Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

RIP Mbunge Sumari.
Huyu ndo aliyeambiwa na Zitto kwamba katoa majibu ya 'Hovyo hovyo', enzi hizo akiwa naibu waziri wa Fedha, wakati wa awamu ya kwanza ya JK.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.
Amina
 
Ni MBUNGE. Ibara ya 68 ya KATIBA ya JMT inasema hivo. Anaishia tu kumchagua Spika. Ili aendelee na kazi zingine za kibunge inabidi aape kwanza. Ibara ya 71(1) inaainisha mambo yatakayomfanya mtu asiendelee kuwa mbunge. La kuapa halimo.

Asante kwa kunijuza
 
Nawapa pole wale wote walioguswa na msiba huu kwa njia moja au nyingine, watoto wake, serikali, majirani na wakazi wa jimbo lake.

lakini msiba huu pia nadhani utufumbue macho katika mchakato wa katiba mpya (sio huu feki) utakapoanza, kuna mambo mengi sana ya kurekebishwa na kuwekwa

..............
SEHEMU YA PILI YA KATIBA, INAYOZUNGUMZIA WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA UCHAGUZI HEBU NINUKUU MACHACHE:-

Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge:-

66.1.b) Ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katika JM imethibitika rasmi kwamba mtu huyo ana UGIONJWA WA AKILI; au;

68. kila Mbunge atatakiwa kuapishwa ktk bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki ktk shughuli za bunge; lkn mbunge aweza kushiriki uchaguzi wa spika hata kabla hajaapishwa

69.(1) kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku 30 tangu aapishwe kushika madaraka kama mbunge kuwasilisha kwa spika nakala 2 za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya (d) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67.

71.(1) Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake ktk bunge litakapotekea lolote ktk mambo yafuatayo:-
a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, km asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii;
b) ikiwa mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
c) ikiwa mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya mikutano ya bunge 3 mfululizo bila ruhusa ya spika;
d) ikiwa amethibitika kwamba amevunja masharti ya sheria ya maadili ya viongozi wa uma;
e) ikiwa Mbunge Ataacha kuwa Mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge;
f) iwapo mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa makamu wa rais;
g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rtasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge

Lakini iwapo mbunge hatakoma kuwa mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au KUFARIKI mapema zaidi; basi mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama mbunge mpaka wakati wa bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, BILA KUATHIRI HAKI NA STAHILI ZINAZOTOKANA NA UBUNGE WAKE.

.........
 
pole kwa wafiwa Mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki kigumu.
R.I.P mh! Jeremia Sumari.
 
poleni sana familia ya JS.
Ajira hiyoooooooo.kwa wanasiasa na ukizingatia posho imeongezwa ya IGUNGA yanarudi.E MUNGU TUEPUSHE
 
RIP mbunge.....misiba kama hii ni reminders kubwa sana kwa wale viongozi waovu kwa raia wao wanaofikiri wataishi milele.....wangejua kufa kupo hata kama una kila kitu hakika wangewatumikia vema raia wao......misiba hii ni angalizo kubwa kwa wabadhirifu na wezi wa mali za maskini wa tz......wote tutakufa siku moja.....usipokufa kwa ajali utakufa kwa maradhi(e.g cancer au kisukari au ugonjwa wa moyo au hata usingizini ukiwa umelala)....hivyo tujiandae kwa kutenda mema kwa wengine ili hata tukifa tukumbukwe........God Bless!
 
Nawapa pole wale wote walioguswa na msiba huu kwa njia moja au nyingine, watoto wake, serikali, majirani na wakazi wa jimbo lake.

lakini msiba huu pia nadhani utufumbue macho katika mchakato wa katiba mpya (sio huu feki) utakapoanza, kuna mambo mengi sana ya kurekebishwa na kuwekwa

..............
SEHEMU YA PILI YA KATIBA, INAYOZUNGUMZIA WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA UCHAGUZI HEBU NINUKUU MACHACHE:-

Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge:-

66.1.b) Ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katika JM imethibitika rasmi kwamba mtu huyo ana UGIONJWA WA AKILI; au;

68. kila Mbunge atatakiwa kuapishwa ktk bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki ktk shughuli za bunge; lkn mbunge aweza kushiriki uchaguzi wa spika hata kabla hajaapishwa

69.(1) kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku 30 tangu aapishwe kushika madaraka kama mbunge kuwasilisha kwa spika nakala 2 za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya (d) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67.

71.(1) Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake ktk bunge litakapotekea lolote ktk mambo yafuatayo:-
a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, km asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii;
b) ikiwa mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
c) ikiwa mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya mikutano ya bunge 3 mfululizo bila ruhusa ya spika;
d) ikiwa amethibitika kwamba amevunja masharti ya sheria ya maadili ya viongozi wa uma;
e) ikiwa Mbunge Ataacha kuwa Mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge;
f) iwapo mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa makamu wa rais;
g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rtasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge

Lakini iwapo mbunge hatakoma kuwa mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au KUFARIKI mapema zaidi; basi mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama mbunge mpaka wakati wa bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, BILA KUATHIRI HAKI NA STAHILI ZINAZOTOKANA NA UBUNGE WAKE.

.........
Swali langu ni kifungu 71(1)(e) kinavyotumiwa sasa na vyama vyetu vya SIASA ni sahihi? Kinachosemwa hapa ni Mbunge kuacha uanachama sio kuachishwa au kufukuzwa kama inavyofanyika. Mahakama zetu zitupatie tafsiri sahihi ya kifungu hiki.
 
Hivi marehemu ana uhusiano wowote na akina Nancy&Nakaaya Sumari au nina majina ya ukoo yanafanana tu?Baada ya jibu,ndiyo nitakuwa na nafasi ya kusema kitu zaidi ya hiki.
 
Kama alitenda MEMA atalipwa MEMA kama alitenda Mabaya atalipwa Mabaya! Amen

@ Duble Chris

Samahani Nje ya mada kidogo:

frustration is given by expectation divide by
outcome
ie
frustration = expectation/outcome

R.I.P. Mzee Sumari
Tunatarajia upendo ulioonyeshwa na wana ccm kwenye mazishi ya dada Regia tutauona kwa wanachedema pia kwenye msiba huu!

walichofanya ccm ni kujaribu kujikweza juu kama sehemu ya promo ya chama chao kinachokufa! kama ulimsikiliza Wahasira sorry Wasira utanielewa, Mimi nawaambia pimeni ushiriki wa wananchi waombolezaji kwenye msiba mtajua, wakimuombolezea kwa kurarua nguo, kujipaka majivu na kujivika magunia mjue walimchagua, ukiona waombolezaji wanauliza wamechinjwa ng'ombe wangapi ujue alikuwa mbunge wa makame na kiravu, yote kwa yote, apumzike kwa amani tutamkumbuka kwa mema yake.
 
Kila nafsi itaonja mauti, pumzika kwa amani mpendwa.....Mwenyezi Mungu akuangazie mwanga wa milele!!! AMINA
 
Back
Top Bottom