Bilioni 2.6 Zimetengwa Kwaajili ya Kugharamia Taulo za Kike

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,165
1,026
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Zainab Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali ilitenga Sh Bilioni 2.64 kwa ajili ya kugharamia taulo za kike ambapo kati ya fedha hizo Sh bilioni 1.06 ni za ruzuku ya uendeshaji na Sh bilioni 1.58 ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mhe Katimba ameyasema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Nora Waziri Mzeru aliyehoji nini mpango wa Serikali kutenga bajeti kwa ajili ya taulo za kike mashuleni.

Amesema hadi kufikia Machi, 2024 Sh Bilioni 2.2 zimetumika ambapo pia wadau mbalimbali walichangia jumla ya Sh bilioni 1.5 na miradi ya shule ya elimu ya kujitegemea ilichangia Sh milioni 119.5

Mhe Katimba amezisisitiza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili ya upatikanaji wa taulo za kike shuleni Zainab Katimba.

GGM9hoqWoAAFxcH.jpg
GLNk8PCWoAA94up.jpg
 
Hebu ongezeni sauti kidogo, maana huku kijijini hata hiyo taulo ya kike ni msamiati mpya kwa watoto wangu
 
Je hizo Fedha zimewafikia walengwa au zimeishia kwenye ufisudi. Ripoti ya CAG inasemajegi
 
Back
Top Bottom