Hakika mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,siku ya jana wengi tumesikia audio ya mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima ndugu Josephat Gwajima ikiwa imelenga kujibu mashambulizi dhidi ya mkuu wa mkoa mh Paul makonda,katika sakata linalotuhumu u halali wa elimu aliyonayo mkuu huyu wa mkoa.
Moja ya vitu vilivyotamkwa na kiongozi huyu wa dini ni kuwa anamiliki vyeti vyote vya mh Paul makonda kile alichoPata division zero na hicho chakugushi.
Mchungaji Gwajima kwa kauli hii ya kumiliki cheti cha mtu mwenye division zero inaalalisha uongo maradufu kwani,kuanzia nnchi hii imepata uhuru NECTA haijawahi kutengeneza cheti cha mtu aliyepata sifuri,Ni aibu kwa mtumishi wa Mungu tena mwenye wafuasi wengi kiasi chako kutumia madhabahu kuongea uongo.mh gwajima huenda akawa napoint dhidi ya elimu ya makonda ila ameitamka kwa kukurupuka,mh Gwajima zungumza kwa kutulia,bado tutatega sikio kukusikiliza na wala hatutakupuza..