Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Ukichapa kazi Na ukasimamia kazi unaonekana adui. Kaulizeni akina John Ulanga, dr Shayo, dr jabiri kilichowakuta kule TPA
Chezea wewe usichezee chakula Cha wazee
 
Haya kwa mazuri yote tuliyoyaona aliyofanya mchechu pamoja na kufufua hili shirika je ni faida gani wamepata watu wa hali ya chini hasa wanaotegemea makazi haya ya NHC au tunachekelea tuu haya majengo ya vioo yaliosimama huku mjini bila kujua umiliki wake halali na kodi zake?

mkuu hebu tuwe wa kweli! kumbuka nhc ilivyokuwa shirika lilishakufa ofisi zao zilijaa panya, vinyesi, cobdoms tu......mchechu kaja kaitoa toka zerooooo to the top ona miradi nchi nzima anayofanya na team yake, kitu kingine kayapigaaa mkorogo majengo yao yote wakati zamani hao wadosi na wwngine walikuwa wanafanya nyumbaaaa hizo kama zao kawaonhezea kodi pia maana unakuta mtu anauwezo lkn analipaaa 40000 kwa mwezi tena city centre
ukweli unajulikanaaaa na unaonekana mchechu kafanya mageuzi makubwa.....sanaaaaaa, na tukimpaaa nafasi tena atazidi fanya makubwa.....
 
Kweli hizo nyumba ni za wenye nazo na sio watanzania, mfano NHC wamejenga nyumba hapa Arusha eneo la makao mapya apartment yenye vyumba viwili na sebule, choo na jiko ni sh million 80 sasa wanajamvi semeni mtanzania wa kawaida ataweza? Au ndio siasa zenyewe.
 
Msechu ni mchapakazi na kwa ninavyofahamu msimamo wa Profesa Tibaijuka hawezi kumuacha huyu kijana kwa majungu ya kiswahili......wengi tunalalamikia gharama za nyumba mpya za NHC lakini tatizo si NHC bali mabenki yetu na riba za kuruka.......Kwa mfano kuna nyumba nzuri za hadi 68 milion lakini msiba ni riba za benki ambayo ni zaidi 18% p.a na unalipa kwa miaka 20......riba zikishuka chuki kwa NHC zitashuka kwa wasioelewa ........Msechu kafanya kazi kubwa sana kwa shirika lililokuwa limekufa.....
 
Mleta mada, ningeomba nikusahihishe kidogo, mtu ambae una mzungumzia anaitwa Nehemia K Mchechu kwa usahihi, na SIO Msechu kama ambavyo umelitumia jina hilo kwenye habari yako.

Jambo lingine, binafsi nafahamu bodi iliyopo sasa haina muda mrefu tangu ilipovunjwa bodi ya awali na kuundwa hii ya sasa inayoongozwa na Mwenyekiti, mama Zakhia Meghi. Hivyo, sifahamu vizuri mahusiano kati ya wajumbe wapya wa bodi na mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba (NHC) ambae yeye ni katibu mkuu wa bodi hiyo, bwana NKM.

Ila jambo ambalo nina uhakika nalo, ni kwamba mhe rais Kikwete pamoja na katibu mkuu kiongozi, balozi Sefue, pamoja na mama Tibaijuka wanakubali sana utendaji kazi wa shirika kwa sasa. Kwa msingi huu, ni dhahiri kwamba serikali haipo tayari kumuondoa Mchechu kwenye nafasi yake.

Binafsi nilikuwa napinga sana uteuzi wa Mchechu NHC kipindi alipoanza kazi NHC, lakini kwa status ya NHC kwa sasa, huyo kijana ni vyema sana aendelee kuliongoza shirika letu la nyumba, nje ya hapo tutarudi kule kule tulipotoka na shirika letu ambalo Watanzania wengi waliliita "shirika la kusimamia magofu Tanzania".
 
Last edited by a moderator:

kweli kabisa nhc itarudi kule kule kipindi kile ofisi zao ziko kama gesti.....za uswahilini.kingine nchi hii mtu akitaka pigania kufufua makampuni ya serikali basi atapigwa vita balaa....
 
KASI ya utendaji kazi ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Msechu imesababisha aundiwe zengwe kwa lengo la kutaka ang’olewe nafasi hiyo.

Jambo Leo, limeelezwa kuwa, tayari Msechu amepewa masharti mazito na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, yakiwamo ya kumtaka apunguze wakurugenzi wake katika idara mbalimbali.

Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa Msechu alipewa likizo wakati akitafakari masharti aliyopewa na bodi hiyo, inatokana na kumaliza muda wake, kabla ya kuingia naye makubaliano mengine ya kulitumikia shirika hilo, kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na uamifu wa hali ya juu.

Msechu ambaye alilikuta shirika hilo katika hali mahututi na kutumia nafasi yake kupanga safu ambayo imerudisha heshima ya NHC kwa kuendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na bei nafuu kwa ajili ya Watanzania, ameonekana kutofurahisha wale ambao hawapendi shirika hilo lifanye kazi yake kwa maslahi ya taifa.

Vyanzo vya kuaminika vimeliambia Jambo Leo kwa nyakati tofauti kuwa, Msechu kwa sasa amemaliza mkataba wake wa kulitumikia shirika hilo na
kinachosubiriwa ni Serikali kupitia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumuidhinisha tena ili aweze kuendelea.
Hata hivyo, wakati anasubiri kuidhinishwa tena, mizengwe imeendelea kufanywa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

“Kwa sasa kinachoonekana ni kama vile kumuundia zengwe Msechu ili asiendelee katika nafasi hiyo ambayo ameifanya kwa uamunifu mkubwa. Kuna baadhi ya wajumbe wa bodi wanaotaka asirudi na ndiyo wanaochelewesha kumuidhinisha.
“Wameamua kumpa masharti mazito katika kipindi hiki wakitaka atafakari, na moja ya masharti hayo ni kwamba, apunguze idadi ya wakurugenzi wake kwenye
idara, huku pia wakitaka apunguze mishahara ya watumishi wake.

“Yote hiyo ni kutaka kumvunja nguvu ili mikakati yao itimie. Sababu za msingi za kutoa masharti hayo hazipo, bali kinachoonekana utendaji wake wa kazi kwa kiwango cha kutukuka ndiyo unaosababisha wasiopenda mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete, wamchukie na kumtengenezea mazingira ya kumweka kwenye wakati mgumu,” kilisema moja ya chanzo cha taarifa hizo (jina tunalo).

Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake.Pia, Msechu ameshindwa kwenda kwenye maeneombalimbali ya miradi ya NHC inayoendelea sasa, na hiyoyote ilitokana na ukweli kwamba, hajafahamu hatma yake ndani ya shirika hilo.

Wakati hayo yakiendelea, utendaji kazi wa Msechu umekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo yote ni kutokana na kazi nzuri ambayo ameifanya ya kulitumikia taifa na kurudisha hadhi yake ambayo ilipotea. Rais Kikwete mara kadhaa amekuwa akizungumzia mafanikio ya shirika hilo ambayo yameletwa na Msechu kwa kushirikiana na wakuu wake wa idara na watumishi wengine.

Hotuba za Msechu ambazo amekuwa akizitoa katika maeneo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa miradi ya ujenzi, amekuwa akiweka wazi ushirikiano uliopo kati
yake na watumishi wengine, ni sawa na timu ya Real Madrid au Barcelona ambazo zinapokuwa uwanjani zinafanya kazi moja tu, ya kuhakikisha zinafanikiwa
kushinda.

Pamoja na hayo, imefahamika kuwa baadhi ya viongozi na wabunge ambao wamekuwa wakitumia shirika hilo kuweka ndugu, marafiki na jamaa zao wapo kwenye
mkakati wa kuhakikisha Msechu anaondolewa NHC. “Baadhi ya viongozi na wabunge wamesimama kidete kuhakikisha Msechu harudi na hiyo inatokana na ukweli
kwamba, hawakubaliani na misimamo ya mkurugenzi huyo ya kuhakikisha haki inatendeka katika kupata nyumba za shirika hilo,” kilisema chanzo kingine.

Alipotafutwa Profesa Tibaijuka ili kuzungumzia hatma ya Msechu, simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana. Hivyo juhudi za kumtafuta zinaendelea ili
aweze kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo. Pia, Mchecu naye alipotafutwa kuzungumzia taarifa za vyanzo hivyo, simu yake ya mkononi iliita bila
kupokelewa.

Chanzo: JamboLeo

Hivi ni Msechu au Mchechu?
 
Mleta mada, "zengwe" hapo liko wapi?

Dah! mbona bodi ya wakurugenzi kutoa ushauri katika vikao vya bodi ni mambo ya kawaida sana.

Nashangaa mtu unajaribu kila njia kuifanya habari ioneshe kuna "zengwe" wakati halionekani.

Watanzania ni mahodari sana kwa majungu na aliyeandika huu udaku ni mmoja wao.

Mleta mada, "zengwe" hapo liko wapi?
 
Go on Msechu

akisha complete mission yake nhc.....awekwe shirika la ndege atc.... alifufue maana limekufaaaa.kuna vigogo hawataki kuliona shirika hilo lina simama tena
 
Haya kwa mazuri yote tuliyoyaona aliyofanya mchechu pamoja na kufufua hili shirika je ni faida gani wamepata watu wa hali ya chini hasa wanaotegemea makazi haya ya NHC au tunachekelea tuu haya majengo ya vioo yaliosimama huku mjini bila kujua umiliki wake halali na kodi zake?

Quite right!! Je ni watanzania wangapi wa kima cha chini wameweza kununua nyumba zao? Nyumba zinauzwa 50 - 100 mill watanunua wangapi?
 
Pamoja na kasoro kadhaa zilizopo......Huyu Kijana aachwe ...APEWE MKATABA MWINGINE aendelee kuliimarisha shirika.......JK usipotoshwe na mtu yeyote........ muache kijana aendelee kuchapa kazi......
 
Quite right!! Je ni watanzania wangapi wa kima cha chini wameweza kununua nyumba zao? Nyumba zinauzwa 50 - 100 mill watanunua wangapi?
nyie mnataka muuziwe nyumba milion 10 au
 
Kuna shida moja mimi naijuwa, kuna shida ya washikaji wa Dar ambao walisoma na wengi wa top management ya NHC ambao hawaja win maisha na wengine failures ndiyo wanawaonea wivu hawa washikaji. Wakicheki jamaa ni watoto wa mjini, wajanja, wamepiga book, mambo safi na wakicheki shirika nalo linaenda basi hawa jamaa wanaona wivu sana sana.

Big ups

1. Nehemia - DG
2. Felix - DF
3. Raymond - DO
4. James -DHR
5. Cosmas - D M&E
6. David - D BUSS. DEV
7. Isaack -D INNOVATION
 
Haya kwa mazuri yote tuliyoyaona aliyofanya mchechu pamoja na kufufua hili shirika je ni faida gani wamepata watu wa hali ya chini hasa wanaotegemea makazi haya ya NHC au tunachekelea tuu haya majengo ya vioo yaliosimama huku mjini bila kujua umiliki wake halali na kodi zake?

Mtu wa hali ya chini Tanzania hata mlo wa siku Ni kitendawili, Hana assets zozote anamiliki then unataka anufaike na shirika la nyumba. Kwa akili yako ndogo inawezekana unataka shirika lijenge nyumba na kuwapa bure hao watu Wako wa chini, no way hiyo itatokea mahali popote duniani.

Hapa naona kuna zengwe yule Mama wa Kihaya anataka kuweka Mhaya mwenzie baada ya kuona mafanikio. Hata UN aliwavuta Nshomile kibao, but NKM ameweka standards juu Sana lazima watachemka Tu. Kwanza namshangaa kwa CV yake Mchechu kuendelea kufanya kazi chini ya hawa LOOSERS wa CCM
 
Matatizo yake, kama zilivyo raha zake, sisi hayatuhusu.

Kila mtu Ana matatizo yake kwenye dunia hii. Jali ya kwako.

Haki ni kwa Mungu tu.
 
Tatizo si ubaya wa msechuuu tatizo ni kabila lakee nhc kuna kabila flani wamejiingiza kwa wingii humoo mizegwe yotee palee waweke mtu wa kwao nyumbani
 
Back
Top Bottom