni chache na kwamba yeye yupo tayari kwenda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.


“Nilipotoa hotuba yangu bungeni nilimtuhumu Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa anahusika na matukio ya ujangili ya uwindaji wa wanyamapori wakiwemo tembo hapa nchini. Sasa katibu huyo amenipa siku 21 nifute kauli yangu na nimwombe radhi, mimi ninasema siombi radhi nasubiri wito kwa kwenda mahakamani,”alisema Msigwa.


“Kinachonisikitisha zaidi wametoa taarifa hiyo kama maelezo makubwa ya kujisafisha kwenye gazeti huku mimi wala ofisi yangu ikiwa haijapatiwa barua yoyote,”alisema.Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajapata barua rasmi kutoka kwa wakili wa Kinana kumtaka aufite tuhuma hizo.
 
Kwao ndio njia pekee ya kuwapumbaza watanzania waamini kuwa amekana na hahusiki. Days are numbered. kuna siku dunia itawaumbua tu
 
Baada ya siku 21 kupita utasikia..."Katibu mkuu wa ccm ameamua kumpuuza na kudharau tuhuma dhidi yake, zilizotolewa na ...!"

Msigwa, kaza uzi, endelea kuwajuza watanzania juu ya genge la ujangili wa wanyamapori wetu.
Tuko nyuma yako.
 
Alikuja juu kuhusu ile biashara yake haramu ya ujangili,amefikia wapi wadau au muda aliompa Msigwa haujafika?
 
haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (mithali 14:34)

ukipewa kazi ya kuhudumia watu lazima ujiheshimu - nyerere

huwezi kutamani kazi ya umma huku unafanyakazi hatari ya ujangili ukidhani hiyo dhambi itakuacha. Dhambi ya ujangili itamfuata mpaka kaburini kwasababu baba, mama na watoto wa tembo wanaomboleza usiku na mchana juu ya msiba uliosababishwa na huyu jangili.
 
kinana.jpgkinana.jpgna hapa bado
 
Back
Top Bottom