Mbunge Aysharose Mattembe: Karibuni Wana-Singida Katika Mapokezi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe anapenda kuwakaribisha Wananchi wote wa Mkoa wa Singida na Wilaya zake katika Mapokezi ya ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Singida itakayoanza tarehe 15-17 Oktoba, 2023.​

Ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Singida itaambatana na Sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwa Mkoa wa Singida tangu tarehe 15 Oktoba, 1963 zitakazofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mjini Singida, tarehe 16 Oktoba, 2023 kuanzia Saa Kamili Asubuhi

Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuzaliwa kwa Mkoa wa Singida (Tarehe 16 Oktoba, 1963) atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ni ziara ya kwanza ya kikazi ndani ya Mkoa wa Singida kwa Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani

Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2022-2023 katika Mkoa wa Singida ametoa fedha Shilingi Bilioni 9 zilizotumika kujenga Shule mpya 12, Madarasa, Ofisi za Walimu na Nyumba za Walimu

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan atakwenda Itigi kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Itigi kuelekea Mbeya. Pia, atakwenda Ikungi kuzindua Vituo Viwili vya Polisi vya Wilaya ya Ikungi na Wilaya ya Mkalama. Rais Samia atazindua Daraja la Bilioni 11 lililojengwa Mkalama.

WhatsApp Image 2023-10-14 at 16.05.51.jpeg
 
Attachments

  • AYSHAROSE MATTEMBE 1.jpg
    2.8 MB · Views: 7

View attachment 2782297
Hongera Sana
 
Back
Top Bottom