Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Mchechu wa NHC aundiwa zengwe

Wewe Mbulumundu, ili nyumba za bei nafuu unazotaka na mambulumundu wenzio zipatikane lazima serikali iweke ruzuku ya fedha. Kokote kule unakoona serikali duniani zimesaidia kupatikana nyumba za bei nafuu na kwa kuweka hela sio kwa njia ya mkato. Hilo shirika la nyumba linanunua cement, kokoto, mchanga na vifaa vyote vya ujenzi unakonunua wewe, sasa hizo nyumba za bei nafuu zitapatikanaje hapo? Au unataka shirika lijenge NYUMBA ZA TEMBE AU NYASI kama alizokuwa anakaa Babu yako kijijini?

Dr Slaa aliwaambia mumchague awashushie bei ya cement hadi shs 5,000 kwa mfuko mkamkataa na kuchagua mcheza ngoma, sasa isomeni namba
#mbulumundu
 
Acheni ushabiki wa kijinga! Jiulizeni kwanza maswali ya msingi ? Board hiyo kazi yake ni nini? ni kweli Mchechu amefanya kazi kubwa NHC hatukatai lakini tujiulize mchango wa Shirika hilo kwa maendeleo ya Taifa ni nini! Au ni kuboresha tu mishahara ya watumishi wa Shirika hilo? NHC sasa hivi wanatoza kubwa kodi kubwa za pango kuliko private sector! Mfano katika jengo lao jipya wanalomalizia hapa Musoma kodi ya "fremu" ni kati ya laki tatu hadi laki nne !kwa mzunguko wa biashara gani!? tatizo hapa nchini tumekuwa na ushabiki wa kijinga kwa kila kitu ! na hii ni kutokana ma-graduate wengi wa vyuo vikuu vya kata wasio na kazi mtaani ! Nehemia lazima mwisho wa siku lazima ajue vision ya shirika ni kusaidia Watanzania na si kuwanyonya Watanzania! Amefanya vizuri ku-improve image ya shirika lakini kama ataki kubadilika kuhusu rates anazotoza basi ama aombe tumbinafsishie shirika hili ama Board imfukuze tu aende akafanyie ujasiriamali wake kwingine! CCM kuweni macho na Mchechu mkimchekea na sifa za kijinga mtazikosa kura za wafanyabiashara wengi walioko NHC 2015!

Halafu mnasema amejenga majengo mengi, shit!! kwa pesa ipi?? Jibu ni mikopo kutoka banks, hamjaongelea mikopo hiyo iki-mature je kuna pesa ya kufanya -repayment?? Nadhani miaka michache ijayo mtegemee financial crisis kwa NHC kushindwa kulipa mikopo ya bank yaliyofanya consortum na kufinance NHC. Nadhani board wameliona hilo risk wanatafuta namna ya ku-mrestisha.
Nyumba za NHC bei juu haziuziki, then mwisho wa siku watabaki na majumba yasiyouzika moja ya sababu kodi kubwa. Bila kuuza hizo nyumba atalipaje mikopo.Namshauri Mchechu awe mpole asipewe Nkataba ili apate kusepa kabla ya kupigwa pingu kwa kusababisha hasara.
 
Sector ya nyumba Tanzania ni majanga, Mchechu atapotezea hadhi hapo kwani hiyo mikopo hawatailipa, kwani ujengaji wa nyumba hauendi sambamba na uuzaji.Mwisho wa siku ni LIQUIDITY PROMBLEM kwa NHC. Kuna jamaa yangu amekopa na kujenga nyumba ili auze, na kujenga tena kinachompata leo ni majanga nyumba haiuziki imebidi apige bei shamba lake la hecta 1000 ili alipe mkopo wa bank kuondoa stress za kibank.
 
Bwn Msoma anayo point
hivi wangapi wanaishi au wanajua kodi ya sasa ya nyumba za NHC, hilo siyo shirika binafsi hivyo kuna vitu ambavyo lazima viwe considered.
NHC chini ya mchecu inachaji gharama ya kuchonga barabara, kuweka nguzo, mabomba ya maji n.k vyote vinawekwa kwenye bei ya nyumba au kodi hiyo bado mnaona sawa?

Ajibu hizo zilizo semwa hoja, au waziweke wazi tuzijue

SP

Kwani hizo gharama si shirika linagharamia au nguzo za umeme kwa mfano, TANESCO hutoa bure?, mabomba ya maji je? DAWASCO hutoa bure? NHC wakienda kwenye viwanda ama maduka ya Hardware wanapewa vifaa bure?., Barabara je Halmashauri za miji ndo zinachonga au shirika linagharamia miundombinu hii kwenye estate zake inazojenga, Je serikali ilishawahi toa ruzuku kwenye vifaa vya ujenzi kwa project za NHC? au kutoa nafuu ya kodi kwa wakandarasi wanaojenga nyumba za NHC?...NHC inakopa ili kujenga na kuuza nyumba hizi, wanarudishaje fedha hii....Umewahi fikiria kuhusu miradi ya mifuko ya jamii inayojengwa kwa fedha za michango ya wafanyakazi zinauzwa bei gani?...call a spade a spade and a spoon a spoon NHC na mchechu waunafanya kazi nzuri. Kama CEOs wote wa taasis za umma wangekuwa kama huyu jamaa, Tanzania ingekuwa mbali mno.......
 
Mleta mada, "zengwe" hapo liko wapi?

Dah! mbona bodi ya wakurugenzi kutoa ushauri katika vikao vya bodi ni mambo ya kawaida sana.

Nashangaa mtu unajaribu kila njia kuifanya habari ioneshe kuna "zengwe" wakati halionekani.

Watanzania ni mahodari sana kwa majungu na aliyeandika huu udaku ni mmoja wao.

Mleta mada, "zengwe" hapo liko wapi?

Unajua nimesoma mada na aina ya uchangiaji najiuliza hata kama wengi wa wachangiaji wanaelewa wanacho jadili. Hivi Bodi kumwambia Mchechu apunguze Kurugenzi kutoka 12 mpaka 4 ni wazo la kijinga?? Wakurugenzi 12 wanafanya kazi gani pale? Kwasababu wengi marafiki zake basi asiguswe?

Dada yangu nashangazwa zaidi na wale wanao sema Mchechu ameikuta NHC hoi,kweli wanaelewa wanacho kiomgea? Hili ni Shirika ambalo siku zote limekua imara na ndio maana Serikali haikuliingiza ktk Mashirika ya Umma ya kubinafsishwa!

Kikwazo kikubwa cha mapato ya NHC ilikua sheria iliyo kuwa inawabana wasipandishe kodi ambayo ilisimamiwa kidete na Waziri Magufuli akiwa Ardhi na Menejimenti iliyo tangulia ikabadilishwa na baada ya kuongezeka kodi mapato ya shirika yameongezeka zaidi.
 
Unajua nimesoma mada na aina ya uchangiaji najiuliza hata kama wengi wa wachangiaji wanaelewa wanacho jadili. Hivi Bodi kumwambia Mchechu apunguze Kurugenzi kutoka 12 mpaka 4 ni wazo la kijinga?? Wakurugenzi 12 wanafanya kazi gani pale? Kwasababu wengi marafiki zake basi asiguswe?

Dada yangu nashangazwa zaidi na wale wanao sema Mchechu ameikuta NHC hoi,kweli wanaelewa wanacho kiomgea? Hili ni Shirika ambalo siku zote limekua imara na ndio maana Serikali haikuliingiza ktk Mashirika ya Umma ya kubinafsishwa!

Kikwazo kikubwa cha mapato ya NHC ilikua sheria iliyo kuwa inawabana wasipandishe kodi ambayo ilisimamiwa kidete na Waziri Magufuli akiwa Ardhi na Menejimenti iliyo tangulia ikabadilishwa na baada ya kuongezeka kodi mapato ya shirika yameongezeka zaidi.

Wasamehe, hawajui wanachokiongea.
 
Mojawapo wa ishu hot kwasasa ni habari za kuundiwa zengwe ili mkurugenzi mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu aondolewe kwenye wadhifa huo baadhi ya wabunge na pengine mawaziri wakihusishwa.

Tunaifahamu NHC ilivyokuwa kabla ya Mchechu na tunaiona Hindi ilivyo sasa chini ya uongozi wake. Ameijengea heshima ameikuza ameibadili ina mwelekeo sasa.

Tofauti na Mchechu kuna Mkurugenzi mkuu wa Bandari Madeni Kipande ambaye gazeti la JAMHURI bila woga liliripoti kwa kina kashfa zake kwa wiki kadhaa.Madeni analiuwa shirika anafanya mengi ya ajabu habari zake zimeandikwa sana.

Litakuwa jambo la ajabu ya karne Mchechu akiondolewa kwenye wadhifa wake huku Kipande akiachwa.

Nataraji upinzani toka kwa wale wanaounga mkono ufisadi.
 
Hivi ndivyo Tanzania ilivyonajisiwa CCM,waadilifu hawatakiwi.
 
siku zote taifa hili lililoshindikana taifa yenye malaria taifa linaongozwa na ccm na hao hso ccm hawataki maendeleo nchini......kama mtu akiwa mchapa kazi kamwe hawato mkubali watamundia zengwe....ila kwa mchechu wataumbuka tu kwani mabadiliko aliyoyafanya yanajulikana
 
Nyumba za shirika hilo lililoanzishwa miaka hiyo ya asali na maziwa nyingi zilinyang'anywa toka kwa wa_asia wakapewa wafanyakazi wa serikali waishi, kwa sasa imekuwa kinyume shirika lina asilimia chache ya raia wa nchi hii kama wapangaji. Kiufupi khali imekuwa kinyume na malengo yake hususan kwa upande wa jiji la Dar.
 
*****
Hii "ishu hot" imekanushwa na Bodi ya NHC kwamba siyo kweli ***** Tuendelee na "Utupaji wa Viungo vya Binadamu*****
 
Huyu bwana aliingia vibaya hasa pale alipotumia strategy ya kununua vyombo vya habari. Kwa mfano clouds ndio amewamaliza kabisa. Issue ya kuondolewa kwenye nafasi yake ilipoibuka juzi nilishangaa power breakfast ikiipinga kwa nguvu hadi nikashangaa sana. Na leo eti yale magazeti yaliyoandika hiyo issue eti wamekataa kuyasoma katika uchambuzi wao wa magazeti.
 
tupewe ukweli tusidanganywe mwisho tutaelewa, nasikia mengi yapo nchi hii mmmmh
 
Mojawapo wa ishu hot kwasasa ni habari za kuundiwa zengwe ili mkurugenzi mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu aondolewe kwenye wadhifa huo baadhi ya wabunge na pengine mawaziri wakihusishwa.

Tunaifahamu NHC ilivyokuwa kabla ya Mchechu na tunaiona Hindi ilivyo sasa chini ya uongozi wake. Ameijengea heshima ameikuza ameibadili ina mwelekeo sasa.

Tofauti na Mchechu kuna Mkurugenzi mkuu wa Bandari Madeni Kipande ambaye gazeti la JAMHURI bila woga liliripoti kwa kina kashfa zake kwa wiki kadhaa.Madeni analiuwa shirika anafanya mengi ya ajabu habari zake zimeandikwa sana.

Litakuwa jambo la ajabu ya karne Mchechu akiondolewa kwenye wadhifa wake huku Kipande akiachwa.

Nataraji upinzani toka kwa wale wanaounga mkono ufisadi.

Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa kiza
 
Tukumbuke siko zote kuwa mtenda mema siku zote huwa hana siku nyingi za kuwepo mahali alipo,hivyo sishangai Mchechu akipigwa zengwe maana kaua sana mirija ya watu pale NHC.
 
Aende tu maana kwanza nasikia kwenye interview alikuwa mtu wa tatu sasa fikilia mtu wa kwanza na wa pili kwa nini hawakuchukuliwa akachululiwa yeye Nehemia Mchechu. Kila zama na kitabu chake wacha kwanza tudeal na Nehemia Mchechu then Madeni Kipande atafuata
 
Kiukweli na kwa moyo mkunjufu nampongeza sana Msechu kwa kazi kubwa aliyoifanya toka aliongoze shirika hilo. Hata hivyo bado pia ana kazi kubwa mbele yake iwapo ataongezewa mkataba mwingine. Nimwombe tu akaze buti na ahakikishe nyumba nafuu zinapatika kwa watanzania.

Hata hivyo kama ni kweli hii itauw ajabu sana kwa rais kushindwa kutmiza wajibu na majukumu yake eti kisa Msechu anafanyiwa hujuma! Hebu sma hii kitu..... "Imeelezwa kuwa, kutokana na mambo yanayoendelea dhidi ya Msechu, ndiyo maana hata Rais Kikwete alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Tanga, hakwenda zaidi ya kutuma mwakilishi wake."

Tamka kimoyo-moyo "Mchechu" mara 5 na usirudie tena huu ujinga wako, na uwaambie hao wenzako wa gazeti lililoandika habari hii wafanye vivyo hivyo.
 
sijui mpaka mlambwe miguu...badilikeni lazima mkubali kuwa mageuzi yamefanywa
 
Pamoja na uchapaji kazi ana "godfather" ???!!!!

Kama hayuko na chama na hana "nguzo" hata akirudi atakaa kwa shida sana!!!!!
Ndio ugumu wa madaraka ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom