Aysharose Mattembe Achangia Shilingi Milioni 10 Kununua Majiko ya Gesi kwa Wanawake wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,960
954

AYSHAROSE MATTEMBE ACHANGIA MILIONI 10 KUNUNUA MAJIKO YA GESI KWA WANAWAKE

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Aysharose Mattembe amefanikisha Semina kubwa ya mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira na Uwekezaji kwa wanawake wa UWT Mkoa wa Singida huku Akiwapatia Majiko ya Gesi yenye thamani ya Milioni10 na futari .

Hayo yamejiri tarehe 05 Aprili, 2023 ambapo Semina kubwa imefanyika katika Ukumbi wa RC Mission Singida Mjini Aprili 05,2023 mbunge huyo ameshirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Mattembe Golden Women Foundation (MGWF) pamoja na Taifa Gas Kutoka Kanda ya Kati na Mkoa wa Singida.

Wanawake wa UWT kutoka Wilaya za Ikungi, Singida Vijijini na Singida Mjini pamoja na Manyoni, Mkalama na Iramba wamenufaika na Semina hiyo huku wakisisitizwa kutunza Mazingira na kujitahidi kufanya uwekezaji Katika shughuli mbalimbali za kujiingizia Kipato ambapo semina hiyo imefunguliwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida, Ndugu Martha Kayaga.

Pia, Wanawake hao wamemshukuru sana Mbunge wao wa viti maalumu kutoka Mkoa wa Singida kwa kuwajali kwa kuwapa majiko ya gesi kwani majiko hayo watayatumia ili kuondokana na matumizi ya kuni pia matumizi ya mkaa kama chanzo cha nishati ambayo yanapelekea Uharibifu wa mazingira huku wakimuombea kwa Mungu kufuatia kuwapa Sadaka ya futari.

WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.33.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.33.01.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.33.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.33.02.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-06 at 14.33.04(2).jpeg
 
Back
Top Bottom