Form Vi For President - No Way
Quote:
Originally Posted by mwanasiasa
Wacha: unataka kusema kuwa kiongozi lazima awe na elimu kubwa ndio ajali elimu? Hii ni hesabu ya wapi? Kuna viongozi wengi duniani ambao elimu zao zilikuwa za kawaida na bado walifanya maajabu katika maendeleo ya elimu na kinyume chake pia ni kweli. Mfano mzuri ni nyumbani TZ; Mzee Mwinyi alinyanyua sana elimu ya juu.
Ni kipindi chake ndipo idadi ya wanafunzi iliongezeka katika vyuo vya elimu ya juu na kipindi chake pia vyuo vikuu vilingezeka. Lakini alipokuja Mkapa akakubaliana na mapendekezo ya IMF na dadake WB kuwa nchi kama Tanzania ilikuwa haitaji elimu ya juu. Wakamshauri awekeze tu katika elimu ya msingi. Ni katika kipindi hiki tulishuhudia elimu ya juu ikiminywa na vyuo vya serikali viliishi kwa shida na vingine vilibaki kaputi kabisa. Sasa nani ana elimu kubwa kati ya Mwinyi na Mkapa?
Ndio nilisema hapo juu kuwa mantiki ya hoja zako bado naitafuta. Labda nitaipata kadiri ninavyosoma post zako.
Halafu tusipotoshe mambo. Pamoja na kwamba naunga mkono kina JJ kwenda shule, sio kweli kwamba kina JJ hawana elimu ya kutosha. Form Six ni elimu kubwa bado kwa kiwango cha wanasiasa wa Tanzania.
Wanahesabika wenye Form Six hata katika rank za uongozi wa kisiasa wa nchi yetu. Kabla sijaendelea, naomba unitajia kiwango cha elimu alicho nacho Katibu Mkuu wa CCM Makamba.
Hatuwezi kuwa na kiongozi wa nchi ambaye ni form VI period.
Unafahamu ukisikia watu wanasema Bush hakusoma, John Major hakusoma, sio kwamba shule hawakwenda kabisa – walikwenda lakini kichwani hamna lolote (ndio hivyo hivyo tena) uelewaji wao wa masuala ni mdogo. Pia kuna msemo elimu haina mwisho, ndio kusema kila siku unajifunza na hii ni tabia tu. Kama wewe hukwenda shule sawa sawa tabia ya kusoma na kujifunza huiwezi ndio kitu ninachoongelea. (samaki mkunje angali mbichi)
Tatizo ambalo naliona kwa mwenyekiti wako ni pale anapotaka watanzania wamkubali kwamba naye amesoma ili apate cheo. Lakini ukweli utabaki pale pale hiyo degree itakuwa uchwara. Huhitaji hesabu kulijua hili.
Ukiangalia chadema sasa hivi kwa maelezo yako uelewaji wenu ni finyu ndio sababu mnaingia kichwa kichwa tu na Conservative Party siasa za chama hiki zinaeleweka fika tangu enzi hizo na mara ya mwisho natumaini unamkumbuka vizuri Iron Lady kama walivyokuwa wanamuita. Kumbuka vile vile mkutano wake na nchi za Jumuiya ya madola kule Zambia kabla Zimbabwe haijapata uhuru wa bendera. Kuelewa haya huhitaji kupiga hesabu.
Chama kinachokuwa bega kwa bega na Conservative ambao kila siku hawapendi maendeleo ya mtu mweusi na vile vile wanakampeni chafu ya kuwazuia waafrika kwenda UK, lakini wao kuja kwenye nchi zetu ni sawa na halali yao kutuibia na kujichana. Uliza mtoto wa Iron Lady baada ya uhuru wa South Afrika kwa nini aliamua kuhamia kule? Hadi pale matatizo yalipomsibu. Sasa hizo ndio sera za Chadema kutaka kuturudisha kule ambako tulikataa miaka ya nyuma. Conservative ni chama cha wenye nacho na nyinyi kwa ukosefu wa kuelewa mambo (mambumbumbu wengi) ndio sababu mnakumbatia mshiko bila kufahamu maana yake. Ndio sababu nilikuuliza wasomi katika Chadema ni kina nani?
Maana siwafahamu? Wewe unapindua kibao na kuniuliza suala la Makamba na CCM pamoja na uozo wao, waulize wakupe majibu, mie sio msemaji wao na vile vile sina sababu ya kushabikia Chadema ati kwa sababu kuna uozo CCM, vile vile nao wana wasomi ambao ni pungufu katika uelewaji wao na hili halihitaji kupiga hesabu yeyote kulielewa. Siwezi kuruka mkoja kukanyaga m*
Wewe ndio unataka nijiunge na Chadema hivyo inabidi ujieleze sawasawa ili niweze kujua kulikoni, lakini kwa kutoelewa kwenu mambo siwezi kujiunga wala kuwapa support.
Hao CCM unaowaogopa tutawaondoa lakini si kwa kupitia Chadema waliooza.
Ulitaka maswali rahisi hata hayo rahisi unajichanganya. Mmeanzisha chama lazima kiwe makini kwani usanii kama wa CCM hatuutaki, lakini nyie mnaojiunga na Conservative Party ni moto wa kuotea mbali.
Wacha