Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Mkuu Barbarosa,kumpinga mtu au kupinga kitu au kuwa na mawazo tofauti kumbe ni IQ ndogo?
Pole sana kijana,siasa inakuharibu kijana.


Hapana! Kupinga au kukubaliana na jambo ni sawa kabisa ila swala linakuja unachokipinga au unachokikubalia hapo ndipo uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo unapooingia, kwa mfano ni kama vile leo hii Raisi wa nchi asema watoto kike marufuku kwenda Shuleni kwa sababu kazi yao ni kuwa mama na kulea watoto, sasa utaona kwamba watakao kubaliana Raisi kwenye hili na kuanza kubisha wana matatizo ya kuweza kuelewa na kufikiri vizuri kwa kifupi ubongo hauwezi kuprocess information wanazozipata vizuri na kuweza kuoanisha matukio ukilingansha na wale ambao watampinga Raisi, hivyo kupinga au kukubaliana ni sawa lkn inatengemea unapinga nini na kwenye swala hili la sukari anayempinga Raisi ni kwamba uwezo wa Ubongo wake kuprocess information ni mdogo na hakuna kitu mtu unaweza kufanya ni kwamba yuko hivyo inabidi ukubali tu!
 
Ndugu angalia kwanza CV ya huyo mtoto amekuja TZ akiwa na miaka 9 hajui Kiingereza wala Kiswahili, kumbuka hao watoto wa academy wanasoma Kiingeraza tangu cheke chea hivyo ina maana huyu binti ametumia miaka michache tu kuziba hilo pengo na bado ameongoza TZ nzima!

Kama niliyosema sijahitimisha chochote ila nimeuliza maswali kwa maana hili swala linajadiliwa Dunia nzima kwamba watu wa Waasia yaani Wachina, Wajapani, Wakorea, wana IQ kubwa klk binadamu wote hapa Duniani hata Marekani takwimu zinaonyesha kwamba Wamarekani wenye asili ya Asia (Ujapani, Uchina na Korea) ndiyo wanaongoza kwa ufaulu wakifwatiwa na Wazungu na sisi ni wa mwisho, asilimia 60 (60%) ya Wanafunzi walioko graduate schools Marekani kwenye Ivy league kama Princeton, Harvard, Yale, & Co. Uni ni asili ya Asia, wamewashinda Wazungu ambao ndiyo wengi kwa kiasi kikubwa tu!
Tuko Pamoja ndugu yangu lakini nadhani pia na mazingira ya shule ya fedha hayafanani na watoto wetu wa shule za kata, matokeo ya vijana wetu ukilinganisha na mazingira halisi wanayosoma na kuishi havifanani. Tuwapongeze waliofaulu vizuri lakini pia tusiwabeze vijana wetu kwani hali halisi ya shule zetu tunaifahamu.
 
ana haki ya kufaulu, hiyo feza girls sio mchezo, laziam uwe na 'feza' kusoma hapo feza...
 
Kwa wale ambao labda hawafahamu Bell Curve ni nini, hii ilipendekezwa na Wanasayansi wa Kimarekani waliokuwa wanafanya utafiti wa IQ (uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo) kwa watu wa asili tofauti tofauti hasa nchini Marekani ambapo kuna watu wa jamii ya kila aina yaani Wazungu (Ulaya), Weusi(Afrika Kusini mwa Sahara), Waasia (Wachina, Korea, Japan &Co.) , lengo lao lilikuwa ni kutaka kujaribu kuelezea hali ya maisha ya jamii mbalimbali yaani kwa nini jamii fulani ni masikini klk jamii nyingine!

Hawa watafiti walikuja na hitimisho kwamba Wamarekani wenye asili ya kwetu Afrika wana IQ ndogo kulinganisha na Wamarekani wenye asili ya Asia na Ulaya na hii inaelezea kwa nini Wamrekani weusi wako kwenye ngazi ya chini ya Kimaendeleo ukilinganisha na jamii nyingine!
Walienda mbali zaidi na kufanya test IQ Dunia nzima na sisi huku kwetu tulikuwa wa chini kabisa wa kwanza wakiwa watu wa Asia (Japani, Uchina, Korea &Co.) wakifuaitwa na Wazungu wa Ulaya!

Hawa jamaa walipingwa sana kwamba ni wabaguzi, Je hili la Mchina kuwa wa Pili kwenye mtihani wa kidato cha nne TanZania nzima inasema nini?
Amepata B ya Kiswahili, lugha ambayo siyo yake na wala sia ajabu haiongei nyumbani amewapita watoto wengi sana wa Kiswahili,
najua kwamba data hazitoshi kuweza kuhitimisha chochote lkn labda kuna ukweli ndani yake kwamba watu wa Asia wana IQ kubwa klk wote Duniani kwa maana sijawahi kusikia Mwafrika diaspora akiongoza kwa kwenye mitihani huko aliko kama yuko naomba nisahihishwe!


Nikiangali kwa mfano kwa hali ya kawaida Raisi aliyeonyesha uzalendo kama Magufuli alipaswa kuungwa mkono sana lkn bado kuna watu wanaponda kilam jitihada anazofanya badal ya kuungana naye na kumsaidia kutatua mataizo, Je hii haipo kwenye IQ? Yaani uwezo wetu wa kufikiri na kujua ni mihimu na nini siyo muhimu!

Nitatoa mfano Raisi amepiga marufuku uagizwaji wa sukari nje mpaka pale yeye atakapotoa Kibali kwa kujidhihirisha kwamba kweli kuna sababu ya kufanya hivyo kuna watu wamejaza seva ya JF wanampinga Raisi kwamba amekosea, wkt Raisi ameseam lengo ni kukuza viwanda vya ndani ili viweze kuongeza Uzalishaji na kuanjiri Watz wengi zaidi, lkn watu wanapinga, sasa kama siyo tatizo IQ ndogo nini?
Kama kipimo chako cha IQ ya mtu ni kule kukubaliana na kila jambo bila kudadisi au kutoa mawazo na fikra tofauti, basi wewe sio tu una IQ ndogo, bali ni mpumbavu wahedi!!
 
Tuko Pamoja ndugu yangu lakini nadhani pia na mazingira ya shule ya fedha hayafanani na watoto wetu wa shule za kata, matokeo ya vijana wetu ukilinganisha na mazingira halisi wanayosoma na kuishi havifanani. Tuwapongeze waliofaulu vizuri lakini pia tusiwabeze vijana wetu kwani hali halisi ya shule zetu tunaifahamu.


Hivyo uliyosema na ndiyo hoja kubwa ya watu wengi wanaopinga matokeo ya Bell curve wengi wanasema kama wewe kwamba IQ inategemeana zaidi na mazingira na siyo urithi, yaani kinacho mtofautisha mtoto mmoja na mwingine ni mazingira aliyokulia na siyo uwezo wake wa kiakili wa kuzaliwa, binafsi niko kati kati ya hawo watu wawili lkn mwisho wa siku huyo binti bado nampa

RESPECT!
 
Kama kipimo chako cha IQ ya mtu ni kule kukubaliana na kila jambo bila kudadisi au kutoa mawazo na fikra tofauti, basi wewe sio tu una IQ ndogo, bali ni mpumbavu wahedi!!


Tofauti kati ya kuwa IQ ndogo na mpumbavu wahedi ni ipi?
 
100% nakuunga mkono, pia hizo hizo IQ za weusi walio wengi waliandama london eti kupinga yaliyotokea zanzibar na wengine wanadai eti wanaenda fungua kesi ulaya kwa kunyimwa haki zao za uchaguzi wa haki, hizi IQ wazungu wanaendelea kupima na kujiridhisha zaidi kuwa tafiti zao ziko sahihi, tena inawezekana walipendelea maana hizi IQ ziko sub zero kabisa!
Tatizo unalodai kuwepo kwako unaenda kwa watu kutaka wakusaidie kulitatua ilhari wee ni mtu mzima mwenye 'akili' timamu, Hovyo kabisa! Unazira kisha unadai unanyimwa haki, hizi ni akili kweli?
Mleta mada umeumganisha vizuri point zako kuanzia kwa mchina mpaka kwenye uhalisia.
Nilirukia kusoma nikajua point kumbe ni walewale wa LUMUMBA B7FC,nimepoteza MB zangu buuuuure
 
Hivyo uliyosema na ndiyo hoja kubwa ya watu wengi wanaopinga matokeo ya Bell curve wengi wanasema kama wewe kwamba IQ inategemeana zaidi na mazingira na siyo urithi, yaani kinacho mtofautisha mtoto mmoja na mwingine ni mazingira aliyokulia na siyo uwezo wake wa kiakili wa kuzaliwa, binafsi niko kati kati ya hawo watu wawili lkn mwisho wa siku huyo binti bado nampa

RESPECT!
Uko sahihi ndugu na umeleta hoja nzuri ambayo kama taifa ni vyema kuitafakari kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
 
ttzo ume changanyanya mafail swala la IQ na swala la sukari haviendani apo ndio una dhihirisha IQ yako ni ndogo pia
 
Tuacheni utani wachina ni wagumu sana kuelewa huyo mchina ni genius tu kazaliwa hivyo.. Mimi nimesoma na wachina nchi za nje ni vilaza hatari. Wao wataluburuza tu kwenye Hesabu basi ..

Hawatubuluzi kwny hesabu peke yake!
Kuanzia kwny Ujenzi wa Barabara, Madaraja, kuuza mapazia,Maua, kutia mimba watoto watu n.k. Hata kwenye kusafirisha Meno ya tembo wetu pia wanatubuluza
 
Kama hata humu JF Kiswahili tunakikosea kwa 90% tutawezaje kufauli mtihani. Mfano haoni = aoni
 
dawa yake na ss twende China na kupata A ya kichina
 
MTANZANIA MWENYE ASILI YA CHINA????? HII SENTENSI HUWA INANIPA UKAKASI KIDOGO SAWA NA ILE YA MTANZANIA MWENYE ASILI YA INDIA.... MCHINA NI MCHINA TU, MUHINDI NI MUHINDI TU... KUJUA KISWAHILI SI HOJA KWAMBA NDIO APEWE UTZ... KWANZA ANGALIA SHULE ALIYOSOMA NA THE WAY ANAVYO TREATIWA NI TOFAUTI NA YULE MTOTO ANAYEISHI KULE NANYUMBU NA NAMTUMBO NDANINDANI HUKOOO..... LEVO ZA MAISHA NI TOFAUT KABISA YANI
 
Back
Top Bottom