Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mpuuzi ni wewe, sijazuia wala kumtetea makonda.
Pointi yangu ni hiii...gwajima kujiingiza katika hili anajichafua zaidi bora hata awasaidie wengine taatifa hizo wazifanyie kazi kuliko yeye ambaye dunia inajua wanaugomvi na makonda.
Pili katika ukristo kisasi hakiruhusiwi, hili la makonda dunia inajua ni mtumishi batili kwani hana sifa.
Zuia povu
Mwenzio akimwaga mboga we mwaga ugali
 
Kama ni kweli itakuwa imetia doa sana team ya vetting na usalama wa taifa kwa ujumla. This is very sad!!!
 
Kwanza kwenye kamusi yangu hakuna Neno MUNGU WA DSM hiyo tu yatosha kujua uwingi wa ujuha na ushabiki maandazi uliojazwa katika Bongo zenu..! Don't argue with a fool.! Rais huamua mtu wa kumteua au kumtengua fullstop.
Kwavile nyie ni malaika, hakuna shida ndugu.
Tumeshachanganya na za kwetu kuhusu uhakiki wa vyeti, tumemwachia Mungu wa Mbinguni.
 
Acha uongo miaka gani hiyo walikuwa wanatoa vyeti acheni uongo wa kijinga,Paul kasoma Nyegezi chuo cha uvuvi alitumwa jina la Paul Makonda na mzee wangu kamfundisha mwambieni huyo Gwajima aache wendawazimu
Na ndivyo alivyosema Gwajima. jina bashite limeanza kutumika wakati akisoma chuo cha uvuvi certificate. kurudi nyuma, unapata mtu anayeitwa Daudi Bashite. Yaani jina Paul Makonda lilianza kutumika baada ya kuzungusha form four. na kwa mujibu wa Gwajima, alichukua kwa mtu.
 
Hii habari inauongo mwingi sana Kwanza anasema darasa la saba hakufaulu lakini akasoma Pamba kisha anasema anavyeti vya ziro form4
Pamba alianzia evening classes kipindi kile zinaitwa Taasisi baadaye wanafunzi wa jioni (Taasisi) waliingizwa kwenye mfumo rasmi au ulkuwa hujazaliwa?? Then anachosema cheti ni result sheet ya watahiniwa wa mwaka huo Pamba sekondari...
 
Nashukuru umejijibu mwenyewe kuwa wanadamu tumekatazwa kulipa kisasi kwani Mungu anasema kisasi ni chake, kama uko tayari nikupe maandiko

Hayo maandiko yako ya Kiroho unayotaka kunipa ningeshauri yabadilishe yawe fursa Kwako ili yaweze kukukomboa Kiuchumi na Kifikra na ukishaona umejikamilisha nayo basi ndiyo unipe na Mimi. Hizi dini ziwafanyeni mjue kufikiri na siyo kuwa wa hovyo hovyo kwani hata mwenye dini yake / neno lake Yesu Kristo wa Nazareth hakuwa wa hovyo hovyo Kichwani kama tunaojifanya kukariri maandiko.
 
Gwajima ndio Nani mpaka umfanye reference hapa?

Tunahitaji ushahidi wa Matokeo ya zero ya na hayo ya kufoji kwanini mzunguke sana Mara sijui Nina namba ya aliempa Vyeti Mara Nina address ya alipokaa wakati anasoma hayo yote ya nini?

Weka vyeti vyake vya Zero hadharani Mchezo uishe
Hata wewe inae bisha bado una nafasi ya kudhibitisha haya.weka vyeti vyake tuamini kweli kama ana singiziwa.
 
Hii habari inauongo mwingi sana Kwanza anasema darasa la saba hakufaulu lakini akasoma Pamba kisha anasema anavyeti vya ziro form4
hebu jaribu kufikirisha kichwa basi kaka. uongo uko wapi hapo? kwani ukifeli darasa la saba huwezi kwenda sekondari? pamba sekondari ni shule ya binafsi (private). private school huwa hazichukui waliofeli darasa la saba?
 
Kuhusu suala la vyeti nadhani gwajima alimaanisha result slip .na ilikuwaje apate division one akafanye certificate badala ya kwenda form five?
Au sijaelewa
 
U
Gwajima ndio Nani mpaka umfanye reference hapa?

Tunahitaji ushahidi wa Matokeo ya zero ya na hayo ya kufoji kwanini mzunguke sana Mara sijui Nina namba ya aliempa Vyeti Mara Nina address ya alipokaa wakati anasoma hayo yote ya nini?

Weka vyeti vyake vya Zero hadharani Mchezo uishe
Unataka uthibitisho we subiri, kuwa mvumilivu amesema raisi asipochukua hatua atatoa vyeti hadharani
 
Mziki umefika penyewe hii ndio wanasema ukichimama -Nchale, ukikaa- nchale, ukigeuka Nchale, ukitulia ya Ucho

Hapa namuona Daudi bashite hata jinsi, akinyamaza wanae, na gwajima kasema atatoa vyeti kama itapotezewa.

Akisema amkamate gwajima kwa uchochezi mamaaa ndio kalifumua, hapa patamuuuu

Na wasipomkamata Gwajima kwa clip hii baaasi watatia tick kwenye aliyoeleza.

Daudi pole mdogo wangu, ukiishi nyumba ya vioo usichokoze Majirani.
Tena usichokoze majirani wenye helikopta
 
Acha uongo miaka gani hiyo walikuwa wanatoa vyeti acheni uongo wa kijinga,Paul kasoma Nyegezi chuo cha uvuvi alitumwa jina la Paul Makonda na mzee wangu kamfundisha mwambieni huyo Gwajima aache wendawazimu
labda useme ulimfahamu akiitwa Paul Makonda tangu akiwa std 7. ila historia ya jina Paul Makonda imeanza baada ya kumaliza kidato cha nne. ila akiwa Pamba Secondary, hakuitwa Paul makonda. Msikilize vizuri Gwajima
 
Pamba alianzia evening classes kipindi kile zinaitwa Taasisi baadaye wanafunzi wa jioni (Taasisi) waliingizwa kwenye mfumo rasmi au ulkuwa hujazaliwa?? Then anachosema cheti ni result sheet ya watahiniwa wa mwaka huo Pamba sekondari...
  • Miaka hiyo mnasoma evening class nilishamaliza shule siku nyingi huo ufafanuzi hajautoa yeye kasema kasoma Pamba hiyo ya Taasisi wewe ndo unasema na kuhusu Cheti kasema anacho hajasema ni matokeo ya kwenye gazeti wewe ndo umefanunua sasa sijui hii Script umeandaa wewe umempa gwajima!!
 
Nikurekebishe kidogo unaposema kuwa katika Ukristo Visasi haviruhusiwi unataka kutuaminisha nini? Hivi Vitendo ambavyo Mwenyezi Mungu aliwafanyia Wayahudi pale walipomuudhi na kutomsikiliza hadi akawapiga Kofi la SAFINA ambalo kiuhakika liliwaangamiza sana Wayahudi hii kwako Wewe siyo KISASI cha Mungu kwa Wayahudi? Tunapojitambulisha kuwa sisi ni Wacha Mungu mno tuwe tunahakikisha tunayajua vizuri maudhui yote yaliyopo katika Kitabu tukufu cha Biblia kuliko kukurupuka na mwishowe kuonekana ni wa hovyo hovyo. Ukipitia vizuri Biblia na Vitabu mbalimbali utagundua kuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe ni Master wa Visasi na ukisoma hasa Kitabu cha Exodus ( Kutoka ) utakumbana na mengi mno. Kila la kheri katika kuyatafuta maarifa ya Kiroho Mkuu.
Screenshot_2017-02-27-00-14-04.png
ATTACH=full]474862[/ATTACH]soma warumi 12:19 na kumbukumbu la torati 32:35
 
Attachments

  • Screenshot_2017-02-27-00-09-58.png
    Screenshot_2017-02-27-00-09-58.png
    25 KB · Views: 49
Back
Top Bottom