Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

Kwa mada hii ya mchina ulemuongelea humu ndani nadhani ilistahili kumuongelea na yule mnigeria aliyepata GPA ya tano Russia yaan aliwabwaga warusi na wengineo wote waliokuwa wanasoma katika chuo hicho.
Hata hao wanigeria na huyo Daktari wao wameamua kumtangaza LKN najua ,ninafahamu na ninauhakika kuna watanzania,wanigeria,waghana,waafrika kwa ujumla wengi waliosoma urusi na wana GPA 5.
 
Naomba nikusahihishe nina mifano ya waafrika wengi waliongoza ktk nchi za watu tena ngazi ya vyuo vikuu na watanzania wakiwa wamojawapo tena lugha za ufundishaji ni lugha za kizawa kwenye nchi hizo ikiwemo nchi za bara la asia na wapo hata wa shule za awali ,kati, na juu kwa marekani.


Sijapingana na wewe au mchangiaji mwingine yoyote yule ila nakuomba umtaje kwa maana kama ameongoza kinchi kama huyu Mchina kumbukumbu huwa ziko wazi, kumbuka huyu ni wapili siyo kishule, kikanda au sijui kimkoa bali Tanzania nzima hivyo kama yupo TanZania au Mwafrika diaspora unayemfahamu kama ulivyosema ni rahisi kumtaja hapa!
 
Hii imenifikirisha sana,kwamba waafrika tuna IQ ndogo nahisi kwa lugha nyengine rahisi ktk nchi yetu tulishawahi kuongozwa na rais mwenye IQ ndogo maana kuna siku akiwa ktk kadamnasi kwa hao wazungu alitamka kwamba "hajui kwanini Tanzania ni masikini",really...hakujua kwanini nchi anayoiongoza ni masikini?sijui na mimi niliewaza hivi IQ yangu itakuwa ktk kiwango gani.
 
Aiseee, yawezekana iwe kweli maana haiwezekani mtu awe wa pili kwa kushinda watanzania 430000
 
Asee ebu chunguzeni ayo matokeo vizuri unaweza kukuta ni ya kichina ati
 
Usipokubaliana na amri za Magufuli hata kama Ni za kipuuzi kiasi gani basi una IQ ndogo?
Oh Lord spare us!
 
Inasikitisha mleta maada akiwa anajiita Mtanzania, muafrika mzalendo anakuja na hoja kama hizi. Matatizo makubwa ya baadhi ya waafrika mfano wa huyu mleta mada ni mawili, mosi, kudharau uafrika wake na kutukuza wengine("white supremacy" and black inferiority) na pili ni kuamini mtawala hakosei ( divine rule).
Ripoti ya utafiti wa elimu nchini Uingereza inaonyesha kuwa wanafunzi wengi hufeli masomo ya Kiingereza na hisabati zaidi kuliko masomo mengine.


Ndugu kufeli ni relative, kusema Wanafunzi wa Uingereza wanafeli Kiingereza bila kutoa frame of reference haina maana yoyote ile hoja yako ingeendana na mada yangu kama ungesema kwamba labda Wanafunzi wa Kiingereza wanafeli Kiingereza ikilinganishwa na wanafunzi wageni yaani wahamiaji ambao siyo lugha yao, hapo sasa ndiyo tungeanza kujadili lkn kusema tu wanafunzi wa Kiingereza wanafeli kiingereza inaning'inia hewani bado inakosa nyama, na isitoshe hakuna nilipohitimisha chochote bali nimeuliza swali na wala sijahitimisha kwamba sisi ni inferior haya ni maneno yako na kwanza nimesema Waasia wana IQ kubwa klk wote Duniani yaani kushinda Wazungu na wengineo, sasa huwo white supremacy wako unaoungelea unafiti vipi hapo na nilichokiandika?
 
Huyo ni Mchina by Birth maana kaja Tanzania miaka 9 iliyopita
 
nikinukuu gazeti la mwananchi huyo ni raia wa china na amezaliwa china amekuja tz miaka 9 ilopita kila kitu kajifunza hapa sasa lazima tumpe heshima kubwa na pia tujiulize Wapi watoto wetu wamekwamia ni lugha ngumu au???
 
Ndio hivyo, mchina ndo kaongoza, kuna madogo walisema hata mock aliongoza, hapo zimepigwa tu zile siasa za charity begins at home basi. Ambazo kwa kweli hata kwa mtazamo wangu sio mbaya manake hakuna namna sasa.
 
Theory yako italeta maana zaidi kama ukiweza kuthibitisha kuwa huyu mchina amehamia hapa (miaka michache iliyopita) akiwa hajui kiswahili...Ila kama huyu "mchina" amezaliwa hapa mjini na amelelewa hapa mjini, tofauti yake na watanzania wengine itakuwa ni rangi tu...

nimesikiliza redio leo japo sijajua alikuja lin tz lakin pind anakuja alikua ajui kiswahili wala kingereza na alianza kufundishwa na mwalimu wake shulen lugha hizo kama masomo ya ziada hivyo utajua alikuja akiwa mkubwa kwan inaonekana
 
100% nakuunga mkono, pia hizo hizo IQ za weusi walio wengi waliandama london eti kupinga yaliyotokea zanzibar na wengine wanadai eti wanaenda fungua kesi ulaya kwa kunyimwa haki zao za uchaguzi wa haki, hizi IQ wazungu wanaendelea kupima na kujiridhisha zaidi kuwa tafiti zao ziko sahihi, tena inawezekana walipendelea maana hizi IQ ziko sub zero kabisa!
Tatizo unalodai kuwepo kwako unaenda kwa watu kutaka wakusaidie kulitatua ilhari wee ni mtu mzima mwenye 'akili' timamu, Hovyo kabisa! Unazira kisha unadai unanyimwa haki, hizi ni akili kweli?
Mleta mada umeumganisha vizuri point zako kuanzia kwa mchina mpaka kwenye uhalisia.
Mtoa mada katoa vizuri kabisa, wewe umeharibu kwa sababu unachangia kiitikadi!
 
Nisome vizuri labda utanielewa, najinukuu ukusadia ,,najua kwamba data hazitoshi kuweza kuhitimisha chochote lkn labda kuna ukweli ndani yake kwamba watu wa Asia wana IQ kubwa klk wote Duniani kwa maana sijawahi kusikia Mwafrika diaspora akiongoza kwa kwenye mitihani huko aliko kama yuko naomba nisahihishwe!

Wengine hawapendi kutangaza mambo yao yanaishia huko walipo. Lakini wapo naweza thibitisha.
 
Kikwete aliwahi kusema kuwa ukisoma au ukisikia kitu Usikipokee kama kilivyo changanya pia na akili zako.

Hivi unaamini wazungu wana IQ kubwa kuliko waswahili? Mtu mwenye IQ kubwa anaweza kaa bungeni na kupitisha sheria ya watu kuoana wa jinsia moja na kuipigia debe dunia nzima?

Wazungu wamekubaliana kuwa kuparamiana watu wa jinsia moja ni kitu sahihi.IQ ZAO ZIKO JUU?
Kwa mara ya kwanza YEHODAYA nakupa like kwa kuongea point mkuu na kusimamia ukweli hata kama utakuwa unampinga pro magamba na pro JPM mwenzako.
Hongera,huko ndio ukomavu wa kimawazo na kifikra.
 
Back
Top Bottom