barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Mara Nyingi Sana jina linaweza kuwa sababu ya wewe Kupenya ama Kukwama kwenye maisha. Baada ya matokeo ya Kidato cha Nne siku ya Jana Story kubwa ni Mchina aliye pata nafasi ya Pili kitaifa ambaye ni Mchina.
CongCong Wang ambaye amepata A tisa na B Moja Ya Kiswahili anasema Cong Maana yake ni Clever na Wang Maana yake ni King... So Jina lake lina maana Clever Clever King. Katika Mtihani wa Mock mkoa wa Dar alikuwa wa 2.
Alianza kusoma darasa la pili alipomaliza darasa la saba akaamua kuchagua NECTA badala ya Mfumo wa CAMBRIDGE sababu mfumo wa NECTA ni mgumu zaidi.
Kiswahili ni lugha yake ya 4 kujifunza anasikitika kupata B wakati MOCK alipata A.
Kati ya masomo aliyokuwa anafurahia zaidi ni somo la Historia ambalo mwalimu alikuwa anafundisha vizuri sana kama Movie.
Source: Clouds Media Group