Bungeni Dodoma: Spika wa Bunge Job Ndugai, amvua Ubunge Tundu Lissu(CHADEMA) Mbunge wa Singida Mashariki kwa kosa la utoro

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Just now from Dodoma,
Spika wa Bunge, amelitangaza jimbo la Singida Mashariki la mbunge Tundu Lissu liko wazi na tayari ameisha mwandikia Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi, kumtaarifu kuhusu uamuzi huo.

Spika ametoa sababu mbili
1. Kutotoa taarifa rasmi ya maendeleo yake huku akionekana huku na kule.

2. Hakujaza fomu za maadili ya viongozi za Tume ya maadili, hivyo kupoteza sifa za kuwa Mbunge.

My Take
Japo hii itaonekana kama this is adding an insult to an injury, lakini kwanza tujifunze kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, ukikiuka, you go hata kama ndio kwanza umetoka ICU!.
Pili viongozi wetu wajifunze kutenda haki na sio tuu kufuata sheria, taratibu na kanuni!. Tundu Lissu amejeruhiwa kwa shambulio la risasi wakati akiwa Bungeni!. Spika anajua, Watanzania tunajua na Dunia inajua!. Kumvua ubunge mtu kama huyu, sio kumtendea haki!. Kiongozi usipotenda haki, karma itamtendea haki kwa kiongozi huyo kuadhibiwa na karma na Lissu kufidiwa na karma.

P

======

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema amemuandikia barua mwenyekiti wa NEC kumtaarifu kuwa kiti cha ubunge jimbo la Singida Mashariki kipo wazi kutokana na mbunge Tundu Lissu (Chadema) kutokuwepo bungeni bila taarifa na kutokujaza fomu ya tamko ya mali na madeni.

"Nimemwandikia Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kuwa Kiti cha Ubunge wa Singida Mashariki ambacho Mbunge wake ni Tundu Lissu kipo wazi".Spika Ndugai

Lissu aliyekuwa pia rais wa Chama cha Wanasheria (TLS) alipigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mnamo tarehe 7 mwezi Septemba 2017 baada ya kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma.

Alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi.

Alipokuwa akizungumza na wanahabari Nairobi kwa mara ya kwanza, Bw Lissu alisema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma walikuwa na uhusiano na serikali.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana.

"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawakilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," alisema Lissu.

Serikali ilikanusha tuhuma hizo.

Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mwezi Novemba mwaka 2017 alipokuwa ziarani Nairobi.

Zaidi, soma;




 
Maagizo kutoka juu yametua mjengoni...

Muhimili mkuu umetaradadi mbele ya mhimili wa "kupongezana"


Risasi zilishindwa ila kuna njia mbadala.... Ila na wewe mjomba Tundu ulishindwaje kumwandikia spika kuwa hutaweza kuwa bungeni kwa kuwa umecharazwa risasi kadhaa? Hivi ukiwa ICU hujitambui unashindwa kweli kumwandikia spika??

Ugua pole na Karibu sana mtaani Tundu Antipas Lissu... huku kazi tu!

Naendelea kumwelewa sana Prof Assad... Kiukweli kabisa "dhaifu" ni neno la kawaida sana kwenye ukaguzi wa mahesabu... lakini kwingine huku ni matusi.
 
Hovyo kabisa!

Naposema hawa watu ni lazima waendelee kufanya makosa ili watanzania wengi zaidi wawakatae,makosa haya ndio makosa yenyewe.

Eleweni(naendelea kusistiza) Mungu kawanyima maarifa na busara ili waangamie(wajimalize wao wenyewe bila kujijua)

Huyu mkulu wa sasa ndio anaweza kuwa wa mwisho kutawala kutoka chama cha kijani.
 
Tunaomba data zaidi, hii ni muhimu, japokuwa Tundu Lissu sasa ni zaidi ya bunge. sema ni jitihada za kumzuia asizungumze. bungeni ni sehemu ya kuunguruma. lakini anaweza kuendelea kuunguruma kama alivyokuwa anafanya kabla
 
Aisee,kutoka kupigwa risasi na sasa kuvuliwa ubunge. Ni nini sababu za kumvua ubunge? Any way even this shall pass. Naamini wanasheria wa Lissu watafight kumrudishia ubunge wake. Hivi Mbunge wa Musoma mheshimiwa Mkono yupo wapi? Yeye kwa nini havuliwi ubunge?
 
Back
Top Bottom