Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MHE. NANCY NYALUSI AHOJI KADCO INASIMAMIA SHUGHULI ZA UWANJA WA NDEGE WA KIA KWA MKATABA UPI?
"Nampongeza sana CAG kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuweza kubaini madudu. Ucheleweshaji wa Malipo kwa wakandarasi umesababisha riba ya Shilingi Bilioni 68.77 kwa Serikali kwa taasisi 12. Hapo hatujazungumzia kwenye Halmashauri na Wizarani" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Hali ni mbaya, tatizo ni kubwa, limeendelea kukua siku kwa siku. Ifike mahali watendaji wa Wizara wamuonee huruma Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais anahaingaika usiku na mchana kuhakikisha kwamba anatafuta fedha kwaajili ya miradi ya Maendeleo" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Mimi nina ushauri (Kuhusu ripoti ya CAG) Naomba ufanyike ukaguzi Maalum kwenye taasisi 12 ili tujue chanzo cha tatizo ni nini ili tuweze kutatua tatizo hili maana inaweza kuonekana ni chaka la watu kuiba fedha za Serikali" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Bunge la 12 Mkutano wa 9 tarehe 2 Novemba, 2022 Bunge liliadhimia kwamba shughuli zote za Uwanja wa Ndege wa KIA zisimamiwe na TAA, lakini hadi kufikia Septemba 2023 shughuli za KIA zilikuwa bado zinasimamiwa na KADCO. Waziri atuambie KADCO inasimamia kwa Mkataba upi na utaratibu upi" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Wizara husika imepuuzia azimio la Bunge kwasababu hawajafanyia kazi utekelezaji na hamna taarifa yoyote na hii ni kuonyesha dharau kubwa kwa Bunge. Haiwezekani Bunge tunakaa tunaweka maazimio lakini hakuna kinachofanyiwa kazi" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa