kasi ya utendaji kazi ya mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa (nhc), nehemia msechu imesababisha aundiwe zengwe kwa lengo la kutaka ang'olewe nafasi hiyo.
Jambo leo, limeelezwa kuwa, tayari msechu amepewa masharti mazito na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, yakiwamo ya kumtaka apunguze wakurugenzi wake katika idara mbalimbali.nchi hii ukiwa mwadilifu sana huwezi kudumu maana unazuia riziki za vigogo.
Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa msechu alipewa likizo wakati akitafakari masharti aliyopewa na bodi hiyo, inatokana na kumaliza muda wake, kabla ya kuingia naye makubaliano mengine ya kulitumikia shirika hilo, kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na uamifu wa hali ya juu.
Msechu ambaye alilikuta shirika hilo katika hali mahututi na kutumia nafasi yake kupanga safu ambayo imerudisha heshima ya nhc kwa kuendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na bei nafuu kwa ajili ya watanzania, ameonekana kutofurahisha wale ambao hawapendi shirika hilo lifanye kazi yake kwa maslahi ya taifa.
Vyanzo vya kuaminika vimeliambia jambo leo kwa nyakati tofauti kuwa, msechu kwa sasa amemaliza mkataba wake wa kulitumikia shirika hilo na
kinachosubiriwa ni serikali kupitia waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, profesa anna tibaijuka kumuidhinisha tena ili aweze kuendelea.
Hata hivyo, wakati anasubiri kuidhinishwa tena, mizengwe imeendelea kufanywa na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo.
"kwa sasa kinachoonekana ni kama vile kumuundia zengwe msechu ili asiendelee katika nafasi hiyo ambayo ameifanya kwa uamunifu mkubwa. Kuna baadhi ya wajumbe wa bodi wanaotaka asirudi na ndiyo wanaochelewesha kumuidhinisha.
"wameamua kumpa masharti mazito katika kipindi hiki wakitaka atafakari, na moja ya masharti hayo ni kwamba, apunguze idadi ya wakurugenzi wake kwenye
idara, huku pia wakitaka apunguze mishahara ya watumishi wake.
"yote hiyo ni kutaka kumvunja nguvu ili mikakati yao itimie. Sababu za msingi za kutoa masharti hayo hazipo, bali kinachoonekana utendaji wake wa kazi kwa kiwango cha kutukuka ndiyo unaosababisha wasiopenda mafanikio ya rais jakaya kikwete, wamchukie na kumtengenezea mazingira ya kumweka kwenye wakati mgumu," kilisema moja ya chanzo cha taarifa hizo (jina tunalo).
Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya msechu, ndiyo maana hata rais kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake.pia, msechu ameshindwa kwenda kwenye maeneombalimbali ya miradi ya nhc inayoendelea sasa, na hiyoyote ilitokana na ukweli kwamba, hajafahamu hatma yake ndani ya shirika hilo.
Wakati hayo yakiendelea, utendaji kazi wa msechu umekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo yote ni kutokana na kazi nzuri ambayo ameifanya ya kulitumikia taifa na kurudisha hadhi yake ambayo ilipotea. Rais kikwete mara kadhaa amekuwa akizungumzia mafanikio ya shirika hilo ambayo yameletwa na msechu kwa kushirikiana na wakuu wake wa idara na watumishi wengine.
Hotuba za msechu ambazo amekuwa akizitoa katika maeneo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa miradi ya ujenzi, amekuwa akiweka wazi ushirikiano uliopo kati
yake na watumishi wengine, ni sawa na timu ya real madrid au barcelona ambazo zinapokuwa uwanjani zinafanya kazi moja tu, ya kuhakikisha zinafanikiwa
kushinda.
Pamoja na hayo, imefahamika kuwa baadhi ya viongozi na wabunge ambao wamekuwa wakitumia shirika hilo kuweka ndugu, marafiki na jamaa zao wapo kwenye
mkakati wa kuhakikisha msechu anaondolewa nhc. "baadhi ya viongozi na wabunge wamesimama kidete kuhakikisha msechu harudi na hiyo inatokana na ukweli
kwamba, hawakubaliani na misimamo ya mkurugenzi huyo ya kuhakikisha haki inatendeka katika kupata nyumba za shirika hilo," kilisema chanzo kingine.
Alipotafutwa profesa tibaijuka ili kuzungumzia hatma ya msechu, simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana. Hivyo juhudi za kumtafuta zinaendelea ili
aweze kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo. Pia, mchecu naye alipotafutwa kuzungumzia taarifa za vyanzo hivyo, simu yake ya mkononi iliita bila
kupokelewa.
Chanzo: Jamboleo