Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,795
2,000
Sakata la kutolewa nje kwa mbunge wa Momba, Condester Sichwale (CCM) kuhusu mavazi, limeibuka tena leo jioni katika kikao cha Bunge baada ya wabunge wanawake kutaka aombwe radhi na aliyetoa hoja.

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).

Katika kikao cha leo jioni wabunge Jacqueline Ngonyani na Stella Manyanya waliomba mwongozo wa Spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Mapema leo Sichwale alitolewa nje kwa amri ya Spika baada ya Amar kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni 170 kuhusu mavazi ya staha.

Ngonyani amesema kilichotokea ni kwamba mbunge huyo alionewa kwani alikuwa na vazi la staha ambalo halikuwa na shida lakini akasema huenda Spika hakuona.

"Mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu la wanawake wa CCM, ninapoona kuna uonevu lazima niseme na hili sikiungi mkono huyu mwanamke mwenzetu ameonewa,"amesema Ngonyani.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa uonevu wa namna hiyo haupaswi kuvumiliwa kwakuwa umemdhalilisha mbunge huyo na wapiga kura wake jimboni.

Kwa upande wake Manyanya amesema tangu asubuhi alikuwa anafuatilia kwenye mitandao na amebaini kuwa Sichwale hakuwa na vazi baya.

Hata hivyo Manyanya amesema haiwezekani wabunge vijana wavae mavazi kama wanayovaa wabunge wanawake watu wazima.

Amesema katika siku za karibuni limeibuka suala la kutoa lugha za kuwadhalilisha wabunge wanawake ndani ya ukumbi ambako wakati mwingine hutamkwa kiungo cha mwanamke halafu wengine wanafurahi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Akson amesema atatoa mwongozo baada ya kufuatilia jambo hilo.

1622614505118.png
 

chikambabatu

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
813
1,000
Sketi ikibana sio shida ila suluali ikibana ni shida, mupitie upya kanuni ya mavazi! Pia naona mavazi yote yaruhusiwe tu, cha msingi suluali isibane kwenye lisani au kwa mbele, spika afutilie ilo tu!
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
804
1,000
Ulikua uonevu na uzalilishaji mkubwa sana na usiovumilika, huyu mzee asilete sheria na maoni ya nyumbani kwake kwenye public, Huyu mzee lazıma ashitakiwe kwa uzalilishaji na spika amuombe razi huyu Mama na wanawake wote, kwani kitendo hiki na Katika chombo hiki ni kimezalilisha Wanawake wote, na huyu Mama hakuwa na kosa Nguo zake zilimsitiri vizuri bila shaka yeyote.
 

KIBIKIMUNU

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
250
250
Ningekuwa spika...ingawa siwezi kuwa spika...ningeamuru wote wanaoendeleza huu mjadala watoke nje kabisaaaa....hivi hakuna changamoto za wananchi wao majimboni mpaka hili liwe Jambo serious HIVI?
 

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
825
1,000
Ningekuwa spika...ingawa siwezi kuwa spika...ningeamuru wote wanaoendeleza huu mjadala watoke nje kabisaaaa....hivi hakuna changamoto za wananchi wao majimboni mpaka hili liwe Jambo serious HIVI?
Watu wavae vizuri. Mavazi ya heshima ni muhimu. Discipline inaanzia kwenye vitu vidogo sana. Huwezi beba jukumu la kuwakilisha watu zaidi ya laki tano afu unavaa skintight bungeni.
Discipline lazima iwepo asee.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,544
2,000
Walikuwa wapi wakati mjinga yule anatoa hoja? Kwa nini hawakuipinga? Ina maana hawakuona kuwa vazi ni la staha hadi sisi tuliposema hapa jamvini? Na wenyewe vichwa zero sawa tu na huyo mzee mtoa hoja. Anataka kijana avae dera!!!!

Yule mzee ni msikiti, hivyo alitaka huyo dada avae hijabu ndio aridhike. Ila bunge futuhi nalo lina vituko vyake acha tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom