Mbunge Condester Sichalwe Aibana Wizara ya Maji Kupeleka Visima Shule za Sekondari 2 Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE CONDENSTER SICHALWE AIBANA WIZARA YA MAJI KUHUSU VISIMA VYA MAJI SHULE ZA SEKONDARI MOMBA

"Tarehe 12 Juni, 2023 niliuliza swali la nyongeza Bungeni kuhusu changamoto tumeipata kwenye Jimbo la Momba kuhusiana na Maji. Wanafunzi katika Shule mbili tofauti wamepoteza maisha, Shule ya Sekondari Momba na Shule ya Sekondari Kamsamba kwa kutumbukia mtoni kwaajili ya kwenda kutafuta Maji kwa mwendo mrefu" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Niliuliza swali la nyongeza Bungeni na Wizara ya Maji wakanijibu kwamba wangeweza kufanyia kazi jambo hili maana niliomba Kisima cha dharura ili kuweza kunusuru maisha ya wanafunzi hawa" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wizara ya Maji walisema wangeweza kutuchimbia Kisima au kama kuna Kisima cha Jirani kuongeza urefu (Extension) ili Maji yaweze kwenda kwenye Shule hizo. Cha kusikitisha tarehe 23 Juni, 2023 niliwasiliana na Meneja wa RUWASA na Meneja wa Wilaya hawana taarifa yoyote ya dharura kuhusu jambo hili" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Sisi watu wa Jimbo la Momba tumejisikia unyonge sana na kuona kwamba Wizara ya Maji walituhadaa baada ya kusema jambo hili wangelichukua kwa dharura. Je, sisi wananchi wa Momba na watoto kwenye hizo Sekondari tutaendelea kufa kwaajili ya kwenda kufuata Maji Mtoni na hata pale tulipoomba tupate Visima vya dharura ili kuwasaidia wanafunzi!" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Mhe. Condester Sichalwe katika maelezo yake amesema kuhusu vifo vya watoto wa shule kukosa Maji. Hapa simuoni Waziri wa Maji wala Naibu Waziri wa Maji. Naomba Waziri wa Nchi ulichukue hili maana linahusisha vifo vya wanafunzi" - Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Maadam jambo limehusisha vifo vya wanafunzi ni muhimu Wizara ya Maji ichukue hatua ili hawa wanafunzi tuwaepushe na madhira ambayo yamewapata na upo uwezekano wakayapata hata hawa ambao wapo kama hiyo kadhia itaendelea" - Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Serikali imefanya hatua kubwa sana kwenye eneo la Maji, ile mitambo iliyonunuliwa kwaajili ya kuchimba Maji imepelekwa kila mkoa, kama uwezekano upo eneo hilo lipelekewe hiyoo mitambo ikachimbe Maji au Serikali ichukue hatua mbalimbali kuzinusuru hizi Shule mbili watoto waweze kupata huduma" - Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 
Back
Top Bottom