Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

RIP Jeremeah Sumari, nakukumbuka kwa majibu yako ya EPA bugeni kuwa DK Slaa utafute kitu kingeni cha kuuliza. Nayakumbuka kwa sababu sijawahi kuona majibu kama yale yakitolewa bungeni na serikali kwa jambo muhimu kwa taifa, ila wewe uliweza, RIP
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Dk Slaa: Kwa nini sikumsalimia JK [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 19 January 2012 20:42 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Fredy Azzah
KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete kutokana na Jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo Dk Slaa alisisitiza kuwa, kwa upande wake, kwenye msiba siyo sehemu ya kwenda kwa ajili ya kusalimiana na watu ama kurekebisha mambo yaliyoharibika bali ni sehemu ya kumwombea marehemu.

"Siyo hulka ya Dk Slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu," alisema Dk Slaa alipozungumza kwa njia ya simu jana.

Alifafanua kuwa, katika eneo la makaburi kulikuwa na mabanda matano ambayo yalipangwa kwa ajili ya Askofu, Rais, Viongozi wa vyama vya siasa, mwili wa marehemu na familia na banda jingine lilikuwa la watu wengine waliohudhuria mazishi hayo.
"Sasa kutoka alipokuwa amekaa Rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia Rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa," alisema Dk Slaa. Alisema alikuwa mtu wa kwanza kufika makaburini kwa lengo la kuangalia jinsi kaburi la mbunge wa chama chake lilivyochimbwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa na watu wa usalama wa taifa.

Alisema kuwa, hata katika wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Regia Mtema, katika ukumbi wa Karejee, kulikuwa na utaratibu kama huo ambapo ilitengwa sehemu ya kukaa Makamu wa Rais, Spika wa Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Makamu wake na yeye Dk Slaa akawekewa sehemu yake kama Katibu wa Chama alichokuwa akikitumika marehemu.

"Mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, Dk Slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia Rais. Katika sehemu kama ile Rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa," alisema Dk Slaa:

"Msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa" alisisitiza Dk Slaa. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Dk Slaa alishindwa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika mazishi ya Regia Mtema yaliyofanyika kijijini kwao Ipangalala Morogoro juzi.Regia alifariki dunia Januari 14 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Ruvu mkoani Pwani.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
RIP J.Sumari,
Bwana aiweke Roho ya marehemu mahali pema peponi. Awafariji wanafamilia, ndugu na marafiki wote katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

RIP Mhe J. Sumari. Poleni sana familia.

Dr Slaa, tunataraji Mama yetu Josephine atatu-update wakati wa mazishi ya Mwanamapinduzi Sumari ... kama alivyofanya kwenye msiba wa R. Mtema.
 
Naomba matokeo ya ubunge Arumeru Mashariki 2010 nifanye tathimini kidogo tafadhari

[TABLE="width: 515"]
[TR]
[TD]S/N[/TD]
[TD]Candidate[/TD]
[TD]Political party[/TD]
[TD] Votes[/TD]
[TD]Percentage [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]1[/TD]
[TD]SUMARI JEREMIAH SOLOMON[/TD]
[TD]CCM[/TD]
[TD="align: right"]34,661[/TD]
[TD="align: right"]62.23[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]2[/TD]
[TD]JOSHUA SAMWEL NASARI[/TD]
[TD]CHADEMA[/TD]
[TD="align: right"]19,123[/TD]
[TD="align: right"]34.33[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]3[/TD]
[TD]JOHN YESAYA PALLANGYO[/TD]
[TD]CUF[/TD]
[TD="align: right"]265[/TD]
[TD="align: right"]0.48[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]4[/TD]
[TD]LINDA PENIELI BANA[/TD]
[TD]JAHAZI ASILIA[/TD]
[TD="align: right"]176[/TD]
[TD="align: right"]0.32[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]5[/TD]
[TD]FANUEL GABRIEL PALLANGYO[/TD]
[TD]TLP[/TD]
[TD="align: right"]88[/TD]
[TD="align: right"]0.16[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: right"]6[/TD]
[TD]CHARLES MOSES MSUYA[/TD]
[TD]UPDP[/TD]
[TD="align: right"]88[/TD]
[TD="align: right"]0.16[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]SPOILT VOTES [/TD]
[TD][/TD]
[TD] 1, 297[/TD]
[TD="align: right"]2.33[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD="align: right"]54,401[/TD]
[TD="align: right"]100[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kwa wale wataalam wa kushupalia kuipa coverage na priority misiba ya watu, haya sasa mmepata wa kwenu. Kazi kwenu..
 
baada ya tabu na shida nyingi, nenda kapumzika ndugu yetu Jerry Sumari..
Lakini imeandikwa....
HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA............
VILEVILE MUNGU HAFURAHII VIFO VYA WACHAKACHUAJI KAMA...............
 
taratibu za mazishi zikoje?.mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
[h=3]spika makinda aungana na familia ya marehemu naibu waziri sumari[/h]on Friday, January 20, 2012
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia jana Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa Picha na Owen David

0 comments

[TD="align: center"]Reactions:: [/TD]




[h=3]makamu wa rais atoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu mh.naibu waziri jeremia sumari[/h]on Friday, January 20, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na watoto wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
 
Naamka asubuhi saa moja majira ya huku (takribani saa nane za mchana Tanzania). Kama ilivyo ada kila nikiwa nje ya TZ nikiamka cha kwanza huwa ni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya nyumbani ili kujua kinachojiri. Sikuamini nilichokiona kwenye ukurasa wa facebook na kwenye mtandao maarufu wa Jamii forums, eti ya kuwa Mh. Jeremiah Solomon Sumari, Mbunge wangu wa Arumeru Mashariki amefariki dunia.

Ilinilazimu kumpigia rafiki yangu wa karibu Mh. Godbless Lema (mb) ili anithibitishie habari hizi kwa kuwa na yeye ni mbunge na nafahamu yupo Darkwa ajili ya vikao vya kamati za bunge. Ndipo alipoithibitishia kuwa Spika wa Bunge amewatangazia wabunge kuondeka kwa mwenzao. Kwa kweli ni majonzi makubwa, pamoja na kwamba tulitofautiana kiitikadi lakini still tulikuwa marafiki na mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa nilimpa hongera though siku-sign matokeo. Mara ya mwisho tulikutana Dodoma hotel, akiwa amepumzika akijisomea kitabu. Kwakweli afya yake haikuwa nzuri sana na aliniambia "Nassari afya yangu ikitengemaa nitakupigia simu, kuna mambo ya kuzungumza" hayo ndio maneno ya mwisho niliyoyasikia kutoka kwake.

Hon. Sumari, umefanya mengi kiasi cha uwezo wako kwa wana-Meru na Taifa hili na kwa ujumla wake. Yale ambayo hukuweza kwa sababu moja ama nyingine, atakayekupokea kijiti ataendeleza mbio. Nimelazimika kubadilisha tiketi yangu, nilipaswa kurudi nyumbani TZ wiki mbili zijazo lakini imenipasa kurudi sasa kukusindikiza. Hii ni kwa kuuthamini mchango wako mkubwa kwa Jimbo langu la Armeru Mashariki na Taifa langu la Tanzania.

Natoa pole nyingi kwa Wanafamilia, na Wananchi wote wa Meru. Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu. Upumzike kwa Amani Mh. Sumari.


Joshua S. Nassari

Bwn Nassari ni bora ukawepo kwenye mazishi na msiba wa Mhs Sumari, maana huu ni mwanzo wa mapambano kwa upya kama ulivyo kusudia toka mwanzo!!!!!!!! Aluta Continua, Mapambano ndio bado yanaendelea!!!!!!!!!!

 
Poleni wanafamilia ya JS na Watanzania wenzangu. Rest in Peace J. Sumari
 
Ayaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! kumbe alikuwa anaongoza jimbo la Arumeru Mashariki kutokea Dar Es Salaam!

Huo ni ugonjwa unaowatafuna wabunge wengi. Cha ajabu ni kwamba wapiga kura nao wameridhia, vinginevyo wangeshawafurusha siku nyingi.
 
Back
Top Bottom