Mbunge Condester na DG RUWASA, Kivegalo Wafika Chilulumo, Ivuna na Kamsamba Kutatua Changamoto ya Ukosefu wa Maji Vijijini Jimboni Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE CONDESTER NA DG RUWASA ENG. KIVEGALO WAFIKA CHILULUMO, IVUNA NA KAMSAMBA KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MAJI VIJIJINI, JIMBONI MOMBA

Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Sichalwe leo tarehe 09 Disemba, 2024 ameendelea na ziara akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe katika Vijiji vya Chilulumo, Ivuna na Kamsamba kwa lengo la kutatua changamoto ya Maji.

Eng. Clement Kivegalo amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imenunua mitambo 25 ya kuchimba visima vya maji ambapo mtambo mmoja upo Momba ila ataongeza Mtambo mwingine ili kasi ya kazi iendelee.

Condester Sichalwe amesema kuwa Agosti 2023, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipofika Kijiji cha Muungano Kata ya Kamsamba alitoa Shilingi Milioni 500 ambazo zinathibitika kuwa zimeshafika lakini mpaka sasa zimefika Milioni 300+ ila zaidi ya Milioni 100 hazijafika.

Mhe. Condester Sichalwe amekemea vikali watu wanaopotosha jamii kupitia Mitandao ya kijamii wakisema kuwa ndani ya Jimbo la Momba hakuna Changamoto ya ukosefu wa maji na badala yake wamuachie yeye Mwakilishi wa wananchi Bungeni aendelee kuwasemea ili kutatua changamoto zilizopo

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo akiwa Kijiji cha Msangano Kata ya Kamsamba amesema amejionea uhalisia wa Chang zilizopo na kuahidi ndani ya miezi miwili ijayo wananchi watapata maji safi na salama.

Eng. Clement Kivegalo amesema RUWASA itachimba visima vya maji kwa dharura iliyopo ili wananchi waweze kutumia maji safi na salama wakati Suluhisho la kudumu likifanyiwa kazi kwa kuleta miradi mikubwa ya maji.

Jimbo la Momba, Kata ya Ivuna imepakana na Ziwa Rukwa ambalo lina chanzo cha maji cha kudumu ambapo Serikali inaweza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuvuta maji, kuyachuja na kuyasafisha kwa mitambo Maalum na wananchi wote wa Jimbo la Momba watapata maji safi na salama ya kutosha.

Condester Sichalwe na Eng. Clement Kivegalo wameambatana mpaka kwenye visima vyenye maji machafu wanayotumia wananchi wa Kata ya Ivuna ambapo maji hayo si safi na salama na hayafai kwa matumizi ya kawaida ya binadamu.

Diwani wa Kata ya Ivuna, Erick Mkamba amesema Kata ya Ivuna ina wakazi zaidi wa 27,000, Vijiji 5 na Vitongoji 22 ila ni Kijiji kimoja tu chenye maji na Vijiji 20 havina Maji kwani tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 Vijiji 20 havipata maji ya bomba.

Eng. Clement Kivegalo amesema na kuahidi wananchi wa Kata ya Ivuna kufanyia kazi changamoto hizo kwa kuchimba visima vya maji safi na salama vya kutosha na kuleta suluhisho la kudumu la maji safi na salama kwa wananchi
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.42.jpeg
    110.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Video 2024-02-09 at 23.09.52.mp4
    9.6 MB
  • WhatsApp Video 2024-02-09 at 22.35.31.mp4
    4.4 MB
  • WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.49.jpeg
    189.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.45(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.45(2).jpeg
    87.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.45.jpeg
    86.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.52(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-09 at 22.28.52(1).jpeg
    101.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom