Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Naamka asubuhi saa moja majira ya huku (takribani saa nane za mchana Tanzania). Kama ilivyo ada kila nikiwa nje ya TZ nikiamka cha kwanza huwa ni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya nyumbani ili kujua kinachojiri. Sikuamini nilichokiona kwenye ukurasa wa facebook na kwenye mtandao maarufu wa Jamii forums, eti ya kuwa Mh. Jeremiah Solomon Sumari, Mbunge wangu wa Arumeru Mashariki amefariki dunia.

Ilinilazimu kumpigia rafiki yangu wa karibu Mh. Godbless Lema (mb) ili anithibitishie habari hizi kwa kuwa na yeye ni mbunge na nafahamu yupo Darkwa ajili ya vikao vya kamati za bunge. Ndipo alipoithibitishia kuwa Spika wa Bunge amewatangazia wabunge kuondeka kwa mwenzao. Kwa kweli ni majonzi makubwa, pamoja na kwamba tulitofautiana kiitikadi lakini still tulikuwa marafiki na mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa nilimpa hongera though siku-sign matokeo. Mara ya mwisho tulikutana Dodoma hotel, akiwa amepumzika akijisomea kitabu. Kwakweli afya yake haikuwa nzuri sana na aliniambia "Nassari afya yangu ikitengemaa nitakupigia simu, kuna mambo ya kuzungumza" hayo ndio maneno ya mwisho niliyoyasikia kutoka kwake.

Hon. Sumari, umefanya mengi kiasi cha uwezo wako kwa wana-Meru na Taifa hili na kwa ujumla wake. Yale ambayo hukuweza kwa sababu moja ama nyingine, atakayekupokea kijiti ataendeleza mbio. Nimelazimika kubadilisha tiketi yangu, nilipaswa kurudi nyumbani TZ wiki mbili zijazo lakini imenipasa kurudi sasa kukusindikiza. Hii ni kwa kuuthamini mchango wako mkubwa kwa Jimbo langu la Armeru Mashariki na Taifa langu la Tanzania.

Natoa pole nyingi kwa Wanafamilia, na Wananchi wote wa Meru. Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu. Upumzike kwa Amani Mh. Sumari.


Joshua S. Nassari

 
Maneno ya busara sana toka kwa kijana Nassari.
Litakuwa jambo jema sana kama utakuwepo wakati wa kuuaga na kuupumzisha mwili wa mh. Sumari.
 
Nimejaribu kukupigia simu Joshua nilipopata habari hizi za kusikitisha kuhusu Mhe. Sumari, Mbunge wetu. Ametaabika kwa siku nyingi na Mwenyezi Mungu amempumzisha. Roho ya marehemu ikae mahala pema milele. Amen.

Sikukumbuka kwamba wewe uko abroad sasa. Ni lini utarudi? Tunakutegemea mapema ukachukue jukumu la kuwakilisha jimbo letu.
 
Hili Jimbo ni la Chadema, maana kama tukisema uchaguzi uende kwa haki bila CCM kuiba kura (kama kawaida yao) Chadema tunashinda.

Mimi natoa ushauri kwa Mheshimiwa DR. (Phd) W. Slaa na board yake,ili kuondoa wizi wa kura na kuhongwa kwa wasimamizi wetu na chama cha magamba,ikibidi Mheshimiwa Dr. (Phd) W. Slaa na wabunge wako mgawane vituo vya uchaguzi ndio muwe wasimamizi wenyewe, maana hawatoweza kuiba mbele yenu, please please wekeni kila kitu pembeni na sisi tupo nyuma yenu kwa support, wabunge mkasimamie kuhesabu kwa kura huko, no wizi.

Tunaenda kuizika Arumeru pamoja a Mheshimiwa Jumatatu.

People's power
 
mbona sielewi kuna mbunge mwingine ameugaa dunia?
 
watu wanahuzuni ya msiba chadema wanafikiria uchaguzi.heri basi huyo nasari kuliko nyie japo na ni cdm.
 
mjiandae na nyumba za watu kuanza kuchomwa motto na CCM kwa ajili ya kuipaka matope CDM. i hope watu
wa arumeru mashariki watawadharau na mbinu zao za kizamani.
 
Rest in peace mheshimiwa Sumari.

Maneno ya Busara sana mh. Nassari. Baada ya kumsindikiza jipangeni tuzibe ufa wa IGUNGA.

Am sure peoples power itashinda.
 
Nawashangaa sana Chadema! Mnashangilia kifo cha Sumari kwa ajili ya kutafuta jimbo kwa mtaji huu usiojali ubinadamu, mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi hawezi kuwapa jimbo kwa kukufuru. Hebu tusubiri, kwa nini tuandikie mate na wino upo ?
 
CCM inazikwa pamoja na sumari arumeru mashariki

Jamani huu ni msiba hebu wekeni kando tofauti zenu, si vema kuzungumza kauli kama hizi wakati ambao ni mgumu sana kwa baadhi ya watu wake wa karibu, kumbuka leo ni kwao kesho ni kwako.
 
Nawashangaa sana Chadema! Mnashangilia kifo cha Sumari kwa ajili ya kutafuta jimbo kwa mtaji huu usiojali ubinadamu, mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi hawezi kuwapa jimbo kwa kukufuru. Hebu tusubiri, kwa nini tuandikie mate na wino upo ?

CHADEMA wanakutesa sana? Si lazima uchangie. Kwenye misiba watu wanakuwa na jokes.
 
Nimejaribu kukupigia simu Joshua nilipopata habari hizi za kusikitisha kuhusu Mhe. Sumari, Mbunge wetu. Ametaabika kwa siku nyingi na Mwenyezi Mungu amempumzisha. Roho ya marehemu ikae mahala pema milele. Amen.

Sikukumbuka kwamba wewe uko abroad sasa. Ni lini utarudi? Tunakutegemea mapema ukachukue jukumu la kuwakilisha jimbo letu.

heshima yako mkuu "founder wa Chadema"
 
Back
Top Bottom