Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Tamka kimoyo-moyo "Mchechu" mara 5 na usirudie tena huu ujinga wako, na uwaambie hao wenzako wa gazeti lililoandika habari hii wafanye vivyo hivyo.
Nshukuru sana mkuu Pokola, Mwenyezi Mungu kujalie zaidi....
 
Halafu mnasema amejenga majengo mengi, shit!! kwa pesa ipi?? Jibu ni mikopo kutoka banks, hamjaongelea mikopo hiyo iki-mature je kuna pesa ya kufanya -repayment?? Nadhani miaka michache ijayo mtegemee financial crisis kwa NHC kushindwa kulipa mikopo ya bank yaliyofanya consortum na kufinance NHC. Nadhani board wameliona hilo risk wanatafuta namna ya ku-mrestisha.
Nyumba za NHC bei juu haziuziki, then mwisho wa siku watabaki na majumba yasiyouzika moja ya sababu kodi kubwa. Bila kuuza hizo nyumba atalipaje mikopo.Namshauri Mchechu awe mpole asipewe Nkataba ili apate kusepa kabla ya kupigwa pingu kwa kusababisha hasara.
Acheni kubwabwaja bila kufanya utafiti. Mahesabu (Financial Statements) ya NHC ya kila mwaka yako wazi na yanakabiliwa na Waakaguzi nguri. Kama unauwezo ya kuyasoma utaweza kujua kama shirika lina au linaelekea kwenye financial crisis au hapana. Mojawapo ya hoja za ukaguzi ni kama kampuni ni 'going concern' maana yake ni kuwa haiko katika hatari ya kufilisika siku za karibuni. Kukopa kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi siyo jambo baya ilimradi miradi yenyewe iwe inazalisha fedha (cash flow) ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mikopo na vile vile shirika linapata faida. Wajenzi binafsi (private developers) wanauza nyumba kwa bei kubwa zaidi ya NHC na zinanunuliwa. Za NHC ni bei nafuu in comparison. Kwa hiyo financial crisis unayoitabiri ni ndoto zako tu. Mfumo wa zamani wa NHC ambapo walikuwa wanaingia ubia na Wahindi kwa mgawanyo wa umiliki wa Wahindi (75%) na NHC (25%) ndiyo ulikuwa na uhujumu wa wazi wazi kwa sababu NHC kama minority shareholder hakuwa na sauti ya kutosha. Mchechu ni mmoja wa MaCEO wachache wa Kitanzania wenye uwezo mkubwa sana. Tukicheza atanyakuliwa na international corporations au aende nje ya nchi na sisi tubaki tunalialia kama ada yetu.
 
nyie mnataka muuziwe nyumba milion 10 au

Lengo la NHC ni nini?? Nani mwenye uwezo wa kununua nyumba kwa 100mill? kwa huu mshahara wa kuungaunga?? Hizo nyumba zitaendelea kununuliwa na wenye uwezo, ambao wengi wao tayari wana nyumba.
 
Nehemiah is an inspirational and transformational leader with high level of liveliness in business management. He was born and grew in Tanzanian where he emerged as the youngest CEO in East Africa region within 7 years, particularly in the highly regulated financial sector. He is a B.com (Finance) of the University of Dar es salaam. He started his career (1999) as a junior banker at Citibank and thereafter briefly joined Barclays Bank Tanzania before joining Standard Chartered Bank Tanzania Limited as a Head of Trading – responsible for Bank's balance sheet management, (assets and liabilities)(2001 – 2002).
In 2002 – 2004 he took further responsibility as a Head of Global market, before his promotion to the alternate director position – Head of Global Markets and Co – Head of Wholesale Banking where he served from 2004 – 2006.
His legacy has always been remarkable and his hand has always turned stones into gold, while at Standard Chartered Bank – he grew the business and at a later stage the business become a major contributor of revenue to the bank from 45% to 87% in 2005, whilst the number of products increased from 3 to 12.
In June 2006, he joined United Bank of Africa Tanzania which he managed to turn around from a loss making to profit making bank in less than a year.
Despite the aforementioned inspirational changes, Nehemiah has been a catalyst in various Financial and Economic reform activities; this includes working in various involvements in different capacities, as President of ACI- Financial Market Association – Tanzania Chapter and Chairperson of the Tanzania Financial Market Leadership Forum. He spent time to introduce global financial products while at Standard Chartered Bank this involved both BOT and Tanzania Bankers Association. Nehemiah, worked as a team Manager of the first successful Subordinated debt issue from a Commercial Banks in Tanzania and first one to be listed in the Dar Es Salaam Stock Exchange. This is the longest maturity corporate bond in East Africa to date.
He is currently the chairperson of the University Of Dar Es Salaam Faculty Of Commerce Alumnae (UDS-FCM Alumnae), A Board Chairman of the Rightways Schools, a board member of National Investment Company Limited (NICOL) and he is also a member of several country task forces.

He is not hardworking and not smart at all, he is simply lucky, the fact is every success is made out of lucky but unfortunately and always there should be someone to be credited for the self presented success.
 
Kiukweli na kwa moyo mkunjufu nampongeza sana Msechu kwa kazi kubwa aliyoifanya toka aliongoze shirika hilo. Hata hivyo bado pia ana kazi kubwa mbele yake iwapo ataongezewa mkataba mwingine. Nimwombe tu akaze buti na ahakikishe nyumba nafuu zinapatika kwa watanzania.

Hata hivyo kama ni kweli hii itauw ajabu sana kwa rais kushindwa kutmiza wajibu na majukumu yake eti kisa Msechu anafanyiwa hujuma! Hebu sma hii kitu..... "Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake."


kama una moyo mkunjufu nenda magu ukawatake radhi ukoo wako wanalalamika umewakana umenunua kabila unajifanya mtu wa nyanja.
 

Attachments

  • 1406387329258.jpg
    1406387329258.jpg
    41.9 KB · Views: 128
Kuna story nilisikia kama two weeks ago kwamba kuna ubadhirifu jamaa kafanya kupitia Wakurugenzi wa idara na Mameneja wake Mikoani na kuna ushahidi kibao umeshapelekwa vyombo vya juu, ikiwemo wizara ya ardhi. Ni vitu ambavyo vilinishtua coz binafsi Mchechu is my Role Model.....kaipaisha sana NHC.

Anyway, huenda ni majungu tu!

watu wengi hawamjui mchechu kwa 3D-ni mjanja na smart kuliko wengi wanavyo mjua, ikitokea ukafanya nae kazi ndo utamjua-to make it short ni mtu naye mjua sana sana na niwahakikishie kuwa hakuna anayemjengea Zengwe isipokuwa Gazet hili ndilo kaliandaa kumsafisha-na mkitambua ndipo mtajua kuwa kweli jamaa ni mchapa kazi ila sio mzalendo kama wengi mnavyodhan
 
KASI ya utendaji kazi ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Msechu imesababisha aundiwe zengwe kwa lengo la kutaka ang’olewe nafasi hiyo.

Jambo Leo, limeelezwa kuwa, tayari Msechu amepewa masharti mazito na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, yakiwamo ya kumtaka apunguze wakurugenzi wake katika idara mbalimbali.

Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa Msechu alipewa likizo wakati akitafakari masharti aliyopewa na bodi hiyo, inatokana na kumaliza muda wake, kabla ya kuingia naye makubaliano mengine ya kulitumikia shirika hilo, kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na uamifu wa hali ya juu.

Msechu ambaye alilikuta shirika hilo katika hali mahututi na kutumia nafasi yake kupanga safu ambayo imerudisha heshima ya NHC kwa kuendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na bei nafuu kwa ajili ya Watanzania, ameonekana kutofurahisha wale ambao hawapendi shirika hilo lifanye kazi yake kwa maslahi ya taifa.

Vyanzo vya kuaminika vimeliambia Jambo Leo kwa nyakati tofauti kuwa, Msechu kwa sasa amemaliza mkataba wake wa kulitumikia shirika hilo na kinachosubiriwa ni Serikali kupitia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumuidhinisha tena ili aweze kuendelea.

Hata hivyo, wakati anasubiri kuidhinishwa tena, mizengwe imeendelea kufanywa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

“Kwa sasa kinachoonekana ni kama vile kumuundia zengwe Msechu ili asiendelee katika nafasi hiyo ambayo ameifanya kwa uamunifu mkubwa. Kuna baadhi ya wajumbe wa bodi wanaotaka asirudi na ndiyo wanaochelewesha kumuidhinisha.

“Wameamua kumpa masharti mazito katika kipindi hiki wakitaka atafakari, na moja ya masharti hayo ni kwamba, apunguze idadi ya wakurugenzi wake kwenye idara, huku pia wakitaka apunguze mishahara ya watumishi wake.

“Yote hiyo ni kutaka kumvunja nguvu ili mikakati yao itimie. Sababu za msingi za kutoa masharti hayo hazipo, bali kinachoonekana utendaji wake wa kazi kwa kiwango cha kutukuka ndiyo unaosababisha wasiopenda mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete, wamchukie na kumtengenezea mazingira ya kumweka kwenye wakati mgumu,” kilisema moja ya chanzo cha taarifa hizo (jina tunalo).

Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake.Pia, Msechu ameshindwa kwenda kwenye maeneombalimbali ya miradi ya NHC inayoendelea sasa, na hiyoyote ilitokana na ukweli kwamba, hajafahamu hatma yake ndani ya shirika hilo.

Wakati hayo yakiendelea, utendaji kazi wa Msechu umekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo yote ni kutokana na kazi nzuri ambayo ameifanya ya kulitumikia taifa na kurudisha hadhi yake ambayo ilipotea. Rais Kikwete mara kadhaa amekuwa akizungumzia mafanikio ya shirika hilo ambayo yameletwa na Msechu kwa kushirikiana na wakuu wake wa idara na watumishi wengine.

Hotuba za Msechu ambazo amekuwa akizitoa katika maeneo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa miradi ya ujenzi, amekuwa akiweka wazi ushirikiano uliopo kati
yake na watumishi wengine, ni sawa na timu ya Real Madrid au Barcelona ambazo zinapokuwa uwanjani zinafanya kazi moja tu, ya kuhakikisha zinafanikiwa
kushinda.

Pamoja na hayo, imefahamika kuwa baadhi ya viongozi na wabunge ambao wamekuwa wakitumia shirika hilo kuweka ndugu, marafiki na jamaa zao wapo kwenye mkakati wa kuhakikisha Msechu anaondolewa NHC. “Baadhi ya viongozi na wabunge wamesimama kidete kuhakikisha Msechu harudi na hiyo inatokana na ukweli kwamba, hawakubaliani na misimamo ya mkurugenzi huyo ya kuhakikisha haki inatendeka katika kupata nyumba za shirika hilo,” kilisema chanzo kingine.

Alipotafutwa Profesa Tibaijuka ili kuzungumzia hatma ya Msechu, simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana. Hivyo juhudi za kumtafuta zinaendelea ili aweze kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo. Pia, Mchecu naye alipotafutwa kuzungumzia taarifa za vyanzo hivyo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

Chanzo: JamboLeo
Wakuu, pamoja na kukanushwa , hili zengwe bado lipo.
 
Acheni kubwabwaja bila kufanya utafiti. Mahesabu (Financial Statements) ya NHC ya kila mwaka yako wazi na yanakabiliwa na Waakaguzi nguri. Kama unauwezo ya kuyasoma utaweza kujua kama shirika lina au linaelekea kwenye financial crisis au hapana. Mojawapo ya hoja za ukaguzi ni kama kampuni ni 'going concern' maana yake ni kuwa haiko katika hatari ya kufilisika siku za karibuni. Kukopa kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi siyo jambo baya ilimradi miradi yenyewe iwe inazalisha fedha (cash flow) ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mikopo na vile vile shirika linapata faida. Wajenzi binafsi (private developers) wanauza nyumba kwa bei kubwa zaidi ya NHC na zinanunuliwa. Za NHC ni bei nafuu in comparison. Kwa hiyo financial crisis unayoitabiri ni ndoto zako tu. Mfumo wa zamani wa NHC ambapo walikuwa wanaingia ubia na Wahindi kwa mgawanyo wa umiliki wa Wahindi (75%) na NHC (25%) ndiyo ulikuwa na uhujumu wa wazi wazi kwa sababu NHC kama minority shareholder hakuwa na sauti ya kutosha. Mchechu ni mmoja wa MaCEO wachache wa Kitanzania wenye uwezo mkubwa sana. Tukicheza atanyakuliwa na international corporations au aende nje ya nchi na sisi tubaki tunalialia kama ada yetu.

Na hata likifilisika, who cares? Si tutakuwa tumeweka chetu kwa mfuko?
 
Hata yeye kafanya madudu kwenye ajira kwa kutumia vigezo ambavyo havikuwa kwenye matangazo husika na anajua alichofanya mambo mengine anajitakia mwenyewe
 
watu wengi hawamjui mchechu kwa 3D-ni mjanja na smart kuliko wengi wanavyo mjua, ikitokea ukafanya nae kazi ndo utamjua-to make it short ni mtu naye mjua sana sana na niwahakikishie kuwa hakuna anayemjengea Zengwe isipokuwa Gazet hili ndilo kaliandaa kumsafisha-na mkitambua ndipo mtajua kuwa kweli jamaa ni mchapa kazi ila sio mzalendo kama wengi mnavyodhan

humo nilipo bold nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa
 
najisikia furaha sana hasa mkoani Lindi kwa muda mrefu kuona nyumba zimekamilika kwa haraka 75%
 
Huyu Msechu ana vitu vyake positive lakini obviously ana upungufu mkubwa.
NHC haikuanzishwa kwa ajili ya matajiri bali watu wa kawaida. Kwenye mipango yake husahau hilo.

Ameanzisha miradi mipya. Ni kitu kizuri lakini napinga kujenga kwenye open spaces katikati ya maghorofa e.g. Ubungo na Keko. Hizo space ziliachwa makusudi kabisa. Kupata hewa, kupaki magari, sehemu za kucheza watoto etc.
Yeye kaamua kujenga kwenye space hizo. What a stupid idea. Kwa nini asijenge maeneo mpya na kuacha space kama hizo? Very poor thinking . Environmentally unfriendly.
 
awepo asiwepo hana faida na shirika lake kwasisi watz wa kima cha chini
 
Nyumba ya mil 600 au 700 ni kwa ajiri ya nani? NHC has lost a plot...sijui nani kawadanganya kuna wateja wengi wa kuweza kununua nyumba za aina hiyo. Wafikirie upya....kuna wateja wadogo...wa kati na wakubwa. Sio wakubwa peke yake
 
Back
Top Bottom