Mbunge Nancy Nyalusi atoa shilingi Milioni 10 kusaidia ujenzi wa wodi ya wanawake Ilala Simba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
MBUNGE MHE. NANCY NYALUSI AMETOA SHILINGI MILIONI 10 KUSAIDIA UJENZI WA WODI YA WANAWAKE ILALA SIMBA.

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Iringa Mhe. Nancy Nyalusi ametoa Shilingi Milioni 10 kwa uongozi wa kijiji cha Ilalasimba kilichopo katika kata ya Nzihi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa wodi ya wanawake kwenye zahanati ya kijiji hicho kama sehemu ya mchango wake kusaidia juhudi za serikali katika kukabiliana na changamoto ya vifo vya mama na mtoto.

Mhe. Nyalusi amefanya ziara hiyo kwenye kijiji hicho cha Ilalasimba akiwa ameongozana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Vijijini akiwemo Katibu wa chama hicho kwenye wilaya hiyo Ndg. Gama J. Gama.

Mhe. Nancy Nyalusi amesema ameamua kufanya hivyo kwanza kabisa ni kutekeleza majukumu yake kama mbunge lakini pia ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye kuboresha huduma za afya nchini.

Aidha Mhe. Nyalusi ameahidi kuendelea kuwa jirani na jamii katika kutatua kero zao jambo ambalo amesema litasaidia kuimarisha ustawi wa jamii kwa kiasi kikubwa.

"Mimi kwa nafasi yangu kama Mbunge nina wajibu wa kuona njia ya kusaidia kutatua kero zenu wananchi na ndio maana leo nipo hapa, na kwa kuwa nina guswa na kero ya afya leo nimeleta kiasi cha Shilingi Milioni 10 ili zisaidie kujenga wodi ya wanawake kwenye zahanati hii ya kijiji chenu"-amesema Mhe. Nancy Nyalusi.

WhatsApp Image 2023-02-17 at 07.45.47(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-02-17 at 07.45.45(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-02-17 at 07.45.45.jpeg

WhatsApp Image 2023-02-17 at 07.45.36.jpeg
 

MBUNGE MHE. NANCY NYALUSI AMETOA SHILINGI MILIONI 10 KUSAIDIA UJENZI WA WODI YA WANAWAKE ILALA SIMBA.​

Haisaidii, homa ya 2025 iko pale pale. Chadema "itawatoboa" macho! Hao akina mama watakuwa wamesahau, watanzania inaelekea hamjawasoma
 
Naona ameanza kupasha pasha misuli. Mbunge wa Jimbo akiona hivyo tumbo joto.
 
Ametoa au amesema atatoa? Ni fedha yake mfukoni au ni hizi za umma anasema ametoa? Maana siku hizi hata fedha za umma zinaitwa ni fedha za Rais!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom