Mbunge Martha Mariki akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,067
994

maxresdefaultsdawqe.jpg

"Nampongeza Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu la Tanzania na jinsi ambavyo ameendelea kuboresha Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo inasababisha wananchi tuendelee kukaa katika hali ya ulinzi na usalama" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nampongeza Mheshimiwa Waziri, Mhandisi Masauni pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Naipongeza Kamati ya Bunge ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa jinsi ambavyo imeendelea kuishauri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuangalia namna nzuri ili Wizara iweze kufanya kazi vizuri katika kuboresha usalama wa nchi yetu"

"Suala la gari la Zimamoto katika Mkoa wa Katavi, Naishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwaajili ya kuleta magari ya Zimamoto nchini lakini Mkoa wa Katavi ni takribani miaka 10 tumekuwa hatuna gari la Zimamoto, tumekuwa tukitumia gari la Airport. Unaweza kuona Mkoa wa Katavi tuko kwenye hali ya hatari, Ndege inapotua Mpanda na ikajitokeza shida"

"Ninaomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mgao wa magari yaliyokuja, Ninaomba sana utupe kipaumbele sisi wananchi wa Mkoa wa Katavi ili tuweze kupata gari la Zimamoto" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Naipongeza Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya Polisi nchini na kujenga vituo vya Polisi Kata katika maeneo yote nchini. Katika Mkoa wa Katavi tunaiomba sana Serikali tuna kituo cha Polisi katika Wilaya ya Mpanda, ni kituo chakavu cha miaka mingi, Wizara itenge fedha kwaajili ya ukarabati"

"Wilaya ya Tanganyika wananchi wametoa nguvu kazi zao kujenga Kituo cha Polisi lakini naomba Wizara itukumbuke wananchi wa Wilaya ya Tanganyika kwa kutenga fedha kwaajili ya Umaliziaji wa kituo" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Tuna changamoto kubwa ya makazi duni ya polisi katika Mkoa wa Katavi na katika maeneo yote nchini. Naiomba Wizara, Polisi wanafanya kazi nzuri sana katika Taifa letu la Tanzania lakini ni dhahiri wamekuwa wakikaa katika makazi ambayo hayaridhishi, Serikali itenge fedha kuboresha makazi ya Askari ili tuweze kuwapa hamasa (Motisha)"

"Serikali imetenga fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi maeneo ya Dodoma, Arusha na Dar es Salaam lakini mikoa ya pembezoni makazi yao ni duni sana hayaridhishi, naomba tuwakumbuke Polisi hususani mikoa ya pembezoni na katika maslahi mbalimbali maana wanafanya kazi nzuri na tunaweza kuwalaumu kuingia katika rushwa lakini maslahi yao ni duni" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Suala la Sayansi na Teknolojia katika Majeshi yetu yote nchini ikiwemo Jeshi la Magereza, Zimamoto na Uhamiaji. Niombe Wizara, ni muda sahihi wa kutenga fedha kwaajili ya kuwekeza katika Sayansi na Teknolojia badala ya Mwananchi anaenda kutoa malalamiko yake anapopata shida ziwepo Kamera na vitendea kazi Maalum ambavyo vitaweka rekodi itakayotunzwa ili katika hatua ya Mahakama pawe na kumbukumbu nzuri na kuepusha ubabaishaji"

"Kuna video ilikuwa inasambaa Mitandaoni ikionyesha Mama akilalamika kuwa mtoto wake amelawitiwa na amekwenda kutoa malalamiko kwa Jeshi la Polisi lakini kesi inapigwa danadana hapati haki yake, Niombe sana Jeshi la Polisi waweze kushughulikia malalamiko hayo" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
 
Back
Top Bottom