Mbunge Aysharose Mattembe Aitaka Halmashauri ya Wilaya ya Singida Kuwa na Miradi ya Maendeleo Kuongeza Ukusanyaji Mapato

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe Asisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Singida inapaswa kuwa na Mradi ambao utasaidia katika Ukusanyaji wa mapato ili kuinua Uchumi wa Halmashauri hiyo.

Pia, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe Amesisitiza Watendaji wa Kata kushiriki Ipasavyo kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa umakini na Umahiri.

Hayo yamejiri Novemba 16, 2023 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani cha Robo ya Kwanza Julai - Septemba 2023 Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Singida Ilongero - Mwahango.

"Halmashauri yetu inahitaji watu Mahiri na makini kwa ajili ya Ukusanyaji wa Mapato ili kuweza kufikia Malengo yake. Nikuombe Mkurugenzi uwe na Taarifa Kamili ya idadi ya watendaji ambao tunawahitaji katika Halmashauri yetu kwasababu Vibali bado vinaendelea kutolewa hata kwenye Wilaya zingine pia Tumeona Wanaendelea kuajiri Watendaji. Nina imani kama tukipata Taarifa Kamili tutafanikiwa kuzifikisha Kwa waziri wa TAMISEMI ili na sisi tupate watendaji kwenye Maeneo yenye Upungufu wa Watendaji" - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe amesisitiza kama halmshauri ya wilaya ya Singida inapaswa kuwa Miradi mbalimbali ambayo itakuwa kama injini ya kuchochea kukuwa kwa uchumi na kuweza kupata Mapato katika Halmashauri hiyo.

"Ningependa Kusisitiza Kama Halmashauri tungepata Mradi ambao sasa utakuwa ni Injini ya kuweza kupata Mapato katika Halmashauri yetu. Kuna miradi mbalimbali ambayo sisi Wabunge tumeipigia kelele ikiwemo Mradi wa Soko ambao utajengwa Merya lakini pia ujenzi wa Stendi. Kwa hiyo ni lazima tujipange tujikite vizuri ili tuweze kupata Mradi ambao tutakuwa na Uhakika wa kukusanya Mapato" - Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe.

WhatsApp Image 2023-11-17 at 02.05.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 02.05.39(4).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 02.05.39(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 02.05.39(5).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 02.05.40(1).jpeg
 
Back
Top Bottom