Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MHE. NANCY NYALUSI (MB) ATOA MSAADA MAGODORO 50 KWA SHULE YA WALEMAVU
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Mhe. Nancy Nyalusi tarehe 24/2/2023 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambapo Pamoja na mambo mengine ametembelea Shule ya Msingi Mchanganyiko Makalala iliyopo wilayani humo na kutoa msaada wa magodoro 50 kwa uongozi wa shule hiyo ili kusaidia kupunguza mzigo wa changamoto ya magodoro katika shule hiyo ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali.
Katika ziara hiyo Mhe. Nyalusi ameongozana na viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Mufindi.
Aidha, Mhe. Nyalusi ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya maboresho kwenye miundombinu ya elimu katika maeneo mengi mkoani Iringa jambo ambalo amesema halipaswi kufumbiwa macho badala yake ni vyema likasemwa ili kila mmoja ajue mambo yanayofanywa na Serikali.
#KAZIIENDELEE #CCM #IRINGA
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.14.jpeg67.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.14(1).jpeg60.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.17(2).jpeg62 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.17(1).jpeg55 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.17.jpeg50.1 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.16(2).jpeg67.3 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-02-25 at 13.27.16(1).jpeg73.2 KB · Views: 3