Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mjadala umefungwa rasmi tunasubiri mamlaka zinazohusika zichukue hatua stahiki......ikifika saa nne na robo(10.15 am) na bado mamlaka hazijachukua hatua mjadala unaendelea.
Mkuu mjadala haufungwi mpaka ang'oke na kupelekwa mahakamani
 
Mpuuzi ni wewe, sijazuia wala kumtetea makonda.
Pointi yangu ni hiii...gwajima kujiingiza katika hili anajichafua zaidi bora hata awasaidie wengine taatifa hizo wazifanyie kazi kuliko yeye ambaye dunia inajua wanaugomvi na makonda.
Pili katika ukristo kisasi hakiruhusiwi, hili la makonda dunia inajua ni mtumishi batili kwani hana sifa.
Zuia povu


Wewe unayetetea uovu ndio unajichafua zaidi.

Kupitia elimu ya Makonda unaona jinsi anavyofanyakazi za kuchafua watu bila uthibitisho,bila stahaa yeye akichafuliwa povu linawatoka.
 
Hahah tutatumbua walimu na wafanyakazi wengine wa serikali tu wakuu wa mikoa hawawezi kutumbuliwa
 
Sijui upumbavu ni tusi,?! Am sorry nimejikuta limenitoka tu juu yako.! Hivi unajua kulikuwa na walimu ambao hata darasani hawajaenda, Ila wanakula mshahara wa gvt kwa jina la mtu? Leo mnataka kufananisha na mtu aliyesoma kwa jina la mtu mwingine, sio kupata kazi.! Je paul hajasoma? Hajapata elimu? Kama amesoma tuhuma zenu ni nini?
Waliofukuzwa kazi wakati wa uhakiki hawakusoma? Wapo waliosoma kwa majina ya wengine na kufaulu vizuri na kufanya kazi kwa bidii...fagio la uhakiki wa vyeti likawafagia hivyo hili hili fagio lisichague nani wa kufagia nani asifagiwe......wote wafagiliwe bila upendeleo!
 
Kuna mtu anajiita Askofu,anaongopea watu kupitia madhabahu kuwa "ana vyeti vya kutoka NECTA" vyenye daraja sifuri.Kama kuna mwenye taarifa hizi,ni lini NECTA wameanza kutoa vyeti kwa wanaopata daraja sifuri? au yupo kwenye arosto?
Huenda kamaanisha ana cheti cha leaving na verified list ya matokeo ya huyo BASHITE...... so kwa kutumia normal IQ alichokifanya Gwajima ni kucross check tu registration number iliopo kwenye CHETI cha leaving afu akaconfirm kwenye list kuwa huyo Bwana bashite ana zero........ ssa kwa kuwa keshatoa siku tusubiri kila kitu kitakuwa wazi
 
Mbona mambo ya vyeti yalianzia kwakina mwiguru na mtoto wa rais Leo kimya, siasa za vyeti muachane nazo mumefeli ndugu, kama kuna ukweli katika hili peleka mahakamani, nawakumbusha tu!
 
makonda, ni kijana alietoka familia duni, pengine kufeli kulitokana na maisha duni ya kijijini ambako huduma nyingi muhimu hakuna, pengine angetokea familia zenye uwezo wa kati angefaulu vizuri sana. hakukata tamaa na amejitahidi kufika alipofika, ametimiza ndoto ya kuwatumikia wananchi, tena kwa kiwango kikubwa cha kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaa ambako ndiko ukuu wa nchi na uchumi upo. amejitahidi kufanya aliyoamini yanaisaidia nchi na mkoa wake. ki msingi amejaribu kufanya mengi mazuri japo hatujaweka kipima chake cha mafanikio. hongera kwa nia yake njema. ila pia kama binadamu tulivyo hatujakamilika, sisi sio malaika!! hapo sasa...! pengine alitaka hata kwa kutumia vyeti vya mtu mwingine aende mbele zaidi ili aje kuisaidia nchi yake.kwa sasa si vibaya kuachia wengine nao sasa waendelee na pale alipoanzisha
 
Pitieni hapa muone huyu mdada anavyomharibia Mheshimiwa Mkuu wetu wa Mkoa. Haka ka mdada inabidi karejeshwe nchini kuja kujibu tuhuma mbalimbali za kuwachafua viongozi wetu na nchi kwa ujumla. Trump rudisha kwao huyu dada.

 
Well done Makonda

Historia yako imekaa vizuri

You are a fighter

Umetoka familia ya kimasikini lakini kwa sasa Mungu amekufikisha hapo Ulipo...Sio jambo dogo kabisa

Na Mungu atazidi kukubariki
 
Mchungaji Dr.Josephat Gwajima, leo kanisani kwake mbele ya umati wa waumini akiwaita wanafamilia wake, ametoa maelezo yakinifu juu ya tuhuma zinazomkabili ndg. Paul Makonda na katika clip inayosambaa kwa kasi mitandaoni.

Askofu Gwajima amedai anaoushahidi wa kutosha kua ndg. Makonda alitumia vyeti visivyo vyake.

Katika clip hiyo mchungaji Gwajima amesema ana vyeti vinavyotoa ushahidi kua Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine.

Swali: Je, Rais atamwacha Makonda na kulifumbia macho hilo suala?



=======

PAUL MAKONDA:

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.

Khaaaaaaaa hyo namba 14 😀😀😀😀
 
Comnent [HASHTAG]#246[/HASHTAG] ameelezea vizuri sana
 
Mkuu endelea jinsi fitina ilivyotumika hadi kufika hapo alipo. Ujumbe wa bunge maalum la katiba, kampeni 2015, ukuu wa wilaya na sasa ukuu wa mkoa.
Hii imekaa sawa.
 
Back
Top Bottom