Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

mhalisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
1,181
Reaction score
322
KASI ya utendaji kazi ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Msechu imesababisha aundiwe zengwe kwa lengo la kutaka ang’olewe nafasi hiyo.

Jambo Leo, limeelezwa kuwa, tayari Msechu amepewa masharti mazito na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, yakiwamo ya kumtaka apunguze wakurugenzi wake katika idara mbalimbali.

Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa Msechu alipewa likizo wakati akitafakari masharti aliyopewa na bodi hiyo, inatokana na kumaliza muda wake, kabla ya kuingia naye makubaliano mengine ya kulitumikia shirika hilo, kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na uamifu wa hali ya juu.

Msechu ambaye alilikuta shirika hilo katika hali mahututi na kutumia nafasi yake kupanga safu ambayo imerudisha heshima ya NHC kwa kuendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na bei nafuu kwa ajili ya Watanzania, ameonekana kutofurahisha wale ambao hawapendi shirika hilo lifanye kazi yake kwa maslahi ya taifa.

Vyanzo vya kuaminika vimeliambia Jambo Leo kwa nyakati tofauti kuwa, Msechu kwa sasa amemaliza mkataba wake wa kulitumikia shirika hilo na kinachosubiriwa ni Serikali kupitia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumuidhinisha tena ili aweze kuendelea.

Hata hivyo, wakati anasubiri kuidhinishwa tena, mizengwe imeendelea kufanywa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

“Kwa sasa kinachoonekana ni kama vile kumuundia zengwe Msechu ili asiendelee katika nafasi hiyo ambayo ameifanya kwa uamunifu mkubwa. Kuna baadhi ya wajumbe wa bodi wanaotaka asirudi na ndiyo wanaochelewesha kumuidhinisha.

“Wameamua kumpa masharti mazito katika kipindi hiki wakitaka atafakari, na moja ya masharti hayo ni kwamba, apunguze idadi ya wakurugenzi wake kwenye idara, huku pia wakitaka apunguze mishahara ya watumishi wake.

“Yote hiyo ni kutaka kumvunja nguvu ili mikakati yao itimie. Sababu za msingi za kutoa masharti hayo hazipo, bali kinachoonekana utendaji wake wa kazi kwa kiwango cha kutukuka ndiyo unaosababisha wasiopenda mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete, wamchukie na kumtengenezea mazingira ya kumweka kwenye wakati mgumu,” kilisema moja ya chanzo cha taarifa hizo (jina tunalo).

Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake.Pia, Msechu ameshindwa kwenda kwenye maeneombalimbali ya miradi ya NHC inayoendelea sasa, na hiyoyote ilitokana na ukweli kwamba, hajafahamu hatma yake ndani ya shirika hilo.

Wakati hayo yakiendelea, utendaji kazi wa Msechu umekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo yote ni kutokana na kazi nzuri ambayo ameifanya ya kulitumikia taifa na kurudisha hadhi yake ambayo ilipotea. Rais Kikwete mara kadhaa amekuwa akizungumzia mafanikio ya shirika hilo ambayo yameletwa na Msechu kwa kushirikiana na wakuu wake wa idara na watumishi wengine.

Hotuba za Msechu ambazo amekuwa akizitoa katika maeneo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa miradi ya ujenzi, amekuwa akiweka wazi ushirikiano uliopo kati
yake na watumishi wengine, ni sawa na timu ya Real Madrid au Barcelona ambazo zinapokuwa uwanjani zinafanya kazi moja tu, ya kuhakikisha zinafanikiwa
kushinda.

Pamoja na hayo, imefahamika kuwa baadhi ya viongozi na wabunge ambao wamekuwa wakitumia shirika hilo kuweka ndugu, marafiki na jamaa zao wapo kwenye mkakati wa kuhakikisha Msechu anaondolewa NHC. “Baadhi ya viongozi na wabunge wamesimama kidete kuhakikisha Msechu harudi na hiyo inatokana na ukweli kwamba, hawakubaliani na misimamo ya mkurugenzi huyo ya kuhakikisha haki inatendeka katika kupata nyumba za shirika hilo,” kilisema chanzo kingine.

Alipotafutwa Profesa Tibaijuka ili kuzungumzia hatma ya Msechu, simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana. Hivyo juhudi za kumtafuta zinaendelea ili aweze kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo. Pia, Mchecu naye alipotafutwa kuzungumzia taarifa za vyanzo hivyo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

Chanzo: JamboLeo
 
Hii inchii ya vivuruge isiopenda maendeleo.mashirika mengi yalikufa kwa stlye hii
 
kusema kweli huyu jamaa amefanya kazi kubwa hakuna mfano.., na uzuri wa kazi za ujenzi huwa zinaonekana.., yaan mi mpaka nilianza kujiuliza huyu ni mTanzania kweli..?! maan waTz hatuna kabisa uzalendo.., tunawaza kuiba tuuu bila kujua tunamuibia nani...! Shirika la ndege naona angepewa yeye ndio awe mkurugenzi.., seriously tutakuwa mbali. Ila kinachoniogopesha ni kwamba mama TIBAIJUKA IS TOO WEAK!! She is very linient.., naogopa atayumbishwa ovyo ovyo..!
 
Serikalini bana yani ukichapa kazi unaonekana tatizo

huo ndio ukweli wenyewe...hata hivyo alibeba watu wengi kama wakurugenzi tena kwa gharama kubwa pengine kuliko hela wazichangazo wajumbe wa bodi. Sasa nani atamtaka aendelee kuneemeka hapo. Halafu watu tunajinadi eti wazalendo....kaazi kweli kweli. Wazalendo wapo wachache sana...wengi ni maslahi tu
 
..aliuliza kadi yake ya chama iko akashindwa kutoa maelezo....akapewa kadi ya njano kote kote
 
Kwani hiyo nafasi si anateuliwa na Rais? au Wajumbe wa bodi ya Wagurugenzi inayomamlaka ya kumpiga chini?
 
Gazeti la serikali legevu ya magamba halijui jina la Mkurugenzi wa shirika la nyumba-shirika la umma.
Mchechu wao wanaandika Msechu... hatahivyo kwa maoni yangu juu ya Mchechu amefanya kazi kubwa sana ya kulifufua shirika la nyumba lililokuwa kaburini.

Miradi mingi ya nyumba inayoendelea kujengwa katika kona mbalimbali za nchi hii ni dalili ya wazi kuwa sasa kazi zinafanyika. Na Mchechu amefanya bidii kubwa sana kwakuwa miradi mingi kama si yote wanayotekeleza wanatumia juhudi zao wenyewe kwa kukopa fedha kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na hawapati hata shilingi moja kutoka serikalini kwa ajili ya uendeshaji wa miradi yao ya nyumba.
 
Mimi simjui Nehemia na wala kumjua haina msaada wowote ule na utendaji wake. Mimi napima uwezo wake kulingana na historia yake ya utendaji kutoka CBA mpaka NHC. CBA was a dead bank ila Nehemia alikuja and turned it a profit making bank like wise NHC ya nyuma na hii ya sasa. This proof does not need this stupid tool kwamba unamjuwa sijui umesoma nae au mmekaa nae Dar no.

Hivi wewe unaebisha kuwa NKM si mzuri have you ever met this young male in a platform???? Unless you do not have access to those technical platforms. Mimi kwakweli I give my big ups to these NHC guys, Raymond Mndolwa, David Shimbwe etc.
 
Mchechu jiweke pembeni mwenyewe, hata mwezi tu, kama hajakutafuta! au NHC kama haijawekwa kuwa Muflisi....
 
Nehemiah is an inspirational and transformational leader with high level of liveliness in business management. He was born and grew in Tanzanian where he emerged as the youngest CEO in East Africa region within 7 years, particularly in the highly regulated financial sector. He is a B.com (Finance) of the University of Dar es salaam. He started his career (1999) as a junior banker at Citibank and thereafter briefly joined Barclays Bank Tanzania before joining Standard Chartered Bank Tanzania Limited as a Head of Trading – responsible for Bank’s balance sheet management, (assets and liabilities)(2001 – 2002).
In 2002 – 2004 he took further responsibility as a Head of Global market, before his promotion to the alternate director position – Head of Global Markets and Co – Head of Wholesale Banking where he served from 2004 – 2006.
His legacy has always been remarkable and his hand has always turned stones into gold, while at Standard Chartered Bank – he grew the business and at a later stage the business become a major contributor of revenue to the bank from 45% to 87% in 2005, whilst the number of products increased from 3 to 12.
In June 2006, he joined United Bank of Africa Tanzania which he managed to turn around from a loss making to profit making bank in less than a year.
Despite the aforementioned inspirational changes, Nehemiah has been a catalyst in various Financial and Economic reform activities; this includes working in various involvements in different capacities, as President of ACI- Financial Market Association – Tanzania Chapter and Chairperson of the Tanzania Financial Market Leadership Forum. He spent time to introduce global financial products while at Standard Chartered Bank this involved both BOT and Tanzania Bankers Association. Nehemiah, worked as a team Manager of the first successful Subordinated debt issue from a Commercial Banks in Tanzania and first one to be listed in the Dar Es Salaam Stock Exchange. This is the longest maturity corporate bond in East Africa to date.
He is currently the chairperson of the University Of Dar Es Salaam Faculty Of Commerce Alumnae (UDS-FCM Alumnae), A Board Chairman of the Rightways Schools, a board member of National Investment Company Limited (NICOL) and he is also a member of several country task forces.
 
Haya kwa mazuri yote tuliyoyaona aliyofanya mchechu pamoja na kufufua hili shirika je ni faida gani wamepata watu wa hali ya chini hasa wanaotegemea makazi haya ya NHC au tunachekelea tuu haya majengo ya vioo yaliosimama huku mjini bila kujua umiliki wake halali na kodi zake?
 
Kiukweli na kwa moyo mkunjufu nampongeza sana Msechu kwa kazi kubwa aliyoifanya toka aliongoze shirika hilo. Hata hivyo bado pia ana kazi kubwa mbele yake iwapo ataongezewa mkataba mwingine. Nimwombe tu akaze buti na ahakikishe nyumba nafuu zinapatika kwa watanzania.

Hata hivyo kama ni kweli hii itauw ajabu sana kwa rais kushindwa kutmiza wajibu na majukumu yake eti kisa Msechu anafanyiwa hujuma! Hebu sma hii kitu..... "Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake."
 
Mimi simjui Nehemia na wala kumjua haina msaada wowote ule na utendaji wake. Mimi napima uwezo wake kulingana na historia yake ya utendaji kutoka CBA mpaka NHC. CBA was a dead bank ila Nehemia alikuja and turned it a profit making bank like wise NHC ya nyuma na hii ya sasa. This proof does not need this stupid tool kwamba unamjuwa sijui umesoma nae au mmekaa nae Dar no.

Hivi wewe unaebisha kuwa NKM si mzuri have you ever met this young male in a platform???? Unless you do not have access to those technical platforms. Mimi kwakweli I give my big ups to these NHC guys, Raymond Mndolwa, David Shimbwe etc.
Watanzania watu wa kimasikini sana kimawazo.
Ukifanya juhudi kubwa kuineemesha serikali wao wanaanza kukuchimba.
Hapo NHC, lazima kuna mtu , tena kigogo, anaitafuta nafasi hiyo ili ajineemeshe.
Huyu kijana wa management style ya dunia ya leo, Nehemia Kyando Mchechu , ameitoa NHC around from a point of bankruptcy!
Lakini wahenga wanasema , shukrani ya punda(serikali) ni mateke!
 
Watu wanaropoka tu wala hawajui operation modal ya NHC, hili shirika sasa hivi linaendeshwa kibiashara linadaiwa mikopo ya bank (Mortgage finance) kama bishara nyingine zozote zile. Sasa nyie mkitaka liendeshwe kama lile la zamani you are wrong.
 
Back
Top Bottom