Mbunge Nancy Nyalusi - Wanawake Tumuunge Mkono Rais Samia Suluhu Hassan

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE NANCY NYALUSI - WANAWAKE TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Mhe. Nancy Nyalusi amewataka wanawake mkoani Iringa kuendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake madhubuti na usimamizi wake mzuri wa rasilimali nchi ambao umesaidia kwa sehemu kubwa kusogeza maendeleo kwenye maeneo mengi ikiwemo mkoa wa Iringa.

Mbunge Mhe. Nyalusi ameyasema hayo katika ziara yake kwenye kata ya Luhota iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Katika ziara hiyo ambayo ni sehemu ya muendelezo wa ziara zake katika maeneo mbalimbali mkoani Iringa, Mhe. Nyalusi aliambatana na viongozi mbalimbali katika ngazi ya wilaya na mkoa wakiwemo Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi na Katibu wa UWT mkoa wa Iringa Bi. Camila Kigosi.

Mhe. Nyalusi amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inastahili pongezi kwani katika maeneo mengi mkoani Iringa ikiwemo kata ya Luhota fedha nyingi zimepelekwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na tuongeze maombi kwa Imani ya dini zetu kumuombea kiongozi wetu kwani yapo mengi amefanya na mengi anakusudia kuyafanya kwenye maeneo yetu kwa ujumla" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa

Mhe. Nancy Nyalusi Amesema kwa mkoa wa Iringa pekee Serikali imetoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, miundombinu na sekta nyingine kadhaa.

Aidha, Mbunge Nyalusi amewataka wanawake kwenye kata hiyo kuendelea kuunda vikundi ili iwe rahisi kwao kunufaika na mipango ya Serikali hasa mikopo kwa ajili ya wanawake.

Mhe. Nancy Nyalusi Akijibu risala ya wanawake katika kata hiyo Mbunge Mhe. Nancy Nyalusi ametoa Shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya ya Iringa Vijijini.

IMG-20230723-WA0086.jpg
 

Attachments

  • IMG-20230723-WA0092.jpg
    IMG-20230723-WA0092.jpg
    203.4 KB · Views: 3
  • IMG-20230723-WA0090.jpg
    IMG-20230723-WA0090.jpg
    67.4 KB · Views: 3
  • IMG-20230723-WA0085.jpg
    IMG-20230723-WA0085.jpg
    81.2 KB · Views: 4
  • IMG-20230723-WA0088.jpg
    IMG-20230723-WA0088.jpg
    60.3 KB · Views: 4
  • IMG-20230723-WA0087.jpg
    IMG-20230723-WA0087.jpg
    60 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-23 at 20.56.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-23 at 20.56.53.jpeg
    64 KB · Views: 3
Back
Top Bottom