Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mwanasiasa,
Hapo umegonga msumari kwenye kichwa. Nimeona hivyo hivyo. Hivi sasa Tanzania ina crisis of leadership. Ni ahadi lukuki tu zinatolewa. Fedha zimechukuliwa bila bajeti kupelekwa mikoani ati kuanzisha ajira.

Zitaishia mifukoni mwa wajanja wachache. Lakini hatuzungumzii badala yake ni Chadema na viongozi wake ndiyo imekuwa mada.
 
Kichuguu.

Unachekesha sana mbona unaleta Udikteta wa chadema humu? unasema nisikuulize chochote wala nisikujibu huku ukijenga hoja, hapa hatupo Chadema kusiko na uhuru wa kuhoji.katika haki ndogo kabisa za binadamu ni kumpa nafasi ya kujibu au kuhoji ina maana Chadema wakiingia madarakani mtu akituhumiwa tu basi anawekwa ndani hana nafasi ya kujitetea?someni adminstrative law kuna kitu judicial review halafu tizama natural justice inasema nini?

Ufinyu wa akili yako.

Watu wanaposema Bush kachukua kazi ya baba yake haina maana kuwa alipotoka baba yake aliingia yeye,kwa akili zako za kichadema utasema NO alichukua baada ya Clinton.

kuna mifano mingi ya hilo nenda kwenye Taasisi mbalimbali hasa hizo za fedha hapa nyumbani utaona labda hazina kuna watu wengi wa kaskazini, jibu kuwa huko nyuma kulikuwa na mtu au watu toka maeneo hayo wameacha athari kwangu mimi ni athari mbaya, ukienda Bima, Nbc,jeshini na hata polisi ndio utakuta kuna misemo ya maeneo fulani ya kazi imeathiriwa na huo mfumo mbaya wa kupendeleana au kujaza watu wake mfano mtu anasema" harrow liafande" na huo msemo unakuta umetawala ktk kitengo fulani ni kuonyesha jinsi watu hao walivyomiliki eneo hilo. samahani Jasusi kama nimegusa,

Kichuguu.

Nimesema Mtei alimpa kazi Mbowe na yeye mwenyewe hajakanusha kwanini wewe uje kujibu wakati mwenyewe yupo hai na ametoa ahadi hiyo?, bahati ya mwenzio usi ilalie mlango wazi, unashangaa kupewa kazi na mke?, yote yanawezekana. hakuna principle yeyote inayosema mtu akikupa kazi hawezi kukupa mwanawe.

kukusaidia uelewa wako mdogo tizama suala la Mkapa kuwa rais wa Tanzania watu wengi wanasema na kuamini kuwa Marehemu mwalimu Nyerere alimsaidia kumpata hayo madaraka, na kuna wengi wanasema na kuamini kuwa Malecela na Lowassa walikosa nafasi za kuwa marais 1995 kwa mkono wa mwl. jee mwaka 1995 mwl Nyerere alikuwa rais wa Tanzania? au alikuwa Mwenyekiti wa chama? au alikuwa makamu mwenyekiti? au alikuwa katibu mkuu wa CCM?

na hakuna mahala kusikia watu wakisema aliyekuwa rais na mwenyekiti wa chama Alhaji Mwinyi alimsaidia Mkapa kupata nafasi ile, au kusikia Malecela ana kinyongo naye kwa kuikosa nafasi ile.

kumbuka hayo ni madaraka makubwa kabisa ktk nchi.
jee Mtei atashindwa kumpa kazi ya ukalani BOT bwana Mbowe?
Kichuguu sitakwenda mbali naona uoni wako mdogo sana.

Kakindo.
usiwe na jazba mweyekiti atakuja kujibu NINI WAPUKI.
 
Mwanasiasa.
Pole na kazi mheshimwa.
sijasema sehemu yeyote uko Southmpton naomba nioneshe.
 
MWANASIASA NA JASUSI.

Mmezidi uongo? nani alianzisha thread ya Tamko la chadema?ni nyinyi wenyewe sisi tulikuja kuchangia tu.hadi mliposema tuanzishe thread ya mbowe.
hata ukitiza hoja nyingi za msingi DR.WHO amekuwa akiuliza? tizama thread ya Richmond imenzishwa na Mbowe? no way ni DR.WHO.

sasa mwenyekiti wenu alipokuja humu hayo matatizo hayakuwepo? pia hamjafungwa au kuzuiwa msifungue thread ya matatizo ta umeme au ajira,

Nilichogundua mmetumwa na mwenyekiti kuja kuzima hizo hoja mwenye hawezi kujibu chochote kwani ni zero tu.

jana mmeingia kwa zamu, umeanza mwanasiasa ni kala na wewe sahani moja hadi ukakimbia, akajaza mzushi Jasusi nikakata zote,akaja quarz mchaga wa Hai nikafunua, akajaza kakindo nikafumua, akaja mount kichuguu nikakata zote, akaja mount kibo nikaua,akaja lunyungu nikamtoa baru,akaja mnyika nikazima,

MMETADHIMINI KAZI YA JANA MMEONA HAKUNA HOJA ya kupambana na mwanaume kama mimi.

sasa mnataka mjadala ufe ili kumuokoa baba yenu.
Kama hamuwezi kunijibu mimi chinga mbumbumbu mtaweza kuwajibu Watanzania/
 
Sasa hivi najiuliza kama kuna chama kingine kinaworth kura yangu Tanzania

maana hakuna aliyekuwa straight au anayekuja na straight answers lakini so far naamini pamoja na matatizo yaliopo CHADEMA wamejitahidi maana hao CUF wamingia mitini kabisaaa
 
nadhani its better kuja clean na suala hili liishe ilityuendelee na hilo jipya la UWANJA WA NDEGE ambalo litaifanya Richmond na IPTL kuwa skendo za kitoto
 
Mnyika.
mbona kimya?yaani Mkurugenzi mzima wa chama huna access za mtandao?chama unakiongoza vipi? tunasubiri majibu yako mheshimiwa.
 
Naam Mwanasiasa:

Hujajibu swali la msingi nililokuuliza mara mbili takriban:

Ulikuwa unajua kama Lucy Owenya na Grace Kihwelu wana mahusiano na Mzee Ndesamburo ya uzazi kabisa?

Kama ulijua kabla je huhisi kwamba hapa kuna walakini, hata kama wamechaguliwa kwa kura, is it fair kichama kinachotaka kuwa mbadala na CCM?

Kama ulikuwa hujui, nipe reaction yako sasa.


Naam leo naanza rasmi kudisect information nilizopewa na kujaribu kuanalyse kama CHADEMA ni biashara ya watu wa kaskazini au ni chama mbadala:

Data nilizopewa zipo biased i have to say manake zimechagua kipengele kimoja tu cha viongozi. Kwa mujibu wa tovuti ya CHADEMA, Viongozi wa kitaifa ni hawa wafuatao:

Freeman Aikaeli Mbowe [KILIMANJARO]
Mzee Saidi Mzee [visiwani]
Wilbroad Slaa [Karatu- Arusha]
Shaibu Akwilombe [masasi lindi]
Himid Yusph-Pemba
Victoria Kimesera [KIteto manyara]


Hawa ndio viongozi wa kitaifa, you can see kuna viongozi sita, watatu wanatoka kaskazini:
Mbowe, Slaa, Kimesera [50% ya top team!!]

Kumbuka tanzania ina mikoa ishirini na sita, lakini viongozi watatu wakubwa wametoka tanzania north!!

WABUNGE:
Chadema imefanikiwa kupata viti kadhaa vya wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu na hivyo kufanikiwa kupata viti maalum, wafuatao ndio wabunge wa chadema:

SLAA[KARATU]
Maulidah Anna Komu -VITI MAALUM
SAID AMOUR ARFI [MPANDA]
CHACHA WANGWE [TARIME]
SUSAN LYIMO [VITI MAALUM]
NDESAMBURO [MOSHI MJINI]
HALIMA JAMES [VITI MAALUM]
MHONGA SAID [VITI MAALUM]
LUCY OWENYA [VITI MAALUM
ZITO KABWE [KIGOMA VIJIJINI]
GRACE KIHWELU [VITI MAALUM]

Unaweza kuona kuwa CHADEMA ingawa kimepata wabunge katika several locations in the country lakini wabunge wa kuteuliwa Owenya,Lyimo,Grace, wote ni kaskazini!!! Ukichanganya na Mzee Ndesamburo na Slaa ina maana wabunge watano kati ya kumi na moja wametoka kaskazini!! Hapo hatujamchanganya Mama Komu ambae anajidai mzanzibari mwenye asili ya uchaga na Mwanasiasa nisaidie Halima anatoka wapi.


Ukiwatoa Anna Komu na Halima James, unakuta kwamba wamebaki wabunge tisa na watano kati yao ni kaskazini, 55%!! ukiwachanganya na hao wawili unaona kwamba ni 45% wanatoka kaskazini!!

What is interesting to note here ni kuwa viti vya ubunge wamepata sehemu tofauti za nchi lakini kwa vile kuna maslahi ya mishahara minono nk basi wabunge wawili ukimchanganya na mzee Ndesamburo mwenyewe ni familia moja! Hivi ni viti vya kuteua, hivyo wangeweza kuvibalance lakini ndio hivyo kwa chama chenye domination na kaskazini....

Ukija kwenye Sekretarieti ya CHADEMA ambayo ina wajumbe 30 utakuta kumi na moja kati hao wanatoka kaskazini. Check for yourself:

http://www.chadema.net/uongozi/sekreta.php

hii ni about 36% of the total members of the secratariet

Katika mikoa ishirini na sita kuona wajumbe wakiwa mostly kutoka mikoa miwili mitatu wakishikilia nafasi nyeti na nyingi zenye ulaji inakupa shida kukiona hiki kama chama mbadala.

The analysis will continue.....
 
Guys,

This discussion is getting sweeter! Some facts and a lot of disinformation. As a said, leo nimekuja kumalizia kusoma viporo ili kesho nijibu.

Kama nilivyoahidi. Nimepiga simu Moshi na kuthibitisha kweli Mwenyekiti hakuwepo(alikuwepo na bado yupo Hull). Ujumbe uliwasilishwa na Grace Kiwelu kwa niaba.

Mwandishi aliwasilisha vibaya, nategemea baada ya kuelezwa madhara ya makosa yake ya kiuandishi ataitoa habari husika tena kwa usahihi.

Hivyo msiendelee kubishana katika hili.

Nitarejea kujibu hoja mbalimbali.........


JJ
 
Afadhali umeweka habari hii sawa bwana Mnyika manake niliweka mimi tarehe tuliyoambiwa mwenyekiti anarejea.

What is interesting ni kuwa kuna watu kama Mwanasiasa wao walipoona mwenyekiti anapigwa mawe wakaanza kutafuta jusitifications bila kuangalia kama taarifa ni kweli au la!!

Inashangaza hata hivyo kwa chama kinacho-operate as a team tena kwako Bwana Mnyika as frontbencher kutojua mwenyekiti yupo nchini au la mpaka upige simu!! unatakiwa kuwa tayari kutetea chama off the cuff na hivyo unahitaji up to date information kuhusu chama na mwenyekiti!

By the way hivi hakukuwa na mbunge mwingine wa kupeleka misaada hiyo mpaka aende Mzazi mwenzake Mbowe?!

Ni lazima Moshi?!! Mmepata jimbo mpanda na tarime msiyatelekeze.....
 
Tafiti,

Unaniingiza kwenye mjadala wakati nimepanga kuingia kesho.

1. Tunafanya kazi in team, nilijua kabisa yuko nje na nilisema hivyo katika majibu yangu ya awali. Lakini kwa teknolojia ya siku hizi ya ndege mtu anaweza kuja na ndege ghafla tu na kuondoka. Sasa nilitaka kuthibitisha kwa muktadha huo. Na ningeshangaa kama ingekuwa hivyo kwa kuwa itifaki ni kitu muhimu.

2. Mwanasiasa alizungumza kutokana na context, alingalia majira-ni kweli kwa baadhi sasa ni likizo. Hata Hull wataanza likizo hivi karibuni.

3. Hilo la Mbowe kuwa na mtoto na Kiwelu ndio nalisikia kwako. Kwa hiyo mpaka utakaponipa ushahidi wa kuthibitisha vinginevyo nakwambia kwa suala kama hilo halipo. Na kumbuka, nawafahamu wote Mbowe na Kiwelu!

'Tunayo haki ya kusema lakini tuwe na wajibu wa kusema mambo ambayo tunahakika nayo'

Kesho wapendwa
 
Umeuliza pia,

kwa nini Kilimanjaro na si Tarime au kwingineko:

Kwa viongozi, motive ya kutoa mchango huwa kati ya zifuatazo:

1. Umeona tatizo la msingi katika eneo fulani.( notice of need)

2. Unahusiana na eneo fulani(sense of community)

3. Umealikwa(invitation/application).

Ninavyofahamu ni kuwa KKKT waliwasilisha ombi. Kwa hiyo kama Tarime wakingewasilisha ombi lingefanyiwa kazi in its own merit.

Lakini, ninachoshangaa tafiti- hukuuliza swali kama hili Mbowe na wabunge walipochangia kanisa Ukonga, wala Mbowe na wabunge walipochangia Taifa star, wala Mbowe alipochangia shule maalum ya vijana inayojengwa chini ya Bakwata(waislamu) ama michango mengine kadha wa kadha kwa makundi mbalimbali.

As your name suggest, research then discuss

JJ
 
so far so good

Mnyika umefanya vizuri kuliweka sawa hili

I am waiting for your response in CHADEMA & CONSERVATIVE alliance thread
 
Dr WHO, hilo la uwanja wa ndege ni lipi tena?



Hilo kubwana mno na itabidi lifunguliwe mjadala unaojitegemea hivyo nitaufungua baadae kadri muda unavyozidi kwenda

OFF TOPIC:

Jamani mimi nimemjibu mama Marjorie Mbilinyi kule kwenye thread ya Salma kikwete lakini naona kimya hivi hao jamaa wa TAMWA wamepotelea wapi ningependa kuona michango ya akina mama vile vile
 
Mnyika

Very well answered manake ningeshangaa kama mwenyekiti amekuja nchini halafu wewe hujui!

Good points on misaada lakini mwanasiasa alirukia I have to say, likizo za academic institutions zinaanza wiki hii friday not before, hata hao HULL wanaanza on the 18th DECEMBER 2006 kama alivyoweka DRWHO....

Otherwise chapa kazi na tunakungojea kwa hamu kesho uje hapa kujibu hoja/maswali ya wengine... mimi yangu nashukuru nimejibiwa...

Ok unadai mbowe na lucy hawana mtoto, je unajua kama wana mahusiano ya karibu na ni mbowe alisababisha ndoa ya kwanza ya Grace kuvunjika?

Unafahamu kama Mzee Ndesamburo huyu Grace ni ex mkwewe na kwamba Lucy ni mtoto wake na wote hawa ni wabunge wa viti maalum kama hawapendelewa ni nini hii?!!
 
It gets more interesting here.......


Naam Mwanasiasa:

Data nilizopewa zipo biased i have to say manake zimechagua kipengele kimoja tu cha viongozi. Kwa mujibu wa tovuti ya CHADEMA, Viongozi wa kitaifa ni hawa wafuatao:

Freeman Aikaeli Mbowe [KILIMANJARO]
Mzee Saidi Mzee [visiwani]
Wilbroad Slaa [Karatu- Arusha]
Shaibu Akwilombe [masasi lindi]
Himid Yusph-Pemba
Victoria Kimesera [KIteto manyara]


Hawa ndio viongozi wa kitaifa, you can see kuna viongozi sita, watatu wanatoka kaskazini:
Mbowe, Slaa, Kimesera [50% ya top team!!]

Kumbuka tanzania ina mikoa ishirini na sita, lakini viongozi watatu wakubwa wametoka tanzania north!!

WABUNGE:
Chadema imefanikiwa kupata viti kadhaa vya wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu na hivyo kufanikiwa kupata viti maalum, wafuatao ndio wabunge wa chadema:

SLAA[KARATU]
Maulidah Anna Komu -VITI MAALUM
SAID AMOUR ARFI [MPANDA]
CHACHA WANGWE [TARIME]
SUSAN LYIMO [VITI MAALUM]
NDESAMBURO [MOSHI MJINI]
HALIMA JAMES [VITI MAALUM]
MHONGA SAID [VITI MAALUM]
LUCY OWENYA [VITI MAALUM
ZITO KABWE [KIGOMA VIJIJINI]
GRACE KIHWELU [VITI MAALUM]




halafu kuna hiii:


Unaweza kuona kuwa CHADEMA ingawa kimepata wabunge katika several locations in the country lakini wabunge wa kuteuliwa Owenya,Lyimo,Grace, wote ni kaskazini!!! Ukichanganya na Mzee Ndesamburo na Slaa ina maana wabunge watano kati ya kumi na moja wametoka kaskazini!! Hapo hatujamchanganya Mama Komu ambae anajidai mzanzibari mwenye asili ya uchaga na Mwanasiasa nisaidie Halima anatoka wapi.


...





sasa TTJ nadhani ukiendelea na msimamo huu wa kuargue based on data from Website ya CHADEMA basi nadhani tutafika mbali na hhivi ndio namna ya kendesha mjadala

safi sana

then tutahamia kuwauliza maswali wale CUF nao wapate kuweka mambo yao sawa
 
DrWHO,
Na wewe nakusubiri ueleze "beef " yako na FDR.


nenda katika THREAD aliyoanzisha MBOWE kisha utajua nani hajamjibu mwenzie

niliambiwa na Mwanasiasa atarudi kuweka mambo sawa lakini kimya..nadhani huyo Chinga bado anamshughulisha

Mbowe ndio hakuniju babisaaa

labda huyo JJ ambaye naona kawa kimya
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom