Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
622
1,000
Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya Wabunge wamevaa mavazi yasiyo na maadili.

Spika baada ya kumuamrisha kuondoka Bungeni pia aliwaambia askari wa Bunge, kuanzia sasa mbunge yeyote atakaevaa mavazi yasiyo na Staha na kinyume na kanuni waishie getini. Sakata hilo lilianza kwa mbunge mwenzake kuomba muongozo wa spika akimtolea mfano kama mbunge aliyevaa mavazi yasiyo na staha.


1622547729773.png

1622547335484.png
1622547930355.png

Mbunge.jpg
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,242
2,000
Bunge katika mwendelezo wa utawala Dume! Mwanamke ana uhuru wa kuvaa chochote anachokipenda kwa siku hiyo na wanaume wasitafsiri hii kuwa she need sex!

Kinachotakiwa bungeni ni madini kutoka kwa Mh. Mbunge sio kavaa nini, pls my speaker tembelea bunge la SA uone, wabunge pale wengine wanavaa maovaroli na wengine kama domestic worker na kila kitu kipo safi, haya masheria ya kipuuzi futilia mbali na unyanyasaji ndani yake.
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,361
2,000
Bunge katika mwendelezo wa utawala Dume!mwanamke ana uhuru wa kuvaa chochote anachokioenda kwa siku hiyo na wanaume wasitafsiri hii kuwa she need sex!kinachotakiwa bungeni ni madini kutoka kwa Mh.Mbunge sio kavaa nini,pls my speaker tembelea bunge la SA uone,wabunge pale wengine wanavaa maovaroli na wengine kama domestic worker na kila kitu kipo safi,haya masheria ya kipuuzi futilia mbali na unyanyasaji ndani yake.
Kama kuna kanuni kandamizi, zibadilishwe sio zidharauliwe. Hata wanaume wamewahi kutolewa.

Screenshot_20210601-105907_Chrome.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom