Momba: DG RUWASA Afika Jimbo la Momba Kutatua Kero ya Ukosefu wa Maji Kata ya Ndalambo na Msangano

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MOMBA: DG RUWASA AFIKA JIMBO LA MOMBA KUTATUA KERO YA UKOSEFU WA MAJI

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo amesema Wastani wa upatikanaji wa maji safi na salama nchini ni asilimia 79.7 lakini kwa Jimbo la Momba Wastani wa upatikanaji wa maji safi na salama ni sawa na asilimia 51, hivyo Momba bado iko chini sana katika viwango vya upatikanaji wa maji

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo leo tarehe 08 Disemba, 2024 amefika Jimbo la Momba katika Kata ya Ndalambo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Sichalwe kwa lengo la kutembelea maeneo yenye changamoto ya Maji na kuyatatua.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 2 Februari, 2024 akiwa Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Condester Sichalwe alisimama Bungeni na kuonyesha video kwa Spika wa Bunge zinazoonyesha wananchi wakichota maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu huku wakienda kuyatumia kwa matumizi ya binadamu.

Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ndalambo, Mhe. Condester Sichalwe amesema kazi yake ni kutatua changamoto za wananchi ikiwemo suala la Maji na hivyo atasimama kidete kuhakikisha wananchi wanapata Maji ya kutosha yaliyo Safi na Salama

Mhe. Condester Sichalwe ameomba Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA kuzungumza na kuwasikiliza wananchi maoni yao na kisha atembelee maeneo korofi ambayo wananchi bado wana shida ya Maji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo amesema ni kweli Momba bado haijafikia viwango vizuri vya upatikanaji wa maji safi na salama nchini na ndiyo maana amefika katika maeneo hayo kuwasikiliza maoni yao na kuona namna ya kuzitatua changamoto zilizopo

Eng. Clement Kivegalo amesema kuwa Serikali imeshatoa mashine kubwa za kuchimba miradi mikubwa ya visima vya maji ambayo yatasambazwa kwa wananchi wote ili wapate maji safi na salama.

Eng. Clement Kivegalo amesema ataongea na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso na Katibu Mkuu Wizara ya Maji ili kutenga fedha za miradi ya Maji inayotakiwa kutekelezwa ikiwemo mradi mkubwa wa Maji unaokuja Ndalambo kutatua changamoto ya Maji.

Wananchi kwa upande wao wamesema Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe anajitahidi sana kutatua changamoto ikiwemo kuwaleta Wataalam wa Serikali kama REA, TARURA, RUWASA, Kilimo na Mifugo ila changamoto ni watendaji wa Serikali wakiahidi hawatekelezi majukumu yao ya kutekeleza miradi kwa wakati.

Akiwa Kijiji cha Nakawale, Eng. Clement Kivegalo amesema kuwa ndani ya miezi miwili mpaka kufikia tarehe 10 Aprili, 2024 visima vya maji ya dharura vitakuwa vimechimbuliwa kwa matumizi ili kuondoa adha ya wanawake kutumia masaa zaidi ya sita kufuata maji.

Eng. Clement Kivegalo amesema Mradi mkubwa wa Maji tayari ulishamalizika tangu tarehe 01 Agosti, 2023 na kinachosubiliwa sasa ni tathmini ya maabara ili kuona kama maji yanafaa kwa matumizi ya binadamu, Kilimo na Mifugo.

Mwisho, Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo na Condester Sichalwe katika Jimbo la Momba walitembelea na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Ndalambo (Kijiji cha Ipumpila, Mengo), Kata ya Nakawale (Kijiji cha Nakawale na Nyenjele
), Kata ya Muyunga (Kijiji cha Mpui na Miyunga) na Kata ya Msangano Kijiji cha Msangano.
 

Attachments

  • IMG_6571.JPG
    IMG_6571.JPG
    1 MB · Views: 6
  • IMG_6590.JPG
    IMG_6590.JPG
    962 KB · Views: 3
  • IMG_6601.JPG
    IMG_6601.JPG
    664.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom