Mbunge Aysharose Mattembe akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,153
1,023
"Namshukuru MUNGU kwa Baraka na Rehema zake kwa kuendelea kunijalia afya njema. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya Hospitali za Wilaya, Hospitali za Mikoa, Hospitali za Kanda, Hospitali ya Taifa, Zahanati, Vituo vya Afya, na vifaa tiba" - Mhe. Aysharose Mattembe, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida.

"Wanawake wa Mkoa wa Singida wamenituma nikufikishie salamu Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Wanakupenda sana, wako bega kwa bega na Rais katika adhma ya kuwaletea Wananchi maendeleo. Pia, wameahidi ifikapo mwaka 2025 wanasimama na Rais Samia na watampa ushindi wa kishindo"

"Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida imekuwa na ujenzi wa kusuasua tangu mwaka 2014 hadi sasa takribani miaka 11 ilihali Hospitali za Mikoa mingine zimeshakamilika. Naomba sana Serikali Hospitali iweze kukamilika ikiwemo majengo yako na jengo la ghorofa 4"

"Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Godwin Mollel mmeshafika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida na mmeshaiona. Wananchi wa Mkoa wa Singida wanateseka, wanalazimika kwenda umbali mrefu Mikoa mingine kwaajili ya kupata huduma za kibingwa lakini Hospitali hii ndiyo mkombozi kwa Mkoa wa Singida kupata huduma za kibingwa ambayo inakabiliwa na uhaba wa watumishi 290 na vifaa tiba. Naomba Hospitali iangaliwe kwa jicho la pekee maana imeachwa kwa muda mrefu sana"

"Naipongeza Serikali kwa kuendelea kuajiri wahudumu wa Afya katika ngazi ya Jamii lakini naiomba Serikali iharakishe mchakato kwasababu wahudumu wanawasaidia wanawake wajawazito kujua siku zao za kujifungua, wasiweze kujifungulia nyumbani au kujifungua njiani, kutambua vidokezo hatari na kupata haraka matibabu na Mkoa wa Singida upate wahudumu ngazi ya Afya"

"Nimefurahishwa na hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya kuwa Kipaumbele cha kwanza kwa Wizara ya Afya ni kutoa huduma za kinga, naomba Waziri katika jambo hili tujikite kwa miguu miwili ili kuweka kinga zaidi badala ya tiba kwasababu tunaona kuna mrundikano mkubwa katika Hospitali zetu maana hatujasisitiza jambo la kinga, tumejikita zaidi katika tiba"

sddefaultlopiuyt.jpg
 
Back
Top Bottom