Njiku azindua mafunzo ya ujasiriamali Singida

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
Afisa Tarafa ya Ilongero mkoani Singida, Yahaya Njiku leo Novemba 10, 2023 amefungua Mafunzo ya Ujasiriamali Tarafa ya Ilongero yanayoendeshwa na Shirika la kiraia la Star Entrepreneur General kama sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais Dkt Samia ya kuwawezesha Wajasirimali na wafanyabiashara wadogo ili kukuza mnyororo wa thamani wa bidhaa wanazozalisha.

Aidha mafunzo hayo yatakayojikita kwenye fani za ubunifu wa utengenezaji keki za sherehe, tambi za mayai, lishe bora, Ufugaji wa kuku, sabuni aina zote, batiki aina zote pamoja usimamizi wa biashara na Masoko, yamedhaminiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe.

Wana Singida tunajivunia Njiku, Kiongozi Kijana mpambanaji, mnyenyekevu, sauti ya makundi yote.

KAZI IENDELEE!
IMG_20231110_215540_374.jpg
 
Back
Top Bottom