Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

hokani

Senior Member
Mar 26, 2013
102
195
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amememtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw Abdulrahman Kinana kutokusubiri muda wa siku 21 alizozitoa Wakili wake kumfikisha mahakamani.

Mch. Msigwa amesema kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kamwe hata kuwa tayari kumwogopa mtu na siku zote atasimama katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.

Msigwa amesema hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa.

Akasema suala la Kinana kwenda Mahakamani ni sawa na kumtishia nyau mtu mzima.

Msigwa ameseme CHADEMA ina mawakili waliojitosheleza na hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho.

Msigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) mjini Iringa katika stendi ya mabasi ya Mikoani, akiwataka wafanya biashara hao kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine Tatu bila kufanya vurugu zozote.

Amesema suala lao la kunyanyasika ameshaanza kulipigania bungeni kwa Waziri mwenye dhamana, hivyo machinga wa Iringa wasikubali kamwe, kunyanyaswa.
 
CORLEON

Member
Jan 17, 2011
42
95
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?
Wamachinga wa iringa ndo tumempa msigwa kura sio wewe........ Anawajibika kwetu sisi sio wewe..... Anatakiwa atujibu sisi na sio wewe.....hata hivo hongera.....unajitahidi kushiriki thread nyingi...
 
Richard Robert

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
593
225
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?
​Msigwa achana na malumbano angalia 2015 inakuja,umefanya nini
Hakuna masharti ya kumjibu mtu. Tena mikutano ya siasa inamfaa sana jangili kama yeye.

Suala la kuogopa uchaguzi na kuwaacha majangili wakiua tembo wetu ni usaliti mkubwa kwa taifa.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
13,584
2,000
Hakuna masharti ya kumjibu mtu. Tena mikutano ya siasa inamfaa sana jangili kama yeye.

Suala la kuogopa uchaguzi na kuwaacha majangili wakiua tembo wetu ni usaliti mkubwa kwa taifa.
Wewe na Msigwa akili zenu hazina tofauti!

Unaandikiwa barua na mwanasheria, unawajibu wamachinga!!!
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,878
2,000
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?
mbunge mtarajiwa unafanya kazi saa ngapi au buku7 per day ndo inaendesha maisha yako
 
mzurimie

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,147
2,000
kwanini mnamsema kama vile ni muongo, acheni waende mahakani.

waruhusu tu mapaparazi kuwepo tusikie yote, sio iwe ile maakama style ya kufukuza mapaparazi kama kawa ya ccm.
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,329
2,000
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?
Kwa ccm machinga ni kama panya...kwa ccm mnaowaona binadamu ni Wachina, wakanada, wamarekani, wafanyabiashara wakubwa na wale mliowabatiza jina la Wawekezaji
 
kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,015
2,000
Umeona tofauti ya Msigwa na kinana. Kinana amempa msigwa taarifa in a very formal way na evidence. Msigwa anaenda kuwajibu wamachinga wa Iringa!

Huyu mtu ana akili timamu kweli?
una point mkuu nimekusoma vizuri....ila kinana ni jangili hata wakina mwigulu waalijua hilo....sasa sijui wewe huwa uma teteaga nini..!
unajua ni ngumu sana kumsingizia uongo mtu mwenye mabavu tana alie shika mpini uku umeshila makali..
 
Top Bottom